WANAJESHI WATATU MAISHANI MWANGU

 

Adeladius Makwega-MBAGALA

Siku ya leo Mwanakwetu anapenda akusimulie msomaji wake juu simulizi fupi ya kweli juu ya Brigedia Watatu Maishani Mwake; Brigedia Niliyempenda, Brigedia Mwanadiplomasia na Brigedia Aliyeniuzi.

Je Brigedia niliyempenda ni nani? Huyu ni yule ambaye baadaye alikuja kufahamika kama Luteni Jenerali Gideon Sayore (Brigedia Sayore) Brigedia Mwanadiplomasi ni Haruni Othuman ambaye baadaye alikuwa Mwambata wa Kijeshi wa Tanzania nchini Misri wakati ule wa Misri chini ya Hosni Mubraak na baadaye Misri chini ya chama cha Udugu wa Kiisilamu nayeye Brigedia Aliyeniuzi jina lake linabaki kibindoni. Hawa ni mabrigedia watatu maishani mwangu.

Kumbuka mabrigedia wote watatu wanatoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

 

 

Kwa kuwa msomaji wangu nakupenda sana nakuomba nikutoe hapo ulipo nikupeleke katika ulimwengu mwingine hasa wa Vyombo vya Ulinzi nchini Tanzania hasa JWTZ ambalo ni JESHI LA WANANCHI TANZANIA. Kwa wale tunaolifahamu vizuri Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) naomba niwakumbushe jambo hili;

“Kwa wanajeshi wetu, anaweza kupitia vyeo kadhaa tangu ngazi ya chini hadi ya juu lakini katika hatua hizo za vyeo vyake jeshini kipo cheo kimoja tu ambacho ataweza kufanya vizuri sana na pengine jamii ndani ya jeshi na hata nje ya jeshi ikamtambua , kumuheshimu na hata kumkumbuka mno.

Huku wapo baadhi ya wanajeshi wanapanda ngazi wanaweza kuonesha umahiri lakini umahiri wao ukabaki jeshini tu lakini nje ya jeshi hili likawa vigumu kutambua umahiri huo hadharani, umahiri wako kuvuka mipaka ya jeshi hii ni ngekewa.”

Hiki ni kitu ambacho Mwanakwetu amekibaini mno maishani mwake katika JWTZ. Kwa hiyo kama una cheo unaweza kujiuliza je cheo hiki kinavuka mipaka ya wapiganaji wezangu? Cheo husika kimeweza kunitambulisha vizuri nadani ya wapiganaji wezangu nje yao?

Pia kumbuka kuwa cheo hicho hicho kinaweza kukutambulisha vibaya na kisikupe heshima katika jamii zote mbili maana cheo siyo vile vyuma mabegani bali ni je jamii unayoitumikia inakutambuaje?

 

Msomaji wangu tambua hili kwa mzee wangu Luteni Jenerali Sayore cheo kilichompa umaarufu mno kwa Watanzania ni Brigedia japokuwa aliweza kushika nafasi kubwa hadi ya Mnadhimu Mkuu wa JWTZ yaani Chief of Operation and Training in (TDPF) lakini Watanzania kama akina Mwanakwetu wataendelea kumuheshimu mno Gideon Sayore hasa kwa ule UBRIGEDIA wake pale JWTZ maana wengi tulimtambua akiwa BRIGEDIA na heshima ya Brigedia SAYORE siyo tu kwa kutunukiwa Mnadhimu MKUU wa JWTZ hapa Watanzania rika za Mwanakwetu wanamkumbuka kwa kazi nzuri aliyoifanya Brigedia huyu ambayo hata hahitaji kutajwa katika makala haya.

 

Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?

Wakati Rais John Magufuli akiwa anamtumbua mtu IKULU ya Magogoni Mei 16, 2019 aliyasema maneno haya kwa Brigedia Aliyemuuzi Mwanakwetu;

“...wewe si ulikuwa Mkuu wa Usalama Jeshini? Kwa suala hili leo hii unaposema ni dogo na uliache utakwenda kulitatua huko mkoani hilo halinak maana kwani suala hili ulitakiwa uwe umelitatua mapema…suala hili si mlimuandikia barua Katibu Mkuu? Sasa mimi nalifanyia maamuzi leo…”

 

Kisa hiki cha maelezo ya marehemu John Pombe Magufuli Ikulu Dar es Salaam kinaanisha hivi suala lolote likiwa katika himaya yako jitahidi kulimaliza maana hicho ni kipimo chako maishani mwako iwe kwa askari au raia. Kisa hili pia kilimaanisha kuwa JWTZ inacho cheo cha MKUU WA USALAMA JESHINI … Kama JWTZ inayo MKUU WA USALAMA inakuwaje haya matukioya kifedhuli yanayoendelea kufanyika katika ardhi ya Tanzania kwa sasa? Je Mkuu wa Usalama Jeshini anafahamu nini katika haya yote? Je amechukua hatua gani kwa sasa? Labda tuseme hivi Mkuu wa Usalama jeshini yeye ni mdogo tuseme MKUU WA MAJESHI anafahamu nini katika haya na amechukua hatua gani yeye kama kiongozi wetu wa JWTZ mpaka sasa?

 

 

Mwanakwetu Upo?

Mwanakwetu anajiuliza siku ya leo juu ya Jacob Mkunda je atakuwa Mkuu wa Majeshi Aliyempenda, Mkuu wa Majeshi Mwanadiplomsia au Mkuu wa Majeshi Aliyemuuzi? Katika hali hii inayoendelea nchini Tanzania?

Nakuomba wewe msomaji wangu uchague kichwa kimoja kati ya hivyo vitatu lakini Mwanakwetu anachagua Wanajeshi Watatu Maishani Mwangu.

Nakutakia Siku njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257

 

 

 














 

 


0/Post a Comment/Comments