Adeladius Makwega-Musoma MARA
Kikao Cha Baraza la Wafanyakazi, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara kilichofanyika Novemba 26, 2025 kimeambiwa kuwa Shilingi milioni 284.8 zimepelekwa GPSA kwa manunuzi ya basi jipya la kubeba watu 40 ambalo litasaidia katika shunguli mbalimbali za ofisi hii ya umma.
Akizungumzaa katika Kikao hii Katibu Tawala Mkoa wa Mara Mwalimu Gerald Musabila Kusaya alisisitiza kuwa basi hili linanunuliwa, kikubwa na kulitunza vizuri, siyo lije hapa likae kipindi kifupi linaharibika, hilo sintolikubali, pia naagiza watumishi wote wapewe nafasi za mafunzo huku wanaokwenda katika mafunzo haya wakirudi wakumbuke kutoa taarifa ya kile walichojifunza na manufaa aliyoyapata katika mafunzo hayo
“Mafunzo ni muhimu na siyo kila mara anakwenda mtu mmoja, mtoe nafasi kwa wote mathalani kwangu pale yupo karani wangu na yeye awe anashiriki mafunzo haya.”
Kikao hiki kilikuwa na ajenda 11 huku awali kabla ya kuanza uliimbwa wimbo wa MSHIKAMO DAIMA.
Wakati haya yakifanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, hali ya hewa ya Mji wa Musoma ni nyuzi joto 28, upepo ukivuma kwa KM 16 kwa saa, ujiani na mvua ni wa asilimia 44 na unyevenyenvu ni asilimia 0.
makwadeladius @gmail.com
0717649257


Post a Comment