WALA NYAMA ZA WAFU?







 


Adeladius Makwega-MBAGALA

“Kuhani hawezi kutoa siri ya kitubio, hata kama mtu amekiri mauaji, lakini atamuhimiza kwa ushawishi wake mkiri huyo ajisalimishe kwa mamlaka husika. Kuhani amefungwa na muhuri usiovunjika wa kitubio na hawezi kuripoti kosa hilo kwa mamlaka husika. Hata hivyo, bado atajitahidi kuhakikisha haki inatendeka kwa kumuelekeza mtu huyo kuelekea kukiri kwa mamlaka kama sehemu ya toba yake na ili apate msamaha.

Muhuri wa kitubio hauwezi kuvunjwa. Kuhani anayevunja muhuri huu anaadhibiwa kwa kutengwa na Kanisa (excommunication). Ingawa kuhani hawezi kuripoti uhalifu, huenda akamuhimiza mkiri akiri kwa mamlaka husika ili kukabiliana na matokeo ya matendo yake.

Kuhani ataweka toba, ambayo inaweza kujumuisha kukiri kwa mamlaka na bado atatoa msamaha pindi mtu huyo atakapokuwa ametubu kwa dhati na kumaliza toba aliyopewa. Kuhani havunji muhuri wa kitubio kwa kumuhimiza mkiri akiri kwa mamlaka. Hii ni sehemu ya mwongozo wa kiroho na wajibu wake wa kumsaidia mkiri kurekebisha makosa yake.”

Haya ni maelezo ya swali lililoulizwa katika mtando mmoja wa Kanisa Katoliki Ulimwenguni kukiwa na maswali na majibu .

 

Kwa Mtakoliki aliyejihusisha na mauwaji na pale anapokwenda mbele ya kitubio wa Padri kipi kinafanyika?

Swali hili lilimjia Mwanakwetu na kuamua kuandika makala haya kutokana na sababu kubwa mbili kwanza ni tafakari iliyotolewa na Kanisa Katoliki la Tanzania kwa matukio ya wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 na kusomwa wa Baba Askofu na Rais wa Baraza na Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Wolfgang Pisa Novemba 15, 2025.

“…mamlaka zinazohusika ziendelee kulaani mauwaji yaliyofanyika na kukiri kuwa hawa waliuwawa ni ndugu zetu, jitihada za makusudi zifanyike ili haki na ukweli itawale katika taifa letu.

Mwenyeenzi Mungu anatoa onyo kali kwa watawala wasiotenda haki, wafalme wakitenda yasiyo haki ni chukizo maana kiti cha enzi huthibitika kwa haki (Methali 16,12)

…Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama waliohusika na mauwaji wote wawajibike au wawajibishwe na mamlaka zao za uteuzi. Hasira ya wananchi ipo kwa kuwa hakuna anayewajibika kwa matendo mabaya waliofanyiwa raia…”

Kwa hakika ukiyatazama majina ya wakuu wa Vyombo vya Ulinzi Usalama au wasaidizi wao kwa ngazi mbalimbali nchini Tanzania wapo Wakristo  kutoka madhehebu mbalimbali na wapo Waisilamu.

Kwa uhakika wapo ambao ni Wakatoliki ambapo ni vigumu kukwepa haya yaliyotokea na hawawezi kusimama mbele ya Watanzania na mbele ya altare wakasema kuwa wao hawajahusika, tena wao wanawajibika mara mbili .

 

Mwanakwetu katika hili anaomba Kanisa Katoliki lina wajibu mwingine wa sasa kwanza wa kuwatambua waamini wake walioshiriki katika matukio haya  katika vyombo vya ulinzi na usalama tangu wakubwa hadi wadogo, kishwa wafuate muongozo wote wa kitubio na vinginevyo watengwe.

Kanisa likifanya hivyo hili litakuwa mwongozo mzuri na siku nyingine wenye kushika silaha au wale waliyo katika mazingira hatarishi ya uhai wa binadamu wenzao wawe makini kwa kila linalofanywa katika maisha yao.

“Katika hili jina kubwa linalotajwa ni Afande IGP Camilius Wambura yeye kama Mkristo na kama ni kweli ni muumini ametimiza wajibu wake ipasavyo?”

Katika hili wapo wanaokwenda mbali kwa kuwa Afande IGP Omari Mahita ndilo lilikuwa jina ambalo lilitajawa kwa mabaya mengi tangu uhuru wa Tanganyika lakini kwa kilichotokea Wakati na baada ya Oktoba 29, 2025 Afande IGP Mahita Amekwenda likizo na Zigo ni la Afande IGP WAMBURA.

 

Jambo la pili ambalo lilisababisha Mwanakweu kuandika makala haya lilikuwa ni kifo cha kijana mmoja wa Mkatoliki ambaye alikuwa akifanya shughuli zake za Bajaji jijini Dar es Salaam. Akiwa kando ya barabara akingoja abiria huku amejilaza katika Bajaji yake risasi ilimpiga na kuingili mwilini mwake. Vijana bajaji na bodabada walikasirika wakisema mbona hatupo kwenye maandamano walimbeba harakaharaka na kumkimbiza Hospitali na walipofika hapo walipokelewa na daktari ambaye alikuwa akipanda bajaji ya huku kijana …

“Jana alinibeba kunipeleka benki na kunilrudisha hapa hospitali… mwenzenu ameshafariki.”

Baadaye mwili huku ulikuwa unahamishiwa kutoka mochwari moja hadi nyingine, huku vijana hawa walikuwa wakifutatilia muda mwingine waliwahi kufika mochawari husika na mwili kuingia hapo baada ya dakika tano na wakati mwingine mwili kufika hapo kabla ya wao.Kwanini miiili hii ilikuwa inahamishwa hamishwa?Baadaye mwili huo ulipatikana kwa neema ya Mungu.

 

Msomaji wangu ebu fikiria ndugu yako amefariki kwa kupigwa risasi kisha kuupata mwli inakuwa tabu, tatizo ni nini?

“Watanzania Siku Hizi Wanakula Nyama za Wafu?”

Familia inaingia gharama kusafirisha mwili kutoka Dar es Salaam hadi kijijini , familia inaingia gharama ya kuzika kwa kununua jeneza na vyakula vya msibani, marehemu alikuwa dereva wa  bajaji anaganga njaa ili maisha yake yasonge tu.

Ndugu yangu ebu jiulize;

“Huyu aliyetoa agizo ya kuwapiga Watanzania risasi ni nani? Huyu aliyetoa silaha hizo ni nani na yupo wapi ? Huyu aliyebeba bunduki hii ni nani ?

Kwa sasa yupo wapi na sasa hivi anafanya nini? Huyu aliyetoa agizo na kuwa na ugumu wa kupata miili ya Watanzania waliuwawa katika kadhia hii ni nani ?

Huyu aliyekuwa anaficha na kuihamisha miili ni wafu nani? Tumjue, Tumuulize ati Mwenzetu Siku Hizi Unakula Nyama za Watu?”

Haya ni machache kati ya mengi ya Mwanakwetu siku ya leo.

 

Mwanakwetu upo? Je Makala hayayaitwaje?

Afande IGP WAMBURA AMPOKEA ZIGO LA AFANDE IGP MAHITA? Siku Hizi Wala Nyama Za Wafu. Mwanakwetu anachagua Wala Nyama Za Wafu.

Nakutakia Siku Njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257

 

 

 

 































 

 


0/Post a Comment/Comments