Adeladius Makwega-MBAGALA
Mwaka wa 2002 Serikali ya Tanzania ililivunja Jiji la Dar es Salaam na Kuunda kitu kinachoitwa Tume ya Jiji la Dar es Salaam, baada ya kuona mambo hayaendi sawa, kipindi hiki kazi kubwa sana ilifanywa na Tume ya Jiji hilo iliyokuwa inaongozwa na ndugu Charles Keenja na alama ya mfano ni ujenzi wa Shule ya Sekondari Benjamin William Mkapa-BMW Sekondary School katika ya Jiji hili ambayo ndiyo shule ya kwanza kubwa kujengwa Mkoani Dar es Salaam kwa kutumia fedha za mapato ndani ya watu Dar es Salaam tangu uhuru.
Kwa wale watu wa Dar es Salaam wezangu na hata wale ambao hawalifahamu eneo hili vizuri naomba nieleze hiki:
“Eneo ilipo BWM Sekondari ilikuwa ni viwanja va wazi vya michezo kwa Shule ya Msingi ya Uhuru Wasichana (Girls School) na Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko ambapo pia ilikuwa ni Shule ya uhuru Vipofu. Viwanja hivi zamani hata timu ya Simba ilikuwa inafanya mazoezi na hata jamaa wa matopeni FC Yanga African kule Jangwani Uwanja wa Kaunda ulipokuwa ukijaa maji walitumia viwanja hivi jirani na Uhuru Mchanganyiko.”
Ndugu yetu Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Wililam Mkapa na Waziri wake Mkuu Fredrick Sumaye walifanya kazi nzuri sana na kulivunja Jiji la Dar es Salaam na hii ilitoa picha ya hali ilivyo ndani ya Serikali za Mitaa.
Kwanini Mwanakwetu ameyakumbuka haya yote ?
“Vijana wawili wadogo Serikalini walikuwa wamekaa wanaongea,’Sisi tunapata pesa za uendeshaji wa ofisi kwa mwezi karibu milioni 8, hii pesa kila mwezi inakuja lakini ukipiga mahesabu matumizi yake yanachanganya kwanza utaambiwa hii ya utafiti , hii ya kile hii ya hiki watumishi wadogo tunapata kidogo sana. Ukijumlisha malipo yote mkubwa anapata karibu milioni tano na ushehe haya yanafanyika kila mwezi.
Ukitaka kuona kuwa kuna hila mkubwa hata kama anakwenda likizo hawezi kuondoka hiyo likizo hadi agawe fedha za uendeshaji wa ofisi na akirudi lazima akute fedha uendeshaji haijagawiwa agawe yeye. Kama fedha hii inagawiwa vizuri na hakuna hila basi angeruhusu wengine waigawe siyo yeye kila mara.”
Mdau mwingine hapo akasema unajua haya mambo ndiyo maana Rais wa Awamu ya Tano marehemu John Pombe Magufuli alikuwa hapeleki fedha ya uendeshaji wa ofisi za umma katika baadhi ya taasisi maana alijua kuwa kuna hila ndani yake, yule baba alikuwa sahihi, yule baba alikuwa sahihi.
Mdau mwingine akasema hoja ya kutokupeleka fedha katika taasisi sikubaliani nalo kikubwa wale walipewa majukumu watimize wajibu wao .
“Mathalani mkoa A umepokea fedha ya uendeshaji wa ofisi shilingi milioni 200 kwa mwezi C. fedha ikishapokelewa Kamati ya Bajeti inaketi kujadili fedha hii iliyopokelewa. Kamati hii ya Bajeti inakuwa na Maafisa Bejeti wa taasisi husika na wakuu vitengo na sehemu, kabla ya kujadili kupokea fedha hizo za uendeshaji lazima wajadili fedha waliyoipokea awali kwa mwezi uliyotangulia je ilitumikaje? Kifungu kwa kifungo na kama kulikuwa na itilafu kipi kilitokea na utatuzi ni nini? Ndipo wanakuja katika kujadli mapokezi ya fedha iliyoletwa kwa mwezi A. Kikao hiki kinakuwa na muhtasari wake maana yake lazima kuwepo na faili lenye mihutasari hiyo ya kila mwezi.
Hapa malalamiko kuwa fulani anajigawia fedha zaidi, anajipendelea kama yatakuwepo yatajadiliwa mwezi mmoja tu na mhusika atachukuliwa hatua, shida hiyo haiwezi kuwepo tena.”
Kumbuka jamaa hawa wanaongea ndugu huyu wa mwisho akaongeza na hili:
“Katika taasisi nyingi kuna mtu anaitwa Mkaguzi wa Ndani lazima awe makini na asiwe mtu wa maslahi binafsi. Hapa mkaguzi anaweza kujiuliza je Kamati ile ya Bajeti inakaa kila mwezi? Je kama inakaa inajadili nini? Kama haikai ni kwanini? Kama kamati hii haikai maana yake mchezo unachezwa na mtu mmoja ! Je fedha ya uendeshaji ya kila kitengo na sehemu inatumika kulingana na mpango kazi? Mkuguzi wa Ndani anaweza kujiuliza je Vikao vya Vitengo na Sehemu vinafanyika? Je malalamiko ya wafanyakazi ni nini? Kikao cha mwezi A watumishi walilalamikia nini kama shida ya mgawo wa fedha ya uendeshaji, mwezi B hilo hilo na huku linawekwa katika muhtasari lazima litafanyiwa kazi lakini kama vikao havifanyiki na Mkaguzi wa Ndani yupo yeye Mkaguzi wa Ndani ndio mwenye shida.”
Mjadala huu ulikuwa mzuri sana huku Watanzania hawa wakiizungumzia Serikali yao na namna bora ya uendeshaji wa mambo na hapa yeye Mwanakwetu akaamua kuyabeba haya kama yalivyo na kuyaweka katika makala haya.
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
Kwa hakika utaratibu wa uendeshaji mambo serikali ni mzuri sana changamoto ni sisi wanadamu . Kikubwa kila mmoja ajue kuwa serikali ni mimi wewe na yule. Mtu mmoja akiweka maslahi yake mbele serikali nzima inabebeshwa mzigo. Hapa kila mmoja wetu aliyeopo serikalini ajitafakari.
Kwa wale wakubwa taasisi ni vizuri kujua hizo pesa za uendeshaji wa taasisi kwa vitengo na sehemu zinatumikaje? Ni vizuri vikao vikafanyika na kuwekwa katika muhtasari na kama kuna malalamiko yafanyiwe kazi.
Huku Wakaguzi wa Ndani watimize wajibu wao mathalani kwa Wakaguzi wa Ndani Ngazi ya Mikoa wanasimamia Halmashauri chini yao ambazo zina watu wengi mathalani kama Mkaguzi Ngazi Mkoa vitengo au sehemu zake hazifanyi vikao vya wafanyakazi wake kila mwezi unadhani hali itakuwaje kwa ngazi ya Halmashauri, Ngazi ya Tarafa, Ngazi ya Kata, Ngazi ya Kijiji na Ngazi ya Kitongoji?
“Watumishi wa Ngazi ya Mikoa hasa Wakuu wa Vitengo na sehemu hawapaswi kukaa kituo kimoja muda mrefu na kama haya mabadiliko yatafanyika yatasaidia taasisi husika kufanya kazi na watu tafauti tofauti, wenye ujuzi tofauti na kubadilishana uwezo na kupunguza madhaifu.
Unaweza kuwa na Mtumishi wa Umma anakaa pahala muda mrefu Dondora wanajenga katika ofisi yake haoni, chumba chote kinajaa dondora hawaoni. Mkaguzi wa Ndani makini lazima ajue hata kama Dondora wanatakaja kujenga katika ofisi yake ajue ili kuhakikisha anadhibiti ofisi yetu ili iwe salama kama ilivyokuwa Kwa Tume ya Jiji la Dar es Salaam enzi ya Mzee Mkapa, maana Shabaha Watanzania Wasiumwe na Madondora.”
Mwanakwetu upo?Kumbuka:
“Watumishi wa Umma Wasiumwe na Madondora.”
Nakutakia Siku Njema.
0717649257
NB MAKALA HAYA NI ZAWADI KWA WAZIRI WA TAMISEMI PROFESA RIZIKI SHEMDOE






Post a Comment