
Adeladius Makwega- MBAGALA
“Mara baada ya eliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Kuba kurejea nyumbani Tanzania na kujiuzulu tu, kiongozi huyu alikuwa akifanya vipindi katika katika mtandao ya You tube na mitandao mingine ya kijamii na taarifa zake kutazamwa na Watanzania kadhaa na ulimwengu mzima huku akizungumza mambo mengi ya Taifa la Tanzania.”
Mwanakwetu alifuatilia kwa kina maelezo ya Balozi Polepole miongoni mwa taasisi alizozitaja sana na kwa jina la kiongozi wa taasisi hii ni TCRA chini ya Dkt. Jabiri Bakari.
“…Jabiri Bakari ni msomi mzuri lakini aangalie hili la Mkata Swichi kila ninapoongea…hili siyo sahihi.”
Mpaka ndugu Humphrey Polepole anatekwa na kupotea neno la MKATA SWICHI limebaki kuwa msamiati mkubwa na huu ukiwa ni mzigo wa TCRA chini ya ndugu Jabiri Bakari.
Swali la kujiuliza je Mamlaka za Mawasilino za mataifa yetu zinafanya kazi bila ya kuzingatia maadili au zinafanya kazi kama wanavyojisikia?
“Udhaifu wa mamlaka ya udhibiti wa mawasiliano mara nyingi hutokana na uhaba wa rasilimali, kuingiliwa kisiasa (kukosa uhuru), majukumu yasiyoeleweka wazi, na changamoto katika kutekeleza uzingatiaji wa sheria. Changamoto hizi zinaweza kusababisha ubora duni wa huduma kwa watumiaji, kudorora kwa ushindani wa soko, na kupungua kwa imani ya wawekezaji.”
Mwanakwetu anapolitazama suala la uhaba wa rasilimali na uwezo ni kweli ukosefu wa ufadhili wa kutosha, rasilimali watu, na utaalamu wa kiufundi, haya hupunguza uwezo wa mdhibiti kufuatilia soko kwa ufanisi, kuchunguza malalamiko, na kutekeleza kanuni na sheria lakini hapa kwa kiasi kikubwa kwa Tanzania tuseme ukweli tangu mwaka 2014 tumepokea misaada kadhaa ambapo sasa kuna maboresho makubwa tazama jambo moja tu wafanyakazi wa TCRA zamani tulimjua Innocent Mungi tu lakini sasa TCRA ina wafanyakazi kedekede, TCRA Imekuwa baba wa ajira , haya yote mazuri lakini malalamiko ya Humphrey Polepole yanakumbukwa?
“…Jabiri Bakari ni msomi mzuri lakini aangalie hili la Mkata Swichi kila ninapoongea…hili siyo sahihi.”
Maelezo haya ya ndugu Polepole yanaonesha kuwa taasisi za udhibiti mawasiliano hazijalindwa ipasavyo dhidi ya ushawishi wa kisiasa au shinikizo kutoka kwa sekta husika ambapo viongozi wamekuwa na ulimbo wakizinasi vilivyo taasisi hizi kwa maslahi yao wenyewe ya kisiasa, huku wakifanya maamuzi yanayowapendelea maslahi yao badala ya maslahi ya umma wa walio wengi, jambo linalopunguza imani ya wananchi kwa taasisi kama TCRA.
“Hili ni tatizo ambapo Tanzania imejifunza na kushuhudia kwa kina na Oktoba 29, 2025 na siku zilizofuata na ni ushahidi wa kila Mtanzania mwenye kumiliki simu janja ambapo mitandao ilizimwa.”
Hapa pia kuna majukumu yasiyoeleweka au Yasiyo thabiti: Ufafanuzi usio wazi wa wigo wa udhibiti, majukumu yanayoingiliana na taasisi nyingine za serikali, au kanuni zinazokinzana vinaweza kusababisha mkanganyiko na mianya katika utekelezaji.
Kwa sasa Mwanakwetu anaamini kuwa TCRA inaonekana kuwa ni dhaifu na goigoi ikifanya kazi kama mamlaka ya Kipolisi, mara kuzima, mara kufungia mitandao. mathalani Tanzania ilishuhudia kufungiwa kwa Mwananchi Comunication kisa kikiwa katuni tu inayowagusa viongozi na hata kufungiwa kwa Jamii Forum.
Bila mifumo madhubuti ya uchunguzi wa umma, utoaji wa taarifa kwa uwazi, na mapitio ya kimahakama, wadhibiti wanaweza kuwa wazembe au kupunguza ufanisi wao wakijiamulia mambo wakiona wao ndiyo sheria wao na wao ndiyo mahakama, hakuna wa kuwafanya lolote lile.
Nani kaidanganya TCRA kuwa wao ndiyo kila kitu?
“Kibaya zaidi TCRA kwa sasa inalaumiwa mno kuwa na mawasiliano duni na wadau mathalani TCRA inafanya usajili, wamekuwea wavivu wa kupigia simu kuongea na wadau juu changamoto wanazokutana nazo. Hata kuuliza shida zao ni nini, mathalanai kuchelewa kusajili , kwanini hawajafanya usajili? TCRA wangefanya mawasiliano na wadau wangejifunza mambo mengi mathalani usajili ni 500,000 wangewaomba wadau walipe hata kidogo kidogo hadi gharama za usajili kukamilika. Hili linajenga udugu.”
Huu ushauri uliwahi pia kutolewa na Profesa Musa Assad akiwa mkoani Mara wakati tume ile ya namna bora ya Serikali kukusanya ushuru na kodi ilipokuwa inazungumza na wananchi wa mkoa wa Mara.
Katika hili Mwanakwetu anakumbusha haya kwa mamlaka zetu za mawasiliano:
“Kutenda kwa ukweli, kuepuka udanganyifu, na kurekebisha makosa kwa haraka pale yanapojitokeza. Kuwajibika kwa vitendo vyao, kutangaza migongano ya maslahi, na kuendeleza michakato iliyo wazi. Kuhakikisha maamuzi yanakuza ushindani wenye tija na kulinda maslahi ya watumiaji bila upendeleo au ubaguzi na kuwa jirani na wateja huku kufunga mitandao siyo silaha ya maana bali ni silaha dhaifu isiyo na tija katika ulimwengu wa sasa.”
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
Kwa hakika malalamiko dhidi ya TCRA ya Dkt Jabiri Bakari ni mengi na kwa sasa Dkt Jabiri Bakari ameharibu jina zuri la mamlaka ya mawasiliano Tanzania ambapo kwa hakika tangu mwaka wa 2014 TCRA ilifanya kazi nzuri wakati Tanzania inahama kutoka analojia kwenda digitali ambapo Watanzania wengine waliifanya kazi hii kwa ueledi. Inawezekana wapo wanaomkumbatia Dkt Jabiri Bakari kwa maslahi yao ya kisiasa hili ni sawa lakini Dkt. Jabii Bakari kwa maslahi makubwa ya Tanzania tangu kwa wananchi mmoja mmoja hasa kwa kile kitendo cha kuzima mitando TCRA imeingizwa topeni, huku ikionekana kuwa TCRA inashilikiana na watesi wa wananchi. Kimataifa Tanzania imepokea misaada kadhaa ya maboresho yake ya tekinolojia hivyo hata kwa yale ya Oktoba 29, 2025 yanatoa picha kuwa TCRA inaendeshwa kisiasa na hilo siyo jukumu la mamlaka ya mawasiliano Tanzania hilo linakiuka maadili ya mamlaka za mawasiliano ulimwenguni.
Mwanakwetu upo? Je Makala haya yaitwaje? Jabiri Bakari ndiye Mkata Swichi Mkuu? Au Kwa Jabiri Bakari Hatuna Msalie Mtume? Mwanakwetu anachagua kwa Jabiri Bakari Hatuna Msalie Mtume.
Nakutakia Siku Njema.
0717659257





Post a Comment