Watumishi Wote Waliondolewa Kwa Vyeti Feki Wamepewa stahiki Zao -PSSSF

Adeladius Makwega-MBAGALA

Majira ya asubuhi ya Januari 22, 2026 Mwanakwetu anapokea maagizo haya:

“Nenda mtaa wa Mkendo kuna kikao baina ya PSSSF na wanahabari wetu wa Mkoa wa Mara kashiriki.”

Mwanakwetu alibeba begi lake na kuianza safari hii haraka.

Msomaji wangu wewe kama mgeni na mji wa Musoma Mtaa wa Mkendo upo Wilayani Musoma ambapo ni mtaa wa katikati ya Manispaa ya Musoma ambapo ndipo Makao Makuu ya Mkoa wa Mara , huku neno Mkendo likitokan ana jina la Mlima Mukendo ulio jirani na Ziwa Victoria kando na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara ambapo ukiwa Ziwa  Victoria hauwezi kuuona mji wa Musoma maana Mlima Mukendo unamzua mtu aliye ziwani kuuona mji huu.

Mwanakwetu alifika katika mafunzo haya huku maneno haya yakisikika:

“Hap hata wale waliondoka katika utumishi wa umma wamepata haki zao zote maana hata ukiangalia mfumo wa malipo wetu(PSSSF) unaonesha huyu ABCD ameondolewa  kutoka na vyeti feki na malipo yake ameyapokea. Kwa mafunzo haya natoa ilani kama yupo mtumishi ambaye hajachukua haki zake atembelee ofisi za PSSSF ataelekezwa namna ya kufanya apate haki zake.”

Haya yalikuwa maneno yaliyomkaribisha Mwanakwetu katika ukumbi ambapo mafunzo ya PSSSF yanayotolewa kwa wanahabari zaidi 50 wa mkoa wa Mara ambapo maeleziohaya yalitolewa na haya hapa ukumbini na ndugu Nuru Mahinya ambaye ni Kaimu Meneja wa PSSSF mkoa wa Mara ambapo alijibu swali ya mwanahabari Augustine Mgeni kutoka Azam Televisheni.


 

Wanahabari kadhaa wa Mkoa wa Mara walipata wasaa wa kuuliza maswali na kujibiwa huku shabaha ya mafunzo haya ni kutoa elimu hii kwa wanahabari ili hii elimu iweze kuwafikia wanachama wa mfuko huu mkoa wa Mara na Tanzania nzima kwa ujumla wake.

Baada ya haya Mwanakwetu akaamua kuyaandika haya kama yalivyo katika makala haya

Wakati haya yakiendelea hapa Musoma Mjini hali ya hewa ya mji huu ni nyuzi joto 27, unyevunyevu ni wa asilimia 10, ujirani na mvua ni wa asilimia 51 na upepo ukivuma kwa KM14 kwa saa.

Mwanakwetu upo?Kumbuka

“Watumishi wote Waliondolewa Kwa Vyeti Feki Wamepata Haki zao.”

Nakutakia Siku Njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257





 

 



0/Post a Comment/Comments