Adeladius Makwega-MBAGALA.
Kwa muda wa juma nzima Mwanakwetu amekuwa akipokea ujumbe mfupi wa baadhi ya Watumishi wa Umma nchini Tanzania anaofahamiana nao wakimtania maneno kadhaa, maudhui makubwa ya ujumbe wao yalikuwa haya:
“Mwanakwetu Krisimasi imepita na mwaka mpya wa 2026 ndiyo huu, sasa kaka mkubwa mbona umekuwa kimya kutuandika makala juu ya kututakia heri ya sikukuu hizo watumishi wa umma wenzako?”
Mwanakwetu alipopokea ujumbe huu alicheka sana kisha akawaambia :
“Si mnaye waziri wenu wa utumishi wa umma na Katibu Mkuu Kiongozi waambieni watakie heri ya Krisimasi na Mwaka Mpya kisha Vitengo vyao vya Mawasiliano Serikalini vya taasisi hizo vifanye akala muone kama zitanoga? Kwanini mnataka Mwanakwetu afanye hivyo?”
Jamaa moja akajibu kuwa mbona Mahakama ya Tanzania umewatayarishia makala?Mwanakwetu akajibu :
“Sasa bahati ya mwenzio unailalalia mlango wazo?”
Mjadala huu ulikuwa mtamu sana na hili likimpa tafakari mno Mwanakwetu maana watumishi wa umma wengine aliajiliwa nao mwaka wa 2004 kama mwalimu , wengine kama watangazaji na wengine alikutana nao huku Halmashauri.
“Kaka Mkubwa kuwa acha Uchoyo wa makala zako tunahitaji ukarimu wako hasa sisi watumishi wenzako wa umma.”
Disemba 31, 2025 Mwanakwetu alilizitafakari jumbe zote, kisha kukata shauria na kuamua kuwaandika makala watumishi wenzake wa umma nchini Tanzania.
“Siku ilianza vizuri sana huku hali ya hewa ya mji wa Musoma ilionesha nyuzi joto 24, unyenyevu wa asilimia 10 ujirani na mvua wa asilimia 63 na upepo ukivuma kwa KM 3 Kwa Saa usiku wake baridi lilikuwa kali huku kitanda cha Mwanakwetu hakikuwa na blangeti. Mwanakwetu alivaa nguo kadhaa na kisha kujifunika shuka tatu.Majira ya saa 4 ya asabuhi jamaa watatu wakaamua kwenda kunywa chai mkahawani. Hapa mkahawani jamaa mmoja akanywa chai, supu na chapati mbili, mmoja akanywa chai muhogo kipande kimoja na supu na mwingine supu na chapati mbili.Wakiwa wanakunywa chai ukaibuka mjadala mmoja juu ya namna ya kuhama eneo moja kwenda lingine kwa mtumishi wa umma.
Hoja kadhaa zilitajwa kutumia cheti cha ugonjwa nahatari ya hali ya hewa kiafya kwa mtumishi, hoja ya kumfuta mwenza, hoja ya kuwahonga wanashgulikia uhamisho maana pesa uchawi wa kizungu. Mdau mmoja akasema mimi nipo katika utumishi wa umma kwa miaka mingi sana, mara nyingi mimi nikitaka kuhama eneo moja kwenda lingine huwa sifungi safari utumishi wala siandika barua kwa mtu yoyote, simuhongi afisa yoyote, sidanganyi kuwa mimi mngojwa, ninayo mbinu yangu ya gharama nafuu sana.
Jamaa mkahawani wakawa wakastaajabu vipi kama natumia mganga wa kienyeji ili na wenzake wapelekwe?Jamaa mmoja akapinga,jamaa mwingine akasema tuambie, Hili jambo linawezekanaje? Jamaa huyu akasema nchi hii Ofisi za Umma zimejaa watu masikini, watu wenye wivu, watu mahasidi na wanaofanyia kazi majungu. Jamaa kando wakasema hilo ni kweli.
Jamaa akasema,
‘Wewe si unataka kuhama hapa Musoma ili uhamie mkoa mwingine , wewe amka asubuhi zungukia vile vizimba vya samaki kama vitatu , piga picha zako vizuri za video na picha mnato huku umeshika samaki mara unawalisha samaki, mara unavua samaki huku ukisema maneno haya, jamani hivi vizimba vitatu vya samaki vina thamania ya shilingi milioni 240 ni mali ya MAKWEGA ENTERPRISES na kila baada ya miezi minane ninapata kiasi hicho. Nawaombeni Watanzania wezangu hasa watumishi wa umma tumie fursa ya pahala popote unapohamia kutumia fursa vizuri na siyo mnakaa mnalalamika. Fursa zipo kila kona ya hii nchi mimi nimetumia Zia Victoria. Hapo ulipo mfanyakzi wa umma zipo fursa za KILIMO, MIFUGO na kadhalika. Mimi nilipofika hapa Musoma nimetumia fursa hii na sasa nina vizimba vitatu karibu mjifunze.’
Jamaa huyu akaendelea kusema kuwa ukisharekodi tengeneza Makala maridakdi kama za Mwanakwetu , weka mapambo yote kisha video hizo zisambaze ukianzia kurasa zako za mitandao ya kijamii. Jamaa wenye wivu , fitina na majungu wamejaa maofisini watakesha kuitazama video hiyo mate na udenda ukiwatoka.Video hii ikishasambazwa katika mitandaa ya kijamiii wewe hesabu siku 60 tu utapata majibu ‘Jamaa kumbe tumehamishia kule mambo yake mazuri sasa tumuamisheni Lindi.’
Kweli utahamishiwa Lindi nia kukomoa miradi yako ife na wewe usiwe na furaha wala amani. Jamaa huyu akasema haya ndyo mambo ya Tanzania yetu yalivyo majungu ufanyiwa kazi haraka kuliko ukisema unamafuata mkeo au nini.”
Kumbuka jamaa hawa walikuwa wanakunywa chai, walipomaliza walilipa pesa zao na kisha kurudi walipotoka kuimaliza siku hii ya Disemba 31, 2025 siku ya mwisho kwa mwaka huo.
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
Msomaji wangu kwa heshima na taadhima makala haya ni maalumu kwa watumishi wa umma nchini Tanzania ambapo Mwanakwetu ameyatayarisha kwa heshima yao huku akiwapa mbinu hii ya kuweza kupata uhamisho mapema, maana mwezenu mjanja mmoja amekuwa akiutumia kila mara.
Mwanakwetu Upo?Kumbuka:
“Kwani Mie Waziri Wenu wa Utumishi.”
Nawatakia Heri ya Krisimasi na Mwaka Mpya Watumishi wote wa umma nchni Tanzania.
0717649257






Post a Comment