Timothy Lugembe,
Mwanakwetu Blog.
Hafla ya utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi vya wanawake , Vijana na watu wenye ulemavu imefanyika Disemba 11, 2025 ukumbi wa Siasa ni Kilimo ikiambatana na Elimu mbali mbali za ujasiliamali na Fedha kutoka kwa maafisa maendeleo, manunuzi , Biashara na Benki kutoka Iringa Dc mgeni rasmi akiwa mkuu wa Wilaya hiyo Benjamin Sitta.
Mikopo hiyo inatolewa kwa mujibu wa Sheria ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ambapo vikundi 73 kati ya 172 kutoka kata 28 vimepokea Jumla ya Shilingi Milion 407.9 kati ya Shilingi Bilioni 1.3 ikiwa ni awamu ya kwanza huku mpango ukiwa ni kutoa fedha hizo kwa awamu tatu na hii inategemea hali ya urejeshaji wa mikopo hiyo ili kutoa fursa kwa vikundi vingine.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Mhe. Benjamin Sitta amesema kuwa lengo la serikali ni kuona wananchi wanajikomboa kiuchumi ili kichangia mapato na kupunguza kaya maskini wilayani humo ikiwemo kuwa na nidhamu ya fedha hasa hasa kwa rika la vijana.
Ameongeza kuwa, wananchi wanatakiwa kujifunza mambo ya kimtandao ili kupata fursa mbali mbali ikiwemo tenda ya asilimia 30% ya kupeleka vifaa kwenye eneo husika ambapo maendeleo ya kijamii kama ujenzi wa shule yanafanyika kitu ambacho wananchi Wengi wamekuwa hawakitambui.
"Mkiona fursa mjue kuwa asilimia 30% ya kupeleka vifaa katika miradi ndani ya wilaya yetu ni yakwenu ninyi hivyo mnatakiwa kuingia kwenye mfumo kupitia mitandao ili mpate fursa hivyo msibaki nyuma" amesema Sitta.
Mwenyekiti wa Iringa DC, Mhe. Stephen Peter Mhapa amewataka wanavikundi kutambua mikopo hiyo ni Kodi za wananchi ikiwa haina riba hivyo wanatakiwa kufanya kazi kutokana na namna walivyo omba mkopo pia ameshauri kuwa makundi tajwa yachukuwe mkopo ikiwa wanashighuli za kufanya ili kuondoa usumbufu wakati wa urudishaji wa fedha hizo.
"Ni vizuri ninyi wakopaji mtambue kuwa hizi ni Kodi za wananchi wa Halmashauri ya Wilaya Ya Iringa fedha hizi tunazikusanya kwa shida ili mpate na ninyi mikopo hii sio zawadi hivyo mkaifanyie kazi", amesema Mhapa.
Pia maafisa maendeleo wameshauri wanavikundi kuwa vitambulisho vya Nida ,kitambulisho Cha mpiga kura , Namba ya utambulisho wa mlipa Kodi ( TIN namba) ili kupata wigo mpana wa fursa.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com





Post a Comment