Adeladius Makwega-MBAGALA
“Palikuwa pametokea tukio la kupotea binti kigoli, jambo hili lilikuwa tete huku likifuatiliwa kwa kina, waliokuwa wanafuatilia walibaini kuwa muda mchache kabla ya kupotea binti na simu yake kuzimwa huyu binti simu yake ya mkononi ilikuwa jirani na simu kadhaa ambapo umbali wake ulikuwa wa kati ya mita sufuli na hadi 10. Jamaa hawa walipofuatilia kwa kurudi nyuma katika mawasiliano yao walibaini kuwa kundi la watu wanakaribia kumi na zaidi na jumla kuu ikiwa mara mbili ya ile ya awali.
Katika kundi hili kulikuwa na mwanamke mmoja tu, hawa jamaa waliwakamata wahusika 20 na hawakuhangaika sana na wanaume, wao walishughulika na huyu mwanamke pekee kwa asilimia 100 ambaye alikuwepo katika jirani na namba ya simu ya yule binti kigoli aliyepotea. Baada ya muda ilibainika kuwa kundi lote la jamaa 19 na binti huyu mmoja watu ishirini walikuwa na makosa waliyoyafanya kwa pamoja ikiwamo kula njama ya kuteka, kutesa, kulawiti, kubaka , kuuwa na kisha kuharibu ushahidi.”
Shauri kwa muamuzi lilikuwa la kushangaza mbele ya Mahakama Tukufu kuwa nusu ya kundi hili walifanya makosa yote ya kula njama ya kuteka, kutesa, kulawiti, kubaka, kuuwa na kuharibu ushahidi?
“Katika kundi lile na jamaa kumi na ushehe na yule mwanamke mmoja aliyekuwemo hoja ikawa inakuwaje huyu mama mmoja aweze kubaka na kulawiti? Hoja hii ilikuwa kwa mtuhumiwa aliyetambuliwa kwa namba mficho XXX-10 hoja ilikuwa mama huyu hakuwa na uume wa kubaka na kulawiti kwa kuwa yeye hakuwa na maumbile ya kiume. Maelezo yaliyotolewa na upande mashtaka kuwa mtuhumiwa XXX-10 hana uume lakini siku ya tukio mara alipotekwa binti kigoli, mama huyu mongoni mwa watekaji alichukua simu ya binti huyu na kuwa nayo na baada ya tukio aliizima smu haraka haraka baada ya kuichukua kutoka katika manyonyo ya binti kigoli.”
Mahakama Tukufu ilijulishwa kuwa mtuhumiwa namba XXX-9 ambaye yeye katika hati ya kiapo aliungama kuwa kuwa japokuwa alikuwepo eneo la tukio yeye alikuwa dereva tu, jukumu lake lilikuwa ni kuwasafirisha jamaa eneo moja hadi eneo lingine na kitendo anachokikumbuka yeye ndiye aliyeusindika (aliyefunga mlango) wa nyumba ambapo tukio hili lifanyika na mithili kwamba ndani hakukuwa na watu bali wenyewe wamesafiri.
Katika mahojiano ya watuhumiwa wengine mbele ya hati ya kiapo ilifahamika kuwa:
“Mtuhumiwa namba XXX-8 yeye alidai kuwa alikuwepo eneo la tukio na jukumu lake lilikuwa ni kumbeba huyu binti kutoka katika gari na kumfikisha katika makazi haya maana yeye alikuwa na mwili wenye nguvu lakini aliapa mbele ya ungamo la kiapo kuwa hakubaka, hakulawiti, wala hakuuwa na wala hakupoteza ushahidi.”
Mahakama Tukufu ilishuhudia hoja nyingine:
“Kwa mtuhumiwa namba XXX-7 yeye alikuwa eneo la tukio na alishuhudia kilichokuwa kinafanyika lakini yeye alipewa kazi ya kumfunga mdomo kwa solotape na kisha kuongeza sauti ya muziki katika makazi hayo, huku mwanzoni binti kigoli alipokuwa anapiga kelele yeye alianza kwa kumziba mdomo .”
Safari ya hoja mahakamani ilidokeza kuwa naye mhutuhumiwa XXX-6 yeye alikuwa mlinzi wa makazi ambayo tukio lililifanyika, wakati zoezi hili likifanyika.
Mjadala mahakamani kwa mabishano ya pande mbili yalikuwa mazuri sana.
Hasa kwa mtuhumiwa XXX-10 mtuhumiwa pekee mwanamke, ni kweli alikuwepo eneo la tukio na kitendo cha kuwepo eneo la tukio kilimuingiza katika makosa yote ya shauri hilo na kilimbadilisha ujanajike wake na kuwa janadume katili na isitoshe kitendo chake ya kuichukua simu na kukaa nayo kwa kuiondoa simu hiyo mkononi mwa mmiliki halali , hiki kitendo ilikuwa ni kufaniksiha makosa yote maana simu hii ilihifadhiwa katika maziwa(nyoyo la kuume la mwanamke mwenzake) kitendo hiki kilipaswa yeye kutambua kuwa huyu ni mwanamke mwezangu na huko ni kuzuia mtu aliyemtafuta binti kigoli kupatikana, kama kuna mtu angemtafuta au kama binti kigoli angekuwa na uwezo kupiga simu na hivyo hivyo ni kuzuia kupoka simu.
Jaji mahakamani alisema maneno haya:
“Mama haukujiuliza kuwa kama wanaume 19 waliweza kumuingilia mwanamke mmoja mbele ya mwanamke mwezake na wewe mwanamke mwenzake hakumsaidia hili lilimanisha kuwa kiakili, kifikra mtuhumiwa XXX-10 hakuwa mwanamke tena bali janadume katili. Kiakili mtuhumiwa XXX-10 maumbile yako yalibadilka na kuwa kiume kwa unyama huu uliyoufanya.”
Maelezo ya jaji yalikuwa makali mno huku akiongeza na hili:
“Maana unapozuia taarifa kwa jamii isijue ni kufanikisha makosa yote yaliyomo katika tukio hilo. Huko kukiwa sawa na kupoka mamlaka binafsi ya mawasiliano, huko ni sawa na kuweka mamlaka ya mawasiliano kwapani. Mama ulikuwa hodari wa kuweka Mpira kwapani.”
Kwake mtuhumiwa namba XXX-7 yeye alipewa kazi ya kumfunga mdomo kwa solotape na kisha kuongeza sauti ya muziki katika makazi hayo mwanzoni binti kigoli alipokuwa anapiga kelele. Mtuhumiwa XXX-7 nayeye aliingia katika makosa yote kwani alifanye hivyo, kikubwa alikuwa anayafanikisha makosa haya kwa uhodari mkubwa.
Hata kwa kwa mtuhumiwa XXX-6 na yeye aliingizwa katika makosa haya haya huku mahakama ikiambiwa haya:
“Mtuhumiwa XXX-6 wakati akiwa lindoni alisikia makelele ya binti wakati akifanyiwa vitendo vya kifedhuli, XXX-6 midadi ilimpanda nayeye kuomba apungeza midadi, hivyo basi lindo hili na silaha alikabidhiwa mtuhumiwa XXX-10 na yeye XXX6 kuingia mzigoni, hivyo basi nayeye XXX-6 aliingia katika kuyafanya makosa yote ya tukio hili.”
Msomaji wangu watuhumiwa wote 20 walitiwa hatiani kwa makosa yote ya tukio hilo na nawalitakiwa kuhukumwa kunyongwa hadi kufa kwa mujibu wa sheria lakini jaji aliyehukumu shauri hili alikuwa anapingana na Death Penaty kwa mujibu wa Imani yake ya dini hivyo basi badala yake Wote Walihukumiwa Kifungo Cha Milele Gerezani .
Jaji huyu ni jamii ya Jaji Raymond Mwaikasu ambaye aliwa kuwa jaji nchni Tanzania wakati anaisoma hukumu yake alisisitiza haya:
“Jukumu la kulinda usalama wa taifa ni la kila raia popote alipo katika taifa husika, huku vyombo vya ulinzi na usalama vimepewa majukumu machache kwa mujibu wa visheria vya vyombo vyao lakini sheria hizo za vyombo vyao haziwezi kumuondolea raia mmoja mmoja jukumu lake la msingi la kulinda usalama wa taifa lako popote alipo maana hili ni jukumu la KIKATIBA na jukumu la kila msingi la kila raia, watumishi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama watambue wao ni raia kama walivyo raia wengine.wenye majukumu ya kisheria kama yalivyo majukumu mengine ya kisheria ya raia wengine ikiwamo sharia ya ndoa.”
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
Bila ya shaka msomaji wangu umekielewa vizuri kisa hiki ambacho Mwanakwetu anajaribu kukimbuka baada ya kusimulia miaka karibu 13-14 nyuma. Hoja kubwa na shabaha ni matukio yaliyotokea siku ya Oktoba 29, 2025 na siku zilizofuatwa nchini Tanzania, Mwanakwetu anajaribu kulinganisha hasa akiyatazama majukumu vya vyombo vya umma vinatosimamia mawasiliano kama vile TBC, TSN na hata TCRA je vilitimiza vipi wajibu wake? Je vilifanya kazi hiyo vizuri au havikutimiza wajibu wake? Mwanakwetu siku ya leo anaamini kwa TBC, TSN na TCRA vinaweza kulinganishwa na watuhumiwa kadhaa katika shauri hili la mfano la XXX lililosimuliwa na Mwanakwetu
Swali ni je yupi mtuhumiwa XXX-10, XXX-7 au XXX-6?
Kwa hakika msomaji wangu wewe mwenyewe pima na kisha jaribu kuona kwa kutumia kipimo cha haki. Hapa kabla ya kuendelea kuyasoma makala haya, nakuomba urejee tena kisa hki tangu mwanzo.
…………………………………………………………………………………………………….
“Nina hakika umekisoma tena kisa hiki je TBC ni mtuhumiwa yupo? TSN ni nani naye TCRA ni yupi? ”
Mwanakwetu ninaamini kuwa majina ya viongozi wa taasisi hizo tatu walikuwa hodari wa kuuweka mpira kwapani sawa ya yule mtuhumiwa XXX-10, watendaji ngazi ya juu na wale waliyohusika moja kwa moja Mwanakwetu anashauri lazima wawajibishwe mara moja kama inavoshauriwa kuwajibishwa kwa wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama.
Mwanakwetu upo?
Je Makala haya yabatizwe jina gani? Wote Walihukumiwa Kifungo Cha Milele Gerezani auaHodari wa Kuuweka Mpira Kwapani?Mwanakwetu anachagua Wote Walifungwa Milele Gerezani.
Nakutakia Siku Njema.
0717649257










Post a Comment