KILA MMOJA AWE NA MAPENZI MEMA

 


Adeladius Makwega-MBAGALA

Haya ni majira ya jioni ya Januari 26, 2026 Mwanakwetu yu na simu yake ya Kiganjani, gafla anakutana na picha fupi ya video inayowaonesha watawa watatu wa kike: mmoja akitazama umati wa watu, mmoja akipiga makofi, huku mtawa mwingine wa kike ambaye alionekana kana kwamba ni mdogo kuliko wote alikuwa akitazama brass band inayopigwa upande wa mbili wa picha hii ambao haukuonekani, gafla sista huyu akawa anacheka.

Kwa utafiti wa Mwanakwetu inaonekna mtawa huyu hakutarajia kama kuna jamaa aliyekuwa anampiga picha ya video na nadhani picha hii imepigwa kwa kutumia simu akiwalenga hao watawa wa kike wa nchini Tanzania.

Picha hii Mwanakwetu ameipanda sana kwa sababu kubwa tatu:

“Kwanza hawa watawa walikuwa wamependeza mno, pili mtawa anayeonekana mkono wa kulia wa picha ambaye ni mweusi alionekana kweli anafuatilia tukio lililokuwa linaendelea na mtawa wa mkono wa shoto alikuwa analifuatilia tukio hili -nadhani sherehe fulani. Kubwa kuliko yote mtawa wa katikati ambaye ni mdogo alikuwa kweli akili yake yote, macho yake yote, mwili wake wote ulikuwa hapo hapo katika tukio hili akilifuatilia na hata mwisho mtawa huyu akawa na kicheko kizuri sana kwa mpiga picha. Kwa utafiti wa Mwanakwetu kicheko cha mtawa huyu wa kike hakikuwa cha kinafiki, kilikuwa kicheko cha kweli, kwa aliye jirani yake na wala hakukuonesha uadui kwa mpiga picha.”

Kutokana na sababu hizo tatu Mwanakwetu alifuatilia shirika la watawa hawa:

“Masista Wakatoliki wa Katekista wa Maria Imakulata Msaada wa Wakristo (SMI) ambao  ni shirika la kitawa la Kanisa Katoliki lililoanzishwa Desemba 12, 1948 huko Krishnagar, India, na Askofu Louis LaRavoire Morrow, SDB. Shirika hili limejitolea katika uinjilishaji, katekesi, na uwezeshaji wa kijamii, likihudumia jamii kupitia elimu, huduma za afya, na huduma za vijijini, kwa kuishi kwa kauli mbiu: ‘Kumpenda Mungu na kuwasaidia wengine ni kumpenda Mungu.’

Lilianzishwa ili kukidhi hitaji la uinjilishaji wa kina; masista hulenga elimu ya imani, hasa katika maeneo ya vijijini.

Kazi zao zinajumuisha ziara za majumbani, kuendesha shule na zahanati, utume wa vijijini, kuandaa watoto kwa sakramenti, na kusaidia makundi yaliyotengwa.I ngawa chimbuko lake ni India, shirika limepanua utume wake hadi maeneo mengine, yakiwemo Afrika Mashariki hapa wamekuwa wakifanya kazi nchini Tanzania tangu mwaka 1998. Wamejitolea katika huduma ya kichungaji, kufundisha katekesi, ziara za majumbani, na kuendesha kliniki katika maeneo mbalimbali yakiwemo Dar es Salaam, Kibaigwa, na Miyuji huko Dodoma Tanzania wakilenga hasa elimu na huduma kwa jamii.

Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?

Mwanakwetu ni hodari wa kufuatilia mitando ya kijami ya dini kadhaa amebaini kuwa ni madhehebu machache na hata mashirika machache sana ya KANISA yanataarifa zao katika mitandao ya kijamii na hata kama wanazo akaunti kumekuwa na hoja za kibiashara hasa za Kwaya ambapo sasa Kwaya nyingi zimekuwa zikifanywa kama chanzo cha mapato.

“Ili waje waimbe katika harusi lazima utoe pesa, ili waje waimbe msibani lazima ulipe, ili waje waimbe katika jumuiya lazima utoe pesa hili ni sawa lakini malipo yasiwe lazima bali pale mnapoimba mkipewa zawadi ni sawa mkikosa zawadi mnamshukuru Mungu.Hili liwe kama Wakristo wa zamani Katekista, Mwinjilisti ,iwe kwaya Padri, Mchungaji mnamuhakikishia chakula na usafiri na hata zawadi kama mkiweza.”

Mitandoa ya kijamii mingi ya makanisa yetu haiweki taarifa kwa wakati na hata kama zinawekwa bila ubora, mathalani mtu anaiweka ibada nzima kama ilivyo, hili ni sahihi basi baada ya kurushwa moja kwa moja kungetengenezwa vipande vifupi kwa makala maalumu nzuri juu ya misa au ibada hiyo huku vikisambazwa katika mitandao ya kijamii vikiwa katika ubora.

 


Kwa Kanisa Katoliki nakumbuka kuwa Mtaguso wa II wa Vatikani mwaka 1962, 1963 na 1964 walisistiza matumizi ya vyombo vya habari katika nyaraka ile na INTER MIRIFICA. 

 

Msomaji wangu naomba ninukuu sehemu ya viambatisho chini kabisa nyaraka hii kuna maneno haya:

“23. Ili kanuni na miongozo ya jumla ya Sinodi hii takatifu kuhusu vyombo vya mawasiliano ya kijamii iweze kutekelezwa kikamilifu, kwa mapenzi ya wazi ya Baraza, ofisi ya Kiti Kitakatifu iliyotajwa katika namba 19 inapaswa, kwa msaada wa wataalamu kutoka nchi mbalimbali, kutoa maelekezo ya kichungaji.

24. Kuhusu mengineyo, Sinodi hii takatifu ina matumaini kwamba utoaji wake wa maelekezo na kanuni hizi utapokelewa kwa hiari na kutunzwa kwa uaminifu na watoto wote wa Kanisa. Kwa kutumia msaada huu hawatapokea madhara yoyote, bali, kama chumvi na nuru, watatoa ladha kwa dunia na kuuangaza ulimwengu.

Zaidi ya hayo, Sinodi inawaalika watu wote wenye mapenzi mema, hasa wale wanaosimamia vyombo hivi vya mawasiliano, kujitahidi kuvitumia kikamilifu kwa ajili ya manufaa ya jamii, ambako hatima yake inazidi kutegemea matumizi yake sahihi. Hivyo basi, kama ilivyokuwa kwa kazi za sanaa za kale, jina la Bwana litukuzwe kwa uvumbuzi huu mpya, kulingana na maneno ya Mtume: ‘Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo, na hata milele.’

Haya ni maelezo na InterMirifica. Kwa hakika kuna changamoto moja ya vyombo habari muda mwingine kukatazwa kupiga picha, kurekodi matukio hadi kibali.

“Siyo ule wakati wa kuanza MAGEUZO la hasha misa nzima hakuna kupiga picha, hakuna kurekodi. Baadhi ya viongozi wa dini hutoa hoja kuwa bado hawajajiandaa. Mwanahabari anachokihitaji ni yale yale mahubiri na siyo kingine na kikubwa kila mmoja awe na nia njema-kila mmoja awe na mapenzi mema, hoja ya msingi ni Kristo Yesu Mfufuka tu. Iwe Ibada/Misa awe muumini, awe Mwinjilisti, awe Katekista, awe Mchungaji awe Padri, Awe Askofu awe Kadinali awe Papa Mtakatifu shabaha ni Yesu Kristo Mfufuka si mwingine.”

Unapoitazama picha hii ya hawa watawa watatu inatoa tashwira kubwa kuwa Masista Wakatoliki wa Katekista wa Maria Imakulata Msaada wa Wakristo wanakaa kwa amani ndani ya shirika lao, wanapendana na wanawapenda watu walio jirani nao maana watawa hawa wameeneza tabasamu la kicheko , tabasamu la furaha , siyo wamenuna sasa kama wangenuna wanamnunia nani? maana huyu Kristo Yesu mfufuka hapaswi kuwekewa mipaka.

 


Mwanakwetu upo? Kumbuka:

“Kikubwa Kila Mmoja Awe na Mapenzi Mema.”

Nakutakia Siku Njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257







 


 

0/Post a Comment/Comments