NJIA YA MUNGU ITAWALE NJIA ZETU BINAFSI

 


 

Adeladius Makwega-RORYA MARA-TANZANIA. 

“Ndugu zangu , leo ni siku ya pekee kwa sababu tunaadhimisha sikukuu mbili muhimu ndani ya oktava ya Krismasi: sikukuu ya Familia Takatifu inayoadhimishwa Jumapili ya kwanza baada ya Siku ya Krismasi, na sikukuu ya Watoto Watakatifu Wasio na Hatia inayokumbukwa kila Disemba 28.

Injili ya Mtakatifu Mathayo inaonesha uhusiano kati ya matukio haya. Baada ya kuzaliwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo, Mamajusi kutoka mashariki walimtafuta. Walipitia katika jumba la Mfalme Herode kuuliza ni wapi angezaliwa mfalme mchanga wa Wayahudi. Hili lilimsumbua Herode na Yerusalemu yote. Aliwaambia Mamajusi wamtafute mtoto huko Bethlehemu na warudi na habari kamili.

Baada ya kumpata mtoto Yesu, Mamajusi walitoa zawadi zao na hawakurudi tena kwa Herode. Alipotambua kwamba alikuwa amedanganywa, akaamuru watoto wote wa kiume wenye umri wa hadi miaka miwili wauawe katika maeneo ya Bethlehemu.

Nako Katika ndoto, malaika alimwonya Yosefu akimbilie Misri, ambako walikaa hadi kifo cha Herode. Waliporudi, wakaishi Nazareti, wakitimiza yale manabii waliyokuwa wamesema kuhusu Mwana wa Mungu.|

Ndugu zangu, Familia Takatifu iliishi maisha ya kuzingatia wajumbe wa Mungu na kuwa tayari kutenda kulingana na neno lake. Kinyume chake, Herode alijikita katika mamlaka yake kiasi cha kuwaangamiza watoto wasio na hatia na familia zao. Tuombe neema ili njia za Mungu zitawale juu ya njia zetu za ubinafsi. Amina.”

Haya ni sehemu tu ya mahubiri ya Kadinali Luiz Antonie Tagle, Mkuu wa Propaganda Fide ya Kanisa Katoliki inayojihusisha na Uinjilishaji wa Watu Ulimwenguni akiwa pale Vatikani.

 

Mwanakwetu alitamani kujua Redio Vatikani walikuwa na nini katika dominika hii?

Ukurasa wa redio hii ulichapisha homilia ilyofanywa na Padri Richard Mjingwa huku Padri huyu alikipiga vizuri kinanda cha tafakari yake kwa kuzitaja changamoto za familia kwa sasa:

 “…Katika maisha ya ndoa na familia, kuna…, raha na karaha zake! Huko ni patashika nguo kuchanika, lakini yote haya ni mambo mpito, jambo la msingi ni kujenga na kudumisha umoja, upendo na mshikamano wa dhati, kwani Ndoa ni Sakramenti ya Kanisa kwa ajili pamoja na Kanisa na kwamba, upendo wa dhati …unawezekana hata katika ulimwengu mamboleo. Hii ni changamoto kwa wanandoa na familia kuhakikisha kwamba, wanadumu katika nia njema, upendo wa dhati na uaminifu endelevu katika raha na taabu; katika magonjwa na afya; wapendane na kuheshimiana siku zote za maisha yao!

Changamoto hizo ni kama vile: Talaka, Ndoa za utotoni, Uchumba sugu, Ndoa za mitaala, Kukosa uaminifu ndani ya ndoa, Ndoa za kurithi wajane, Mahusiano ya Jinsia moja, Ndoa baada ya ndoa ya kwanza halali, Ndoa zisizo na watoto,…. Matatizo mengine ni pamoja na: Familia za mzazi moja, Familia zenye mchanganyiko wa Imani, Familia zinayoishi katika mazingira magumu ya uchumi, Familia zenye watoto walemavu, Familia zisizo na mzazi hata mmoja, Familia zisizoishi imani, Familia zisizo na maadili, Familia zilizopoteza uwezo wa kulea, Familia zisizo na kipato. Asili ya matatizo katika ndoa na familia ni pamoja na: Utamaduni na Mazingira: Tunaishi katika historia yenye mazoea, mila, desturi na mapokeo ya wazee wetu. Iko sehemu ya utamaduni wetu isiyokubaliana na ukweli wa kimungu ambao ni wa lazima katika kuishi ndoa safi na familia bora. Mpaka sasa katika mazingira yetu zipo tamaduni zinazoruhusu talaka, ndoa za utotoni, uchumba sugu, ndoa za mitaala, ‘nyumba ndogo’, ndoa za kurithi wajane, …na ndoa baada ya ndoa ya kwanza halali. Ni jukumu la kila mkristo, ndani ya familia, kuchekecha utamaduni wake, kwani kumekuwa na chenga zisizopita katika chujio la Kristo aliye Mwanga wa maisha yetu.”

 

 

 

Katika Makala haya Mwanakwetu anakuomba msomaji akushirikishe mambo mawili:Mosi: Katika tafakari hii ya Redio Vatikania ilipambwa na picha moja nzuri, Baba Mtakatifu LEO IV akiwa altareni na kando yake walei wawili mke na mume na huyu baba akiwa amembeba mtoto kichanga.

 

 

Jambo la pili tunaelezwa kuwa Yosefu ,Maria na Mtoto Yesu walikimbilia Misri ambalo ni eneo nadhani mtawala alikuwa mwingine siyo Herode na walirudi baada ya ndugu huyu kufariki. Nilikuwanajiuliza katika ulimwengu wa leo hii hivi mtawala akakusaka, kisha suluhu ni kukimbilia mbali na utawala wake, hivi kama ingekuwa leo Yosefu, Maria na Mtoto wangeweza kupenya vizingiti vya UHAMIAJI? Kwa hakika kwa uwezo wa Mungu wangepenya vizuri tu, lakini sote tujifunze haya mambo ya mipaka, uhamiaji, uraia yasiwe chanzo cha kuumizana na kuuwana huku wakimbizi wapewe nafasi maana huku anakotoka ni hali ngumu kuliko hapo alipokimbilia.

 

Wakati haya ni Kanisani nayo hali ya hewa ya Rorya ambayo ni Wilaya katika Mkoa wa Mara ni nyuzi joto 20, ujirani nmvua ni wa asilimia 80, Unyevunyevu ni asilimia 90 huku upepo ukivuma kwa KM 6 kwa saa.

Mwanakwetu Upo? Kumbuka:

“Tuombe Mungu ili Njia ya Mungu Itawale Njia Zetu Binafsi.”

makwadeladius@gmail.com

0717649257 

 




 

0/Post a Comment/Comments