MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI KATIKA ENZI YA MABADILIKO YA TABIA NCHI NA UWEKEZAJI WA KIMATAIFA AFRIKA

 

Rashid Msiri,

Mwanakwetu Blog.

Toka enzi za uumbaji wa dunia hadi hivi sasa ardhi imeendelea kutambulika kama nyenzo kuu ya maendeleo ya jamii kwa vizazi na vizazi lakini bado Kuna maswali mengi ya kujiuliza,

                “je, kwanini milio ya risasi na mapanga imekuwa ikisikika hadi sasa kwa jamii za wakulima na wafugaji Afrika?”

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kusema “ardhi ni mali ya umma.haitakiwi kuwa chanzo cha migogoro bali msingi wa mshikamano” lakini kauli hii bado imekuwa ni kizungumkuti katika nchi nyingi za Afrika.

Hadi hivi Sasa kila mwaka zimekuwa zikilipotiwa taarifa mbalimbali barani Afrika juu ya kuwepo kwa migogoro mikali kati ya wakulima na wafugaji kwa maeneo mengi bara hilo huku kukiwa na sababu mseto zinazoonekana kuwa ndio mizizi ya migogoro mingi ya ardhi.

Afrika Magharibi ndio eneo la moja kwa moja ambalo limeonesha athari kubwa ya migogoro mingi ya ardhi barani Afrika huku kukishudiwa mapigano kati ya wakulima na wafugaji ambayo yamepelekea vifo vya raia kwa baadhi ya maeneo.

Kwa mujibu wa taasisi science direct nchi ya Nigeria inaonekana kuwa ndio nchi ambayo imeshuhudiwa migogoro mikali dhaidi kati ya wakulima na wafugaji kwani tangu mwaka 1998 katika ukanda wa Middle Belt unajumuisha majimbo Benue, plateau, Nasawara kumeshuhudiwa vifo vya raia wengi wa eneo hilo kwani katika eneo la Benue State pekee kulishuhudiwa vifo vya watu 1683 katika migogoro ya wakulima na wafugaji Huku kesi 200 ziki rekodiwa katika eneo la Nasawara pekee.

Vile vile nchi ya Burkina Faso katika ukanda huo wa Afrika Magharibi nayo imekuwa ni moja ya kielelezo cha migogoro ya wakulima na wafugaji na hii ni kutokana na upinzani wa makabila ya Mossi na Fulani kutokana na eneo hilo kuwa na ukame na upungufu wa ardhi kutokana na kuzingilwa na vikundi vya kigaidi kama Islamists ambao wengi wao walipaswa kuwa wafugaji.

Hakuna lipoti za moja kwa moja zinazonyesha athari kubwa za moja kwa moja za migogoro hiyo kama vile vifo ila tafiti nyingi zimekuwa zikionyesha shinikizo kubwa la migogoro ndani ya taifa hilo.

Pia Nchi ya Mali ni moja ya eneo ambalo limekuwa likishihudia migogoro mikubwa ya ardhi hali iliyopelekea kutokuwa na usalama kwa baadhi ya maeneo ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti ya taasisi ya African Center imeonyesha migogoro mingi ya ardhi imeripotiwa katika ukanda wa Mopti na ukanda wa kati wa taifa hilo huku mamia ya vifo vikishuhudiwa kutokana na migogoro ya wakulima na wafugaji huku uwepo wa vikundi vya kigaidi vinavyolenga jamii za wafugaji hali ambayo imepelekea tangu mwaka 2015 kuwepo kwa ripoti za mamia ya vifo na kuhamishwa kwa wakazi kutokana na migogoro ya Ardhi.

Sababu au chanzo cha migogoro ya ardhi vimekuwa vikitofautiana kutoka eneo moja hadi jingine zipo sababu nyingi mseto zinazoonekana kuwa ndio vichocheo vya migogoro hiyo mfano taifa la Senegal kwa kipindi cha hivi karibuni limekuwa likipitia migogoro ya ardhi Kati ya wakulima na wafugaji ingawa nchi hiyo Hadi hivi sasa haijapitia athari kubwa kama vile vifo ukilinganisha na mataifa kama Nigeria na Mali ila kumenukuliwa kuwepo na migogoro hiyo inayosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi ambayo yamepelekea upungufu wa mvua, malisho hali iliyopelekea kuwepo kwa msigano wa kijamii kwa baadhi ya maeneo,

Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya mashirika ya vyombo vya habari kama vile AP News.

Je,Nini Sababu ya migogoro mingi ya ardhi Kati ya wakulima na wafugaji Afrika ?

Migogoro ya ardhi Kati ya wakulima na wafugaji kwa eneo kubwa la bara la Afrika imekuwa na sababu mseto kwani jamii imetofautiana kwa nyanja tofauti kama vile sayansi,siasa, uchumi na kijamii.

Kutofautiana huko kwa jamii pia hutokana na eneo husika kijografia na athari walizopitia kutoka kwenye tawala za mwanzo hapa ukilengwa utawala wa kikoloni barani Afrika.

Urithi wa mipaka ya kikoloni imeonekana ni moja ya sababu zilizopelekea kuwepo kwa migogoro ya ardhi Kwani mataifa mengi hayakubadilisha utaratibu wa mifumo ya usimamizi na matumizi ya ardhi uliowekwa na mkoloni hali iliyopelekea kuendelea kwa migogoro .

 Wakati wa kikoloni barani Afrika ardhi ilitambulika kama Mali ya serikali na sio jamii hivyo taratibu za ugawaji wa maeneo kwa ajili ya shughuli za uzalishaji mali hazikuzingatia matumizi ya jadi ya ardhi kwa jamii bali waliweka kwa manufaa yao.

Sababu nyingine ambayo imekuwa ikitajwa kwa karibu zaidii ni Mabadiliko ya tabia nchi ambayo yamekuwa ya kipelekea ukame hali inayosababisha malisho hafifu,kukauka kwa vyanzo vya maji.

Hali hii husababisha kuhama hama kwa wafugaji kusaka marisho kwa ajili ya mifugo yao ndio huchochea migogoro ya ardhi Kati ya wakulima na wafugaji pindi wafugaji wanapoingia kwenye maeneo ya wakulima.

Swali la kujiuliza ni kwamba “kama mazingira yangekuwa ni sababu pekee nchi zote zenye ukame zingekuwa kwenye vita na migogoro mikali ya wakulima na wafugaji,” Kwa Nini si hivyo?

Mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel, Amartya Sen amewahi kusema hakuna njaa kwenye nchi ya demokrasia inayofanya Kazi hii inakuonesha taasisi imara huzuia majanga yasiongezekeze hata kama ni ya kimazingira.

Afrika imendelea kushuhudia migogoro mingi ya ardhi Kati ya wakulima na wafugaji kutokana na udhaifu wa kisera wa usimamiaji na matumizi sahihi ya ardhi.


Wakati mwingine si matumizi sahihi ya sera iliyopo bali ni kutokana na kuwepo kwa utekelezaji hafifu wa sera hizo kutokana na siasa kutokuwepo kwa uongozi bora na siasa safi.

Nchi nyingi za kiafrika zimekuwa na sera zaifu na sheria zinazokinzana kwani hakuna mfumo unaoaminika wa usimamizi na umiliki wa ardhi Kwani serikali nyingi zinatambua ardhi ni ya taifa ila jamii inajua ardhi ni ya mababu na ni urithi wao.

Migogoro mingi huibuka baada ya mikinzano ya sheria za kisasa na Mila za jadi huku kuwepo na mfumo usiokuwa na usawa wa haki uliotawaliwa na rushwa.

Je, Afrika Mashariki tunaiweka upande upi kushindwa au kufanikiwa?

 Afrika Mashariki imekuwa na hisia mseto kwa maeneo mengi ya wachambuzi na wanaharakati wapo wanaoiona kuwa imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na kutokuwepo kwa athari kubwa za migogoro hiyo kiasi cha kuzua hali ya hatari ukilinganisha na maeneo mengi ya Afrika.

Lakini wapo ambao wamekuwa wakipingana na kauli hiyo kwa kuonyesha bado Kuna udhaifu mkubwa wa msimamiaji wa sera za usimamizi wa ardhi kulingana na sheria za nchi husika.

Hali hii imeleta ulinganifu kuwa wakati kwa kati kwani zipo nchi zilizo fanikiwa na zilizo shindwa kwa mfano,

Tanzania ni moja ya nchi ambayo imekuwa ikitajwa kuwa ina mafanikio makubwa kwenye muundo wa sera za usimamizi wa ardhi na ugawaji wa ardhi ngazi ya vijiji na usimamizi wa maeneo ya malisho kutokana na sera ya Village land Act ya 1999 lakini bado kumekuwa na changamoto kubwa ya utekelezaji wa sera hizo pia kuwepo kwa maamuzi ya juu bila kushirikisha jamii na migogoro ya mara kwa mara katika maeneo ya Morogoro,Manyara na Simanjiro.

Lakini katika baadhi ya nchi za umoja wa jumuiya ya Afrika Mashariki bado kumekuwa na changamoto kubwa kwa baadhi ya mataifa kwa kumekuwa na migogoro ya moja kwa moja licha ya kuwepo kwa sera nzuri mfano,

Nchi ya kenya inatambulika kwa kuwepo na mifumo mizuri ya kisheria lakini tafiti nyingi zinaonyesha kuwepo kwa uingiliaji mkubwa wa kisiasa kutokana na kuwepo kwa siasa kikabila na migogoro mingi mikubwa katika maeneo ya Baringo na laikipia hii inaonesha kuwepo kwa utekelezaji hafifu wa sera yao ya community land Act 2016.

Moja ya taifa la Afrika Mashariki ambalo linaonesha lipo kwenye dalili ya kushindwa kwenye migogoro hiyo ni taifa la Uganda kwani inaonesha kuwepo kwa mfumo wa Ardhi wenye mgongano (customary vs sharehold),s serikali kuchukua Ardhi kwa maendeleo pia kuwepo kwa migogoro kati eneo la karamoja hali inayopelekea matumizi ya silaha kwa nyakati tofauti.

Taifa la Sudan ya Kusini limekuwa ndio kielelezo cha kushindwa kwa jamii za Afrika Mashariki na hii ni kutokana na uwepo wa vita vya wenyewe kwa wenyewe chanzo kikiwa ni ardhi huku kukiwa hakuna taasisi thabiti inayofanya usimamizi wa ardhi.

Hali hiyo inaonesha ukanda wa Afrika Mashariki upo katika hatua Salama ya kuweza kukomesha migogoro hiyo ila kutokana na uwepo wa sera nzuri ila zinakosa ujasiri na utekelezaji mzuri wa kisiasa.

Yapo baadhi ya maeneo barani Afrika ambayo yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza migogoro mingi ya wafugaji na wakulima kutokana na maridhiano ya pande mbili juu ya matumizi jumuishi ya ardhi kwa kuzingatia mahitaji.

Mfano hai wa maeneo hayo ni ,

Eastern Burkina Faso – mradi wa RECOPA INITIATIVE

RECOPA (Pastoral communication network) ni mradi wa kimtandao unashirikisha wakulima, wafugaji na serikali katika baadhi ya maeneo ili kutatua migogoro ya ardhi kwa njia ya ramani za matumizi ya ardhi, alama za malisho na njia ya mijadala hii imepunguza migogoro mingi ya ardhi kwa eneo hilo hii ni kutokana na taarifa kutoka kwenye taasisi ya African Center.

Upi ni mtazamo wa taasisi na mashirika ya kidunia?

Mtazamo wa taasisi na mashirika ya kidunia umegawanyika katika maeneo mengi ila yote yamesaria kwenye nyanja za mabadiliko ya tabia nchi, Usalama wa chakula na Uongozi.

Kwa ripoti za mashirika kama UNFCCC na FAO (Food and Agriculture organization) zinaonyesha migogoro hii ni kama moja wapo ya athari zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi na mazingira yanayopelelea uwepo wa ukame, mvua zisizotarajiwa na upungufu wa malisho ni moja ya sababu mseto zinapelekea kuzuka kwa migogoro ya ardhi Kati ya wakulima na wafugaji.

Hii ni kutokana na ripoti za mikutano ya COP26 official reports; FAO 2022

Kwa mujibu wa ripoti ya benki kuu ya dunia na taasisi ya IFPRI (International food policy research institute) 2021 imeonyesha migogoro ya ardhi hupunguza usalama wa chakula kutokana na athari za udhalishaji wa chakula zinazotokea pindi migogoro inapotokea

Lakini kwa mujibu wa taarifa ya shirika la UNDP kupitia taarifa yake ya 2020 yenye kichwa “preventing violent conflict over lands in Africa” inasema ya kuwa kushindwa kwa uongozi ndio sababu kuu ya migogoro mingi ya ardhi barani Afrika hii kutokana na kuwepo kwa sera za ardhi zisizo tekelezeka, ukosefu wa ramani, kuwepo kwa rushwa na siasa zinazoingilia usimamizi wa ardhi kwa njia ya haki na usawa.


“Umasikini sio ajali.unatengenezwa na binadamu na unaweza kuondolewa na binadamu” nukuu hii aliwahi kuitoa baba wa taifa la Afrika Kusini Nelson Mandela inasadifu moja kwa moja yakuwa changamoto zote hizi zinaweza kutomezwa endapo kutakuwepo kwa usimamizi na utekelezaji mzuri wa sera na sheria, pia uwepo wa ushirikiano wa kijamii na makubaliano ya kijamii juu ya ugawaji wa maeneo mbalimbali ya kilimo na ufugaji kwa kuzingatia usawa wa teknolojia ya ramani na usimamizi wa rasilimali.

Kwa kuzingatia hayo Afrika na dunia inaweza kutatua migogoro ya ardhi kwa 80% kwani migogoro ya wakulima na wafugaji si hukumu ya mazingira ni hukumu ya uongozi.


rashidmsiri@gmail.com

0754645826




0/Post a Comment/Comments