LINDA UHAI WAKO NA WA WENGINE

 


Adeladius Makwega-MBAGALA

“Matumizi ya hukumu ya kifo yaliongezeka sana duniani mwaka wa 2025, hasa kwa sababu watu wengi waliuawa kwa makosa ya dawa za kulevywa ambayo hayahusishi mauaji ya kukusudia-Hii ni kinyume na sheria za kimataifa na halisadii kuzuia uhalifu .”

Anasema Mkuu wa haki za binadamu wa umoja wa Mataifa Volker Turk.

Januari 21, 2026 Ukurasa wa Mitandao ya Kijamii wa Umoja wa Mataiafa umemnukuu kwa maneno haya Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia haki ya binadamu Volker Turk akizungumzia mapambano ya kutokomeza Hukumu ya Kifo.

 

Mwanakwetu alipoisoma taarifa hii akilini mwake yalimjia mambo matatu:

|Kwanza ni jina la Said Abdallah Mwamwindi ambaye alikuwa mkulima wa mahindi aliyemuwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa IringaDkt Wilbard Kreluu Disemba 25, 1970 wakati wa vijiji vya UJAMAA pale Mkungugu Isimani Tarafani Iringa Vijijini mkoani Iringa.Mwanakwetu kwa kuwa alifanya kazi katika eneo hili kati ya mwaka 2004-2009 kama Afisa Elimu Msaidizi Daraja la tatu katika Shule ya Sekondari Isimani Tarafani Wakati huo ilikuwa chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ambayo ilikuwa shule iliyowapokewa wanafunzi wengi kutoka eneo hili ambalo tukio hili lilitokea.Wanafunzi mmojawapo anayemkumbukwa na Mwanakwetu anaitwa al ustadh Mwinyi Kasike ambaye pia Shule ya Sekondari Isimani wakati huo alikuwa kiongozi wa wanafunzi Waisilamu aliyasema maneno haya:

“Wazee wetu wanasema tukio hili lilipotokea wanakijiji wengi wa Mkungugu walikamatwa ili watoe ushahidi upande wa Jamhuri na ndugu wengi walikimbia kijijini hapo na kwenda maeneo mbalimbali ya Mkungugu kukataa kutoa ushahidi maana walijua ushahidi utakatolewa ulikuwa unasaidia Said Abdallah Mwamwindi ndugu yao ili anyongwe, kitendo hiki kilikuwa kama kinaongeza chuki katika Kijiji cha Ujamaa Mkungungu hivyo Kijiji cha Mkungugu koo zile nyingi za asili wengi wao walikimbia kijijini hapo na wengine walifia huku huku ugenini walipokimbilia.Huku tukisikia kuwa wazee wanakwenda kuzika maeneo haya ndugu zao walipokimbilia

Hali hii ilifanya kijiji cha Mkungungu kuzorota sana kimaendeleo maana walibaki vikongwe, maajuza akina mama na watoto.”

Ndugu Kasike alisema anaamini kuwa miongoni mwa Watanzania walinyongwa wakati huo mara baada ya rufaa ya Said Abadallah Mwamwindi kushindwa ilikuwa ndugu huyo.











 

Jambo la pili ambalo Mwanakwetu alikumbuka baada ya kusoma nukuu hii ya Umoja wa Mataifa ni Utafiti wa Bi. Neema Chusi ambaye alikuwa mwanachuo cha Chuo Kikuu cha Tumaini Iringa Kitivo cha Sheria mwaka wa 2002 katika utafiti juu ya Hukumu ya Kifo Imepitwa na wakati, Bi chusi alisema maneno haya:

“Kitanzini mkoani Iringa palikuwa pahala ambapo Mwarabu, Mjerumani na baadaye Mwingereza alikiwa akipatumia kinyongea watu. Kwa hiyo Wahehe, Wabena na Wakinga wakati huo walipoambiwa unakwenda kintanzini maana yake ilikuwa wanapelekwa kunyongwa na hali hii iliongeza chuki katika jamii.”

Kisa cha tatu alichokumbuka Mwanakwetu kilikuwa hiki:

“Daktari mmoja alikwenda kumuona mgonjwa ambaye alikuwa Mkristo mshika dini yake kweli kweli wa dhehebu la Lutherani, mgonjwa huyu mshika dini alikuwa amezidiwa sana na hali ilipokuwa mbaya hamu ya chakula ilikuwa haipo na hili likafanya afya yake ikazorota mno. Daktari ambaye pia ni muumini wa Kanisa la Kinjili la Kilutheri la Tanzania akamwambia mgonjwa wake kuwa nakuomba ujitahidi ule chakula maana kutokula chakula ni sasa ni kujiua mwenyewe na kitendo hiki ni dhambi sisi kama Wakristo, haukuitenda kabisa dhambi hii ukiwa na nguvu, iweje uitende dhambi hii ukiwa mgonjwa na tena kwako mwenyewe? Kweli mgonjwa yule alianza kula chakula na alipata moyo na kuanza kula chakula chake vizuri kwa dhana ile ya kushika imani yake ilimsaidia mgonjwa kupata nguvu japokuwa baadaye alifariki dunia lakini siyo kwa kukacha kula chakula alifariki kwa maradhi tu yalikuwa yanamsumbua.”

Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?

Hivyo visa vyote vitatu Mwanakwetu ameivitumia kujenga hoja ya Volker Turk ambaye ni Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayesimamia haki za binadamu ikiwamo kulinda uhai wa binadamu.Mwanakwetu anasema ni jukumu la kila mmoja wetu kulinda uhai wake mwenyewe na mtu mwingine.

“Ni jambo la kichekesho kitendo kile kile kinachokatwaza kufanywa na mtu mwingine alafu mwingine anapewa mamlaka ya kufanya hivyo kisheria kwa mkono wa nyuma hili hapana, hili halikubaliki kuuwa ni kosa kuuwa ni kosa hakuna mjadala.”

Katika hili hata wale wanaobeba silaha iwe katika vyombo vya ulinzi na usalama, wanapotekeleza majukumu yao tangu mdogo hadi mkubwa wawe makini , kulinda uhai wa raia, isiwe kitendo cha kuruhusiwa na sheria kubeba silaha kimfanye mbeba silaha kisheria akawa na kiburi akaona kuwa yeye anamamlaka ya kufanya atakavyo, hili halikubaliki.Kwa hiyo wakati huu dunia inapambana na kufutwa kwa Hukumu ya Kifo hata hili la wabeba silaha kuwa makini liende sambamba na mataifa yatakayoonesha matumizi mabaya ya silaha yasiruhiwe kununua silaha na mamlaka zao ziwe chini ya uangalizi wa Umoja wa Mataifa baada ya kutokea matukio haya, maana historia inadokeza kuwa haki zinapokiukwa kuna kila dalili ya haki zaidi kukiukwa mbeleni.

Mwanakwetu upo?Kumbuka:

“Linda Uhai Wako na wa Wengine.”

Nakutakia Siku Njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257

 

 

0/Post a Comment/Comments