ACHENI KABISA KULIPENDA HILI JANI

 



Adeladius Makwega-TARIME.

“Kata ya Kitare ni Kata iliyopo katika Halmashauri ya Mji wa Tarime, Mkoani Mara nchini Tanzania yenye mitaa 13 miongoni mwao nin mtaaa wa Nkongore. Eneo hili lina Zahatani, Shule ya Msingi na Sekondari kubwa, ukiwa na madhari nzuri yenye chanikiwiti na ardhi yenye udongo mwekundu, migomba, kahawa na mazao mengine yakistawi vizuri.”

Penina Ryoba Kisiri maarufu kama Mama Ibra anafanya biashara yake na mkahawa mdogo wenye mabenchi mawili katika eneo hili ambapo ndiyo mkahawa pekee.

Mwanakwetu anaingia na kununua chapati tatu na kunywa soda majira ya alasiri. cha kustajabisha chapati hizo zikiwa za moto. Hili likiwa ni tukio geni maana ni mara chache kukuta chapati za moto majira ya saa tisa alasiri.

Mwanakwetu akiwa anakula chapati hizo akamuuliza mama muuza kwaninini waitwa Mama Ibra wakati wewe jina lako ni Penina Ryoba Kisiri?

Mama Ibra akajibu bila hiana:

“Jina hili nimepewa kwa sababu wanangu hapa kijijini wanateseka sana kwa kukosa eneo la kulima, hivyo Ibra Ibra, Ibra kutoka na mateso yao ya kuganga njaa. Zamani wanangu walikuwa wanalima mlimani lakini Serikali ilizuia kuutumia mlima huu. zamani tulikuwa tunalima Bangi na ilikuwa inatusaidia kulipia karo za watoto na gunia la Bangi lilikuwa linauzwa laki mbili, mimi nililima ndani ya miezi minane tu. Kwa sasa siwezi kulima tena Bangi maana wanangu wengi wamekosa masomo .

Kwa hapa kwetu gunia la mahindi ni 150,000. Bangi ilikuwa tunalima kwa miezi mitatu huku mahindi tunalima kwa miezi sita.

Huu mlima ulichukuliwa na Serikali , wazee wa kimila wakasema watavua nguo (watatupa radhi )kama tukilima Bangi tena kwa hakika Bangi hatulimi kamwe.”

Kumbuka msomaji wangu Mwanakwetu anakula chapati zake zilizopikwa na Mama Ibra ,kisha hapa hapa akamuuliza mbona Mama Ibra mapishi yako matamu sana? Maana nilikuwa sijui kama ndugu wa mheshimiwa Easter Matiko wanajua kupika namna hii?

 

Mama Ibra akajibu:

“Ehee akina mama wa Tarime tunajua kupika, siye hodari sana na tena hapa haukula samaki yaani ningekuungia na samaki vizuri baba ungekula wewe!”

Kumbuka msomaji wangu kuwa hii ni Disemba 28, 2025 Mkuu wa Mkoa wa Mara yupo Kata ya Kitare Wilaya ya Tarime.

Huu Mlima wa Mkongore ndiyo mlima unaodaiwa kuwa ulikuwa unalimwa sana Bangi na kusafirishwa kuuzwa nchini Kenya. Huku ikidaiwa kuwa tangu kale Mkongore walikuwa wanalima sana Bangi lakini hali ilikuwa tete mwaka 2017 baada ya kuwa na msako mkali na vijana wengi kukamatawa na wengine kukimbia na eneo hilo na baadaye serikali ililichukua na kuwakabidhi Jeshi la Magereza hadi mwaka wa 2025/ 2026 eneo hili lipo chini ya Uangalizi wa Jeshi hili.


 

Msomaji wangu kumbuka Mkuu wa Mkoa wa Mara Disemba 28, 2025 yupo katika Kata ya Kitare inayongozwa na Diwani aitwaye Philipo Marwa na yeye ali awali akisema kuwa mke huwa aachwi kwa kosa moja hapo akibainisha hawan umeme kwa mitaa yote 13 na ubovu wa barabara.

Katika ziara hii kulipambwa na uwepo wa vijana, akina mama, akina baba na wazee na miongoni mwa wazee ni Samweli Matutu Mwita ambaye anamiaka 70 akizaliwa katika Kijiji /Mtaa wa Mkongore, Ndugu Matutu yeye kwa sasa ni Mkulima huku awali alikuwa akifanya kazi na Kiwanda cha nguo cha Kilimanjaro Textile Jijini Dar es Salaam kama Mchanganyaji wa rangi, alisema Kijiji chao kilianza mwaka 1974 huku wakiomba Serikali kuwarejeshea mlima wao ili waweze kulima mazao na hawatolima tena Bangi huku akisema vijana wamekoma kulima Bangi.

Kanali Mtambi akizungumza na wananchi wa Kata ya Kitare aliwaelezwa wafuate sheria huku akiwahakikishia utatuzi wa suala la umeme na ujenzi wa barabara.


 

Kanali Mtambi aliwaambia wananchi wa Kata ya Kitare waache kulima Bangi ili wawe kurejeshewa Mlima wao akizungumzia kilimo cha Bangi aliwaambia kuwa hali anayoiona bado inampa mashaka kwani alimuona kijana mmoja aliyevaa kofia yenye picha ya jani la Bangi.

“Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa jani hili silifahamu na wala silitumii kabisa.”

Aliungama kijana huyu katika Mkutano huo wa hadhara.


 

Mkuu wa Mkoa wa Mara aliwaomba Watu wa Kata hii waache kulima na kuvuta Bangi maana haina maana na ndiyo maana Serikali inapiga marufuku jana hili lina madhara ya afya na akili ya binadamu. Kanali Mtambi pia aliwaambia wananchi hao utajiri upo kwa njia halali siyo mifumo mibovu ya kilimo cha Bangi.

Kweli mara baada ya mkutano huu Mkuu wa Mkoa na timu yake walianza safari ya kutoka Tarime kurejea Musoma Mjini.

Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?

Kwa hakika ziara hii ya Mkuu wa Mkoa wa Mara ilikuwa nzuri, huku maagizo kadha ya Serikali yakitolewa kwa viongozi wa Wilaya hii na yeye Mwanakwetu akivutiwa mno na watu wa Wilaya hii walivyokuwa Wakarimu na wacheshi japokuwa Mbunge wa Traime Mji hakuwepo pengine alikuwa Bungeni Dodoma vikaoni.

Mwanakwetu Upo?Kumbuka

“Acheni Kabisa Kulipenda Hili Jani.”

Nakutakia siku Njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257













 

 

0/Post a Comment/Comments