
Adeladius Makwega-MBAGALA
Siku ya Januari 21, 2026 ilianza murua kabisa kwa jua la kadili likiwaka vizuri hapa pahala, huku Mwanakwetu akipitia mitandao mbalimbali ya kijamii, kigulu na njia.
Hii ni safari mitandaoni, safari ya Mwanakwetu ilianza facebook, ikaenda whasaap na baadaye kizingiti ilikuwa hapo Instragram katika ukuta wa Balozi Hoyce Temu, Balozi Mdogo wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa.
Balozi Temu alikuwa kanyoa nywele zake vizuri hakuwa na mtindo wowote ule. Siku hii huyu Balozi wa Tanzania namna alivyopendeza alikuwa kama sumaku kwa Mwanakwetu hapa mtandaoni.
Hapa hapa Mwanakwetu alikutana na picha ya Balozi Temu kavalia vazi la kimasai akitembea katika makazi hayo ya Umasaini.
Mwanakwetu akauliza inakuaje Hoyce Temu na vazi la Kimasaini wakati yeye mchaga?Jamaa mmoja kando akasema unajua Wachaga na Wamasai ni wale wale. Mwanakwetu akaendelea kuzitazama picha za mheshimiwa huyu kwa muda kidogo, kumbe nyuma ya Mwanakwetu kulikuwa na mbeya mmoja akawa anafuatilia hekeheka za Mwanakwetu tangu awali akiwa ukurasa huu wa Balozi Dkt. Hoyce Temu.
“Nakuona Mwanakwetu ! Huyo ni Balozi Temu? Eee vipi Balozi wetu ni halali au haramu?”
Mwanakwetu akacheka kisha akajibu Balozi Hoyce Temu lazima awe halali labda wengine wanaweza kuwa haramu. Jamaa akacheka sana huku akisema sasa mbona mnabagua wengine halali na wengine haramu?
Hapa hapa kukaibuka hoja nzito juu ya haramu au halali.
“… isiyo halali hukosa ridhaa ya wananchi, inakiuka haki za msingi, inashindwa kutoa usalama au huduma muhimu, au ilichukua madaraka kinyume cha katiba, jambo linalofanya uhalali wa mamlaka yake kuwa wa kutiliwa shaka. Hata hivyo, utambuzi wa kimataifa unaweza kutofautiana, na hivyo kusababisha dhana kama … zilizo uhamishoni au mataifa yanayobishaniwa.
Uhalali wa …hutegemea imani ya wananchi kwamba … ina haki ya kutawala, mara nyingi kupitia taratibu za haki kama uchaguzi huru na wa haki na utawala bora kama utawala wa sheria na haki ya kijamii.
…isiyowakilisha kwa dhati matakwa ya wananchi, mara nyingi kutokana na uchaguzi uliodanganywa au upinzani kukandamizwa. Kutokuwa na uwezo wa kutoa usalama wa msingi, chakula, maji, au huduma nyingine muhimu za umma.
Kukiuka haki za binadamu, kukandamiza waandamanaji , au kutumia vurugu kubwa dhidi ya raia. Kupata madaraka kwa nguvu au kwa njia haramu, nje ya michakato ya kidemokrasia.”
Jamaa akauliza vipi kwa maelezo haya Balozi Hoyce Temu bado halali au haramu? Mwanakwetu akacheka sana kisha akasema Balozi Hoyce Temu bado halali. Jamaa akasema Mwanakwetu acha ubishi, acha mahaba, sema ukweli. Mwanakwetu akasema nasema kweli Balozi Temu ni HALALI.
Jamaa akasema Mwanakwetu toa sababu. Hapa hapa naye Mwanakwetu akajibu kwa maelezo haya:
“Unajua Balozi Hoyce Temu na wenzake 22 wao ni wa Mei 22, 2021 na wapo wengine wengi na ndiyo maana nasema Balozi Hoyce Temu ni Halali.”
Jamaa akacheka sana majibu ya Mwanakwetu juu ya Halali au Haramu kwa Balozi wetu kisha kila mmoja kuondoka zake.
Mwanakwetu upo?Kumbuka:
“Balozi Temu ni Halali.”
Nakutakia Siku Njema
0717649257






Post a Comment