Adeladius Makwega-MBAGALA
Ni majira ya asubuhi ya Alhamisi ya Januari 9, 2026, Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Evans Alfred Mtambi anapokea sehemu ya Wajumbe wa Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yalitokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 nchini Tanzania, taifa la Afrika Mashariki.
“Magari mawili meusi yanaingia katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, kisha anashuka baba mmoja mrefu sana aliyevalia suti nyeusi na mama mmoja mrefu wa kadili aliyevalia maridadi na kusalimiana na Mkuu wa Mkoa kisha kuwasalimu Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mara, wakiwepo wote bila uwakilishi, alafu wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mara walitawanyika na kisha Mkuu wa Mkoa kuongoza ugeni huu kuingia ofisini mwake.”
Ndani ya ofisi hii ya Mkoa wa Mara walingia wajumbe hawa wawili na jamaa wengine; mmoja mtu mzima na mwingine kijana waliovalia suti zinazoshabiana, hawa wajumbe, kwanza yule mama alisaini vitabu vitatu vya wageni kisha yule baba kusaini vitabu vitatu vya wageni.
Mkuu wa Mkoa wa Mara akatoa maelezo yake mafupi juu ya Mkoa wake ambayo mara nyingi anapopokea wageni huyafanya .
Kisha mama yule Mjumbe wa tume akajitambulisha kwa sauti ya chini kidogo lakini neno lililosikika na mwandishi wa makala haya ni BALOZi na hata mjumbe wa pili yule baba mrefu alitajwa Balozi na majina yake mawili na kisha wajumbe hawa kwenda katika ukumbi maalumu walipokuwa wakikutana na waliwahoji.
Mazingira ya nje ya eneo hili ambalo wale wajumbe wawili walikuwa wakikutana na wanaowahoji yalionesha kuwa na hekaheka za ingia toka ya watumishi kutoka Vyombo vya Ulinzi na Usalama kama walikuwa wakihojiwa wao.
Mazungunmzo yao nje ukiwashitukiza walikuwa wakiulizana maswali kadhaa wenyewe kwa wenyewe:
“Kwani wanahoji nini.”
Jamaa mwingine alijibu
“Kuna kweshenia.”
Hii ndiyo hali aliyoibaini Mwanakwetu siku hii.
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
Kwa hakika ni kweli tume ipo kazini na sasa imekanyaga mkoani Mara na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Mtambi na Katibu Tawala Mkoa wa Mara Mwalimu Gerald Musabila Kusaya.
Mwanakwetu akiwa hapa alichunguza hii tume inafanya kazi na akina nani tangu ilipoteuliwa?
Wakati Kanali Mtambi anazungumza nao wajumbe wale wawili kumbuka walikuwepo watu wagine wawili kijana mmoja na mtu mzima mmoja ambaye alikuwa akiingia na kutoka ofisini .
Kwa utafiti wa Mwanakwetu alibaini kuwa mmoja alikuwa ni mtumishi wa Ikulu mwingine alikuwa hamfahamu, kuhusu madereva wa magari haya mawili hawakujaliwa kushuka garini siku nzima, hivyo hawakuweza kutambuliwa ni kina nani?
“Kwa kitendo cha kukaa ndani ya gari muda wote hii iIitoa ishara kuwa ni madereva kutoka Vyombo vya Ulinzi na Usalama maana huwa wana tabia hii.”
Msomaji wangu nilijikita kujua hawa wasaidizi wa wajumbe wa tume ni kina nani nilikuwa na hoja nyingi.
“Nilipokuwa nalitazama hili nilikumbuka kuna wakati Jimbo Katoliki la Same kulitokea changamoto za mwenendo nadhani wa Askofu Jacob Koda ambaye alikuja kujiuzulu nyadhifa hiyo, nadhani Askofu Mstaafu Koda alijiuzulu kutokana changamoto hizo. Mwanakwetu nilisoma Same sekondari mwaka 1994-1995 na wakati huo lile Kanisa Uaskofuni ndiyo linajengwa na baadhi ya Wakatoliki wa asili wa Same niliyosoma nao shuleni ambao walikuwa wana TYCS niliwauliza shida ni nini? Vatikani ilituma tume kuchunguza mwenendo wa Baba Askofu huyu na baadaye Jacob Koda alijiuzulu .
Sehemu ya timu ile ilikuwa na wajumbe akiwemo Askofu Lebulo ambaye ni mzaliwa wa Same kutoka TEC ambaye alikuwa Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha wakati huo na wajumbe wengine kutoka Vatikani.”
Ni kweli tume lazima iwe na wasaidizi lakini watu hao ni kina nani na wanatoka wapi?
“Mathalani Askofu Mstaafu Jacob Koda angejichunguza mwenyewe, mapadri wake na masista wake hili vigumu, hili ni gumu na ndiyo maana Vatikani ilituma timu maalumu na nakumbuka Mwanakwetu nilishakuwa mwanahabari wakati huo na niliandika Makala Vatikani Iseme Askofu Koda Kafanya nini?”
Iwe wajumbe wanauliza maswali kwa mdomo au kwa kweshenia kikubwa huyu mtu anayewasadia kazi kama kukusanya maoni haya ni mtu wa namna gani? Anaweza kulinda maslahi mapana ya taifa? Siyo wale wale walioshauri na waliyotufikisha hapa?
Wajumbe wa tume ni baba na mama zetu lazima tujue na walio karibu nao katika kazi hii je ni watu wema? Ni watu waadilifu? Maana waharifu wa leo hawana heshima , hawan adabu ni watu punguani maana mpaka leo hatujui alipo Balozi wa zamani wa Kuba ndugu Polepole.
Mwanakwetu upo? Kumbuka
“Wajumbe wa Tume Wanafanya kazi na Watu wa Namna gani?”
Nakutakia Siku Njema.
makwadeladius @gmail.com
0717649257








Post a Comment