Ati Funga ya Ramadhani ya Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Tanzania ni Batili

 

Adeladius Makwega-MBAGALA.

“Wizara ya Mambo ya Nje ni idara ya serikali inayohusika na kuendesha sera ya nje ya taifa lolote lile, kusimamia mahusiano ya kimataifa, na kukuza maslahi ya kitaifa nje ya nchi. Majukumu yake makuu yanajumuisha uwakilishi wa kidiplomasia, kujadiliana mikataba, kulinda raia walioko nje ya nchi, kuendeleza maslahi ya kiuchumi, kukuza ushirikiano wa kimataifa, na kutoa huduma za itifaki.”

Huku majukumu muhimu ya Wizara hii ni:

Uundaji na Utekelezaji wa Sera ya Nje: Kubainisha na kutekeleza malengo na mikakati ya sera ya nje ya taifa. Pili, mahusiano ya Kidiplomasia: Kusimamia mahusiano na mataifa mengine na mashirika ya kimataifa (mfano, UN, EAC). Tatu, Uwakilishi Nje ya Nchi: Kuendesha balozi, ofisi za ubalozi mdogo (konseli), na misheni za kudumu, pamoja na kusimamia wanadiplomasia wa kigeni. Nne, Kulinda Raia na Maslahi yo: Kutoa huduma za kikonseli, kulinda usalama wa taifa, na kukuza maslahi ya raia walioko nje ya nchi. Tano, Mikataba ya Kimataifa: Kujadiliana, kusaini, na kusimamia mikataba ya pande mbili na ya pande nyingi. Sita, Diplomasia ya Kiuchumi na Kiutamaduni: Kukuza biashara, uwekezaji, na mabadilishano ya kitamaduni. Saba ni Huduma za Itifaki: Kusimamia ziara rasmi, hadhi za kidiplomasia, na kinga za kidiplomasia. Nane Utoaji wa Taarifa: Kuelimisha umma kuhusu masuala ya kimataifa na ushirikiano wa kikanda, kama vile Jumuiya ya Afrika Mashariki.”

Hapa Mwanakwetu anasoma makala moja iliyoandikwa mtandaoni juu ya Wizara ya Mambo ya Kigeni .

Kwa tathimini ya Mwanakwetu kulingana na majukumu ya wizara hii anaona kuwa chini ya Mtoto wa Thabiti Kombo ni kipindi pekee ambapo Tanzania imebebeshwa tuhuma kadhaa za ndani na kimataifa ikiwamo matukio ya ulawiti, ubakaji, utesaji, upoteaji wa watu na hata mauwaji ya makundi kadhaa ya waandamanaji, huku majina kadhaa yakitajwa kufanya haya mabaya na waliofanyiwa hivyo ambao wameponea tundu la sindano wakipaza sauti zao na wakiwasonda vidole watu kadhaa kwa majina yao, majina ya baba zao na majina ya babu zao.

“Hadi sasa Mtoto wa Thabit Kombo amejibu nini? Mtoto wa Thabit Kombo ameshauri nini? ”

Mwanakwetu anaona kuwa kwa maelezo yanayotolewa na Mtoto wa Thabit Kombo inaonesha wazi yeye binafsi anashabikia haya mambo ya aibu na hachukizwi nayo. Waziri wa Mambo ya Kigeni alipaswa kuonesha moyo wa kiungwana katika hali kama hii na kama haya mambo yanaendelea kwa heshima ya baba yake ThabitiKombo, ndugu yetu Mahmoud angejiuzulu.

Msomaji wangu kumbuka Mwanakwetu anasoma maoni juu ya wizara ya Kigeni ya Tanzania huku akiitafakari kwa kina juu ya wizara hii. 

 

Mwanakwetu anasema nini siku a leo?

Kwa hakika kulingana wasifu wa Waziri wa sasa wa Mambo ya Kigeni wa Tanzania ambaye ni Mtoto wa Thabit Kombo inadaiwa alizaliwa Julai 8, 1970 na kwa hadi Julai 8 , 2026 anatimiza miaka 56, huyu ni mtu mzima mwenye watoto na pengine kujukuu lazima kila hatua ya Uwaziri wake itumike kuwaponya Watanzania na kuijengea Tanzania jina zuri kwa faida ya kizazi chake na Watanzania wote, kauli zake ziwe za umakini maana jina Thabit Kombo siyo jina la kuchezewa shere lazima yeye mwenyewe atambue kuwa anawajibu wa kulinda heshima ya mzee wake kwa kila hatua anayofanya na kila analotamka.

Wakati Mwanakwetu anakamilisha makala haya haya mdau mmoja alikuja nyumba ya Mwanakwetu akasoma haja moja ya makala haya kisha kusema maneno haya:

“Mahmoud hata kama anafunga Ramadhani hii, funga yake ni batili, anashinda njaa tu… anajichosha tu, kwanza ajiulize yeye anafunga Ramadhani, Polepole yupo wapi? Ajiulize Oktoba 29, 2025 kulitokea nini? Labda Mungu amsogezee neema ya toba…vinginevyo funga zote za Ramadhani za Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Tanzania ni Batili…”

Mwanakwetu akacheka sana maneno haya ya kuibatilisha Ramadhani ya mheshimiwa Mahmoud Thabiti Kombo akasema kama kwa Mahmoud mambo ni hivyo kwa wale wengine mambo yakoje? Je kuihalalisha Ramadhani ya Mahmoud Thabiti Kombo afanyaje? Jamaa akacheka akisema ili ni darasa la siku nyingine lazima Mahmoud Thabiti Kombo apige upya Shahada.

 

Mwanakwetu akasema maneno haya:

“Ndugu yangu Mahmoud Thabiti Kombo njoo ule nyama ya nguruwe iliyookwa vizuri nyumbani kwa Mwanakwetu maana Ramadhani yako wanazuoni wa dini ya Kiisilamu nduguze Mwanakwetu wameibatilisha wameiharamisha tayari.”

Ndugu huyu alipoondoka kando ya Mwanakwetu nayeye Mwanakwetu kuyaongeza maneno haya katika makala yake kama yalivyo

Mwanakwetu Upo? Kumbuka

“Funga ya Ramadhani ya  Waziri wa Mambo ya Kigeni Tanzania ni Batili.”

Nakutakia siku njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257

 

 

 

0/Post a Comment/Comments