Adeladius Makwega-TARIME
Ni siku ya Ijumaa ya Januari 16, 2026, Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Evans Alfred Mtambi anafika Wilayani Tarime Tarime katika shughuli maalumu ya vijana kutoka viunga vyote ya mji huu wenye utajiri mkubwa wa madini nchini Tanzania ambapo kiongozi huyu anatumia muda wake kusikiliza kero za vijana wa mji huu.
Kipenga cha malalamiko kilipopigwa wakwanza walikuwa ni Vijana wa Bodaboda ambapo Bokeye Chacha Omahe alisema haya:
“Shida kubwa ni ubovu wa barabara hili linatupa tabu hata tunashindwa kufanya kazi zetu vizuri, tunaomba barabara zote zitengenezwe kwa wakati. Pia tunaomba utatuzi wa kuonewa na polisi kila mara wanatukamata tukiwa kazini.”
Akijibu hoja hii Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi alisema haya:
“Suala la ubovu wa bodaboda Wilayani Tarime anajua na yupo mkandarasi ambae ataikamilisha. “
Kanali Mtambi aliongeza kuwa haya masuala ya vijana tunapokea taarifa zao vizuri lakini kuna wakati kuna umuhimu wa kukaa nao a kuwasikiliza wenyewe wanasema nini na hili ndiyo maana amefika Wilayani Tarime.
“Suala la Polisi nimelipokea na linafanyiwa kazi nawaombeni mfahamu kuwa namba yangu ya simu ipo wazi, pale unapopata shida piga simu yangu. Bodaboda Mkoa wa Mara mmejengewa ofisi ngazi ya mkoa, viongozi wenu wa Wilaya na Mkoa wajulisheni hatua shida yoyote inapotokea, zitachukuliwa hatua na msiwe wanyonge katika hili.”
Kanali Mtambi alisisitiza kuwa malalamiko yote yanazungumzika vizuri na kila dereva wa gari au bodaboda lazima awe na leseni ili uendeshaji uwe salama na kwa hakika undeshaji vyombo vya moto mkoa wa Mara umebadilika na huko vizuri.
Kanali Mtambi aliwaomba vijana hawa kuwachagua viongozi wao ambao wanakuwa daraja baina yao na serikali.
Kwa upande wake Moses Chacha Kinoge alisema kuwa changamoto za vijana wengi Mkoa wa Mara ni kazi .
“Sisi mheshimiwa hatuna kazi na mimi kama nikiwezesha nipatiwe mtaji ili niweze kufanya biashara.”
Akijibu hoja hii Mkuu wa Mkoa wa Mara alisema hoja za ajira za vijana zinaweza kutatuliwa kwa kupatiwa mitaji na hili linafanyiwa kazi na kijana husika aliambiwa kuingia katika vikundi ili aweze kupatiwa mtaji huo.
Shughuli hii ilikusanya vijana kutoka shughuli mbalimbali wakiwamo wafugaji, wakulima , wavuvi, wachimbaji madini , bodaboda na madereva kila hoja zilitolewa na kujibiwa.
Wakati haya yakifanyika hapa Tarime Mjini, hali ya hewa ya Mji huu ni nyuzi joto 30 ambayo ni hali ya juu ya joto kunukuliwa na Mwanakwetu tangu afike mkoani Mara mwaka wa 2025 , huku unyevunyevu ni wa asilimia 10 , ujirani na mvua ni asilimia 22 na upepo ukivuma kwa KM 11 kwa saa. Kwa duniani nzima siku ya Januari 16, 2026 Mji mwingine wenye nyuzi Joto 30 ni Minn City Vietnam na baadhi ya Miji ya Austria na huku Nijeria.
Hali ya Mji wa Minn City huko Vietnam huwa ni nyuzi joto karibu 18 wakati wa katikati ya Januari ya kila mwaka lakini kupanda kwa joto hili hadi nyuzi 30 kunatokana na mabadiliko ya tabia nchi.
Mwanakwetu upo?Kumbuka:
“Changamoto za Vijana Zinatatuliwa.”
Nakutakia Siku Njema.
0717649257





Post a Comment