KAMPUNI YA JAMBO IACHE KUIVUNJIA HESHIMA EMBE YA MVIRINGE

 



Adeladius Makwega-MBAGALA/SHINYANGA/MARA

Ni majira ya asubuhi ya Jumamosi ya Januari 17, 2026, Mwanakwetu anafika kazini kwake maana kulikuwa na kikao cha kiserikali juu ya maandalizi ya jarida moja la Mkoa wa Mara. Kikao hiki kilitumia dakika chache, kisha kumalizika na ukawa wasaa wa utawala binafsi.

Gafla Mwanakwetu alipokea simu kutoka kwa ndugu mmoja ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe, hili Mwanakwetu alikubaliana nalo kisha ndugu huyo akasema maneno haya:

“Kwanza Mzee Wangu Shikamoo, mimi ni mfanyabishara wa maembe, tunavuna na kununua vijijini,wilayani na mikoa mingine ya Tanzania, hapa nina malori zaidi 10 yangu mwenyewe kisha tunauza hapa Shinyanga katika kampuni ya Jambo. Hawa jamaa wametuweka hapa nje kwa siku kadhaa hadi embe zetu zinaoza, tunaomba utusaidie kupaza sauti zaidi maana wanavyofanya hivi ili embe zetu zioze na wanunue kwa bei ya chini na mzigo mkubwa kwa hasara.”

Mwanakwetu aliwaomba ushirikiano wa wafanyabiashara hawa ili aweze kuzungumzia jambo la haki na lisiwe na uonevu kwa upande wowote ule. Ndugu hawa walisema awali kampuni ya Jambo iliwatumia ujumbe huu:

“Ndugu Mteja wangu, napenda kukutaarifu kuwa Bei ya embe imepanda kutoka shilingi 270 hadi shilingi 300 kwa kilo, Karibu sana Jambo products Shnyanga, Asante.”

Mwanakwetu alitaka kujua Kampuni ya Jambo wanasema nini juu ya hili. Hapa alipatikana Mkurugenzi wa Jambo Food ambaye namba yake ya simu ilifichwa kiasi lakini ipo katika mfumu huu 0767….11 na yeye bila hiana alisema maneno haya:

“Ni kweli tunafahamu kuwa yapo malori kadhaa nje lakini huku ndani tuna mzigo mkubwa, hivyo tunafanya utaratibu ili tuweze kuupokea mizigo yote ya embe na tunanunua na tuliwapa taarifa wakulima wetu.”

Mwanakwetu alipochunguza hali hii alibani kuwa lori lenye mzigo wa embe likiwa na embe ambazo zimevumwa kama lina tani 30 embe hizo zikianza kuiva na kuoza mzigo unapungua uzito kutoka tani 30 inaweza ikaja kuwa tani 10 ambalo hili ni tatizo kibiashara na hili linamnufaishia mnunuzi ambaye ni JAMBO lakini hasara kwa wakulima .




 

Mwanakwetu aliyakusanya haya yote ndipo mwishoni akaamua kuyaandika katika makala haya ili yawafikie wahusika kwa haraka iwezekanavyo ikiwamo uongozi wa Mkoa wa Shinyanga , Wizara ya Kilimo, Wizara ya Viwanda na Biashara na wengine wanaohusika wa hili.

 

Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?

Mwanakwetu anakubaliana na hoja za pande zote mbili lakini hoja ya kuwakalisha nje wakulima na mizigo yao ipo juu ya malori inaonesha hali ya dosari kubwa ambapo ni kuwatia hasara wakulima wetu wa embe nchini Tanzania na hili alikubaliki.

“Hapa wakulima wamelipa ushuru wa halmashauri wa tani 30 magetini, ambapo malipo ya ushuru wa embe yanategemea na halmashauri mathalani Handeni wanahesabu mifuko ya embe –hapa mfuko mmoja ni shlingi 1000, wakati Kilimanjaro wanahesabu ukubwa lori ambapo ni kati ya shilingi 150,000-250,000 (TANDAMU). Hapa bado gharama ya kukodi gari hilo hadi kufika kiwandani na bado gharama la kubaki kiwandani kabla ya mzigo kushuka.”

 

Jambo la pili ambalo Mwanakwetu analiona ni hili, wakulima hawa wamesema kuwa gramu 1000 za embe mviringe zinauzwa kwa shilingi 300 ya Kitanzania katika kiwanda cha jambo ambapo embe ya aina ya MVINGE kwa kimombo ni APPLE MANGO inadawa kuwa inauzwa sana duniani ambapo bei yake ni ya kilo inaanzia kati ya dolla 1-3 kulingana na namna ilivyotengenezwa ambapo dola moja ni sawa na shilingi 2500 ya kitanzania. Ukichukua shilingi 2500 ukitoa shlingi 300 nakisi yake ni ni shilingi 2200 hili halikubaliki.

Kwa suala la bei hii makala haya yanawasilisha moja kwa moja kwa Wizara ya Kilimo ya Tanzania kwa ndugu yetu mheshimiwa Daniel Chongolo popote alipo alifanyie kazi na pia Wizara Biashara watazame angalau kuwasaidia wakulima hawa wa bei ya Kilo ya embe Viwandani ipande nchini Tanzania.

Mwanakwetu katika makala haya anaona siyo busara kutoeleza matumzi ya embe ya MVIRINGE na haya hapa ni baadhi ya matumizi ya embe hizi:

“Embe ya aina ya apple MVIRINGE ni matunda yenye matumizi mengi ikiwamo virutubisho kadhaa ambavyo husaidia kuimarisha kinga ya mwili, afya ya ngozi na mfumo wa mmeng’enyo wa chakula, na kuyafanya yawe bora kwa vitafunwa, juisi, na hata michuzi.Mabichi & Vitafunwa: Yanaliwa kama yalivyo, kwenye saladi za matunda, au yakichanganywa na mtindi. Smoothie & Juisi: Changanya na matunda mengine (kama mchicha au beri) kwa kinywaji chenye lishe bora.Vitafunwa Vitamu (Desserts): Tumia kwenye pai, aiskrimu, pudding, au bidhaa za kuoka kwa kuongeza utamu wa asili.

Vyakula vya Chumvi: Changanya na kuku kwenye saladi, ongeza kwenye kari, au utumie pamoja na wali kama biryani.Vionjo (Condiments): Tengeneza chutney, salsa, au raita ya mtindi.

Faida za Kiafya na Lishe (kutoka kwenye Apple Mangoes) Kinga ya Mwili: Yana vitamini C kwa wingi, inayosaidia uzalishaji wa seli nyeupe za damu.Mmeng’enyo wa Chakula: Chanzo kizuri cha nyuzinyuzi, husaidia kuzuia kufunga choo na kuboresha afya ya utumbo.Ngozi na Nywele: Vitamini A na C husaidia kutengeneza kolajeni na kulinda seli za mwili.Afya ya Moyo: Potasiamu husaidia kudhibiti shinikizo la damu, huku nyuzinyuzi na vioksidishaji vikisaidia kudhibiti kiwango cha kolesteroli.Yana polifenoli na karotenoidi zinazopambana na madhara ya viini huru mwilini.Yana vitamini A, C, E, folate, chuma, na potasiamu kwa wingi.Yana virutubisho maalum kama mangiferin, ambavyo vinaweza kusaidia kupunguza uvimbe mwilini.Hutoa sukari za asili zinazosaidia kuongeza nguvu na nishati.”

Kwa faida zote hizi na kwa heshima ya faida za embe ya MVIRINGE ,kiwanda cha Jambo kinapowakarishe nje wakulima wetu na embe zao za MVIRINGE hadi kuoza huku ni kuiviunjia heshima Embe ya MVIRINGE na kuwavunjia heshima wakulima wa embe Tanzania akiwamo Mwanakwetu mweneyewe, huku hoja ya bei ya shlingi 300 nayo kutowaheshimisha wakulima wa embe hii.

Makala haya yanatoa pole kwa wakulima wa embe MVIRINGE waliowasiliana na Mwanakwetu na ana hakika jambo hili litafanyiwa kazi kwa haraka na mamlaka husika.

Mwanakwetu upo ?Kumbuka:

“KAMPUNI YA JAMBO IACHE MARA MOJA KUIVUNJIA HESHIMA EMBE YA MVIRINGE.”

Nakutakia Siku Njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257

NB Makala haya yamewasilishwa moja kwa moja kwa Afisa Habari Mkoa wa Shinyanga , Afisa Habari Wizara ya Kilimo na kwa  mkurugenzi wa Jambo Food Production ili yafanyiwe kazi haraka.

 










 

 


 

0/Post a Comment/Comments