
Adeladius Makwega-MBAGALA.
Tangu majira ya mchana ya Disemba 8, 2025 na Majira ya Jioni ya Disemba 9, 2025 Mwanakwetu amefanya muhtasari wa saa hizo karibu 24 nchini Tanzania kwa yale aliyofanikiwa kuyakusanya:
“Kulikuwa na mkutano wa ZOOM MEETING unafanyika pahala fulani ajenda kuu nadhania ilikuwani Disemba 9, 2025. Mkutano huo uliandaliwa vizuri na ndugu mmoja tangu mwanzo hadi mwisho na hata chakula cha mchana hakuweza kula kutokana na umuhimu wa maandalizi na kikao hicho. Baadaye maandalizi ya mkutano yalikamilishwa na huo mkutano kuanza na hapa ndipo kijana muandaaji alipopata fursa ya kwenda kula.”
Msomaji wangu kama unavyofahamu vijana wa Kitanzania kwa hivi sasa wanafahamu sana Tekinolojia, hivyo aliyekuwa anaweka mambo sawa ya MKUTANO HUO NI GZEE.
“Nilikuwa nawaaunganishia wazee na waheshimwa katika mkutanoa huo. Mheshimiwa mmoja akasema wee GZEE unataka nikupe simu yangu iliweze kuchukua taarifa zangu? GZEEE akacheka akisema huu ndiyo utaratibu lazima unipe simu yako nikuunganishe na link ya ZOOM meeting.”
Wazee hao walibakia katika kikao nayeye GZEE kwenda zake kula. Mwanakwetu akacheka akisema wazee hawa wanawaogopa mno GZEE kwa sasa lazima wakae waoongee nao maana GZEE wanaifahamu tekinolojia , tekinolojia ni silaha kubwa katika ulimwengu wa sasa:
“Tekinolojia ina umuhimu mkubwa kuliko hata SUB MASHINE GUN yenye magazeni yake.”
Jambo ya kuumiza nafsi huyu GZEE aliyekuwa anaunganisha mitambo wakati wa matukio ya Oktoba 29, 2025 mdogo wake alidunguliwa Risasi na polisi na kufariki hapo hapo. Kwa sasa unaweza kuona unafanya jambo kuokoa jahazi kumbe ndiyo unavyozidi kulizamisha jahazi.Je utafanya kazi na nani?
Siku hii ilipita salama salimini na kulipokucha yaani Disemba 9, 2025 Mwanakwetu alizungumza na ndugu yake mmoja ambaye yupo Wilayani Mafia Mkoa wa Pwani Nchini Tanzania na yeye aliyasema maneno haya:
“Naona vijana wanaandamana, sasa hii Amani ya Tanzania ni ya kuishikilia kama fimbo ya nabii Seleiman! Hii hali itakuwa hivyo hadi lini? Maana Mwanakwetu vitabu vya dini ya Kiisilamu vinasema kuwa siku moja Nabii Seleiman alitoa kazi kwa majini huku yeye kasimama kando. Katika Uisilamu tunaambiwa kuwa Nabii Seleiman alikuwa na uwezo wa kuwafanyisha kazi majini pia Nabii Seleiman alikuwa Mfalme wa Majini, huku alikuwa na uwezo wa kuwaamrisha. Sasa Mfalme Seleiman aliwapa majini hayo majukumu yao, kila jini jukumu lake, sasa katika kuyasimamia majini hayo huku yakichapa kazi Mfalme alikuwa ameshika bakora yake huku kaigemia, majini yanachapa kazi usiku na mchana.
Kumbe Mfalme Kafa, huku fimbo imeendelea kuusaidia mwili wa Mfalme aonekane kama yu hai , kumbe kesha kufa siku nyingi. Hadithi inasema Mungu akawatuma mchawa wakawa wanaila ile fimbo ya Mfalme tangu ardhini kuelekea kilipo kiganja cha Mfalme, wakati mchawa wapo kazini wanaibungua fimbo ya Mfalme, ule uzito wa mwili wa Mfalme Seleiman ukashindwa kuhimili bakora iliyobunguliwa, kisha mwili wa mfalme ukaanguka chini. Hapo hapo ndipo majini yakabaini kumbe Mfalme Seleiman ameshakufa siku nyingi.”
Mwanakwetu anasimulia kisa hiki huku akicheka namna majini yalivyokuwa yakichezeshwa shere na Mfalme Seleiman kwa mujibu wa dini ya Kiisilamu.
Ndugu huyu wa Mwanakwetu akaongeza na hili:
“Sasa Mwanakwetu hii Amani ya Tanzania ya Kuishikilia kama fimbo ya Nabii Seleiman itadumu hadi lini? Sasa nyie wanahabari wa Tanzania mnafanya kazi gani? Mbona mnatuchea shere, kama hii TBC. Hivi hapa natazama TBC wanaonesha Upandaji wa Miti. Hapa naona Dkt .Ayub Ryoba TBC imeshinda kabisa, si aondoke zake? Kwa sasa mlitakiwa mzunguke mtuambie kitu gani kinaendelea vijijini na mitaani, Vyombo vya kimatiafa vikionesha mnaleta gubu, mkiambiwa mfanye mnaleta siasa! Tunataka mtimize wajibu ili sisi kesho tujue kama tunakwenda kazini na /biashara zetu au la na siyo kutuacha njia panda, hili halikubaliki, sasa hakuna live Dkt.Ryoba TBC imemshinda.”
Mwanakwetu aliendelea kucheka tu na hata alipozunguka katikati ya mji wa Musoma aliona Wanajeshi wa JWTZ wakiwa wametapakaa mitaani.
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
Kikubwa katika makala haya ni nafasi ya GZEE katika maisha ya sasa haikwepeki maana wana uwezo mkubwa na kutowasikiliza na kutowapa kipao mbele ni kujiangusha wenyewe matumizi ya nguvu yanazidi kuongeza chuki na mwisho wa siku anayetoa maamgizo ya kutumia nguvu hawezo kufanikiwa. Jambo la pili msomaji wangu tambua kuwa makala haya ni muhtasari wa matuko kadhaa ambayo yamekusanywa na Mwanakwetu Tangu Disemba 8- 9, 20
25 katika maeneo kadhaa ya Tanzania.
Mwanakwetu upo?
Kumbuka;
“Amani Tanzania Kuishikilia Mithili Bakora Seleiman Mfalme.”
Nakutakia Siku Njema.
0717649257
NB Shukrani za dhati kwa GZEE wote na Waisilamu wa Mafia Pwani Tanzania kwa visa hivi vilivyojenga makala haya.













Post a Comment