“Furaha Furaha, Sasa Hivi Tutoke,Furaha Furaha , Sasa Hivi Tutokeeee, Furaha Furaha Sasa Hivi…Mwalimu Kwa heri,Kwaheri Tunakwenda Zetu Nyumbani Mungu Akipenda Tutaonana. Furaha Furaha, Sasa Hivi Furaha Furaha Sasa Hivi Tutoke…”
Msomaji wangu huo ni wimbo wa darasa la Kwanza Shule ya Msingi Kimanzichama Mkuranga Pwani ya Tanzania mwaka 1983 Mwanakwetu(Adeladius Makwega Kazimbaya), akiwa na wenzake kadhaa akiwamo Mohammed Kidundusi na Tatu Mohhamedi wakiimba kwa mwalimu wao sasa tano kasoro ili warudi nyumbani maana walikuwepo shuleni tangu asubuhi ya siku hiyo.
Huu wimbo unakumbukwa na Mwanakwetu Disemba 2025 huku mwaka huu ukipunga mkono wa kwa heri ya kuonana, hautarudi tena kama ilivyo vigumu kwa Mwanakwetu kurudi darasa la kwanza kukutana na wenzake.
Naweza kusema msomaji wangu kuwa hii kumbukumbu ya Mwanakwetu inayomjia akilini mwake wakati anaugubika mwaka wa 2025 huku akiugubua mwaka mpya 2026 kumbuka kinachogubikwa Vigumu kugubuliwa, haya mambo gubika gubua.
Wakati Mwanakwetu anatafakari hii gubika gubua, simu yake ikaiita, akaipokea na kuzungumza na vijana wake kadhaa ambao walikuwa wakifanya maandalizi ya kufungua shule. Vijana hawa wawili wapo sekondari mmoja yu shule ya msingi.
Kila mmoja akaongea lake katika simu hii kisha kijana mmoja akauliza swali hili:
“Baba tofauti kati ya Judge na Justice ni nini?”
Mwanakwetu akalipokea swali hili kwa mikono miwili kisha kutoa jibu hili:
“Jaji ni neno la jumla linalomrejelea afisa wa mahakama anayesimamia kesi katika mahakama za ngazi ya chini au ya juu na Justice ni cheo au heshima inayotolewa kwa majaji waandamizi/majaji wakuu wanaokaa katika mahakama za juu kabisa kutoa hukumu. Kwa kifupi, Justices wote ni majaji, lakini si majaji wote huitwa Justice; jina hilo linataja ngazi, heshima na mamlaka ya mahakama wanayohudumia.”
Mazungumzo ya simu yanaendelea hapa Albert Adeladius Makwega kijana anayeingia kidato cha tatu akasema hapa tulikuwa tunabishana je Justice siyo jaji?
Sasa tumepata majibu.
Maswali haya kumbe yalisababishwa na ugeni wa Justice Rehema Kerefu Jaji wa Mahakamaya Rufaa ya Tanzania aliyewatembelea vijana wa Mwanakwetu Disemba 27, 2025. Mwanakwetu akawauliza mbona hamkupiga picha ya Justice Rehema Kerefu?
“Mzee tulitaka tuombe tupige naye picha lakini, lakini lakini Justice Rehema Kerefu yule ni mheshimiwa sana.”
Mwanakwetu alipotambua hili alizungumza na mkubwa hapo nyumbani ambaye ndiye aliyeupokea ugeni na kuelezwa kweli Justice Rehema Kerefu alitembelea hapo.
Mwanakwetu kimoyo moyo akawaonea gere vijana wake kwa kuupokea ugeni huo mkubwa wakati wa sikukuu.
“Jamani kumbe nimeukosa ugeni huo!”
Kwa kuwa simu ilikuwa na sauti ya juu vijana hao walijibu kwa pamoja mzee Umeukosa Ugeni.
Aliyekuwa anaongea na Mwanakwetu katika simu akauliza je Mwanakwetu anamjua Justice Kerefu? Mwanakwetu akajibu
“Namjua kwa sura yake katika vyombo vya habari: mama mmoja mweupe hivi pia najua hata kesi zake kadhaa alizotoa hukumu mahakama ya rufaa miongoni mwayo ni ile ya kurejewa kesi ya Salumu Ndwete Skopioni alafu kuna kesi moja ilikuwa na kampuni inayouza nadhani matairi makubwa ya magari migodini ilikuwa inapinga kulipa kodi fulani nyingi, Justice Kerefu na wenzake waliamuri kampuni hii kulipa hiyo kodi mara moja.”
Mazungumzo haya yaliendelea kwa muda mara mvua kubwa ikaanza kunyesha pahala alipokuwapo Mwanakwetu hivyo basi wakawa hawasikilizani na huyu ndugu. Kuona hivyo Mwanakwetu akaamua kuikata simu hiyo kisha kuyaweka mazunngumo haya ya jioni hii katika makala haya unayoyasoma msomaji wangu.
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
Mwanakwetu kwa makala haya anawatakia makarani wa mahakama wote nchini Tanzania, mahakimu wote nchini Tanzania, Majaji wote nchini Tanzania na Majustice wote nchini Tanzania heri ya Krisimasi na mwaka mpya wa 2026 ambapo heri hii inatolewa na Mwanakwetu kutokana na ugeni wa Justice Rehema Karefu nyumbani kwa vijana wa Mwanakwetu Disemba 27, 2025 ugeni huu umefanya Mwanakwetu kuwakumbuka watumishi wote wa mahakama ya Tanzania na kuwapa heri hizo.
Mwanakwetu anatambua kwa mwaka 2025 ametayarisha makala 74 zenye maudhui juu ya Mahakama ya Tanzania na makala haya yanabadilisha takwimu na kuwa makala ya 75 juu ya Mahakama ya Tanzania huku hizo makala zidisha kwa tatu utapata Makala 225 yaani makala moja ya sauti, moja ya video na moja ya maandishi.
Makala zote hizo ni zawadi ya Mwanakwetu kwa mahakama ya Tanzania na hii ni maalumu ni kwa heshima ya Justice Rehema Kerefu aliyewatembelea vijana wa Mwanakwetu Disemba 27, 2025.
Mwanakwetu upo? Kumbuka:
“Yule Ni Mheshimiwa Sana.”
Nakutakia Siku Njema.
0717649257
%202022%20TZCA%20650%20(24%20October%202022).pdf.png)


%202022%20TZCA%20650%20(24%20October%202022).pdf.png)
%202022%20TZCA%20650%20(24%20October%202022).pdf.png)


%202022%20TZCA%20650%20(24%20October%202022).pdf.png)





Post a Comment