
Adeladius Makwega
Wakristo wameambiwa kuwa mwezi wa kumi umemalizika ambao ni Mwezi wa Mama Bikira Maria na sasa mwezi wa 11 ukiwa mwezi maalumu wa kuwaombea marehemu wetu waliopo toharani.
Haya yamesemwa na Padri Julius Ogola katika Kanisa la Mtakatifu Agustino Parokia ya Mwisenge Jimbo Katoliki la Musoma Jumapili ya 31 ya Mwaka C wa Kanisa.
“Hakuna gharama yoyote kuwaombea marehemu wetu, ombeeni marehemu wetu mkiwa msali wenyewe nyumbani na hata hapa kanisani, ombeni misa.”
Kwa hakika misa hii ilikuwa na waamini waliosali kanisa lenye mapengo mapengo katika mabenchi yao ambapo kwa desturi kanisa hili hujaa sana waamini na hadi kuketi nje.
Katika jumapili hii ni walinzi wawili wa Parokia hii ndiyo walikuwa katika viti vya nje na mtu mmoja mwanamke ambaye alikuwa anasimamia misa hii.
Hakukuwa na muuzaji wa visakramenti vyovyote nje ya kanisa hili na hata duka la parokia halikuwa wazi ambapo kwa kawaida visakrament huuzwa na watu nje ya kanisa na duka la Parokia huwa wazi kila misa na kila dominika.
Hata wakati wa kutoka nje ya ukuta wa Kanisa hili la Mtakatifu Agustino watu walikuwa wakikatazwa kufika Barabara ya Majita Maarufu kama Majita Road ambapo huku kuna maduka ya kununua vyakula na njia kuu ya kwensa Musoma Mjini na Musoma Vijijini, vituo vyote vya mafuta vimefungwa na bodaboda chache ndiyo zinazozunguka.
0717649257











Post a Comment