Adeladius Makwega-MBAGALA.
Usiku wa kuamkia Novemba 18, 2025 Mwanakwetu awali aliongea na familia yake kwa muda mrefu sana juu ya masuala la taaluma ya vijana wake wawili wakiume kisha muungwana huyu kuuchapa usingizi.
Majira ya usiku akiwa usingizini aliota ndoto moja ya mandhari yake akiwa kijana mdogo sana Mtaa wa Mangaya jirani na Masjidi Sinina na pia Mtaa wa Mbagala Sabasaba ndoto yenyewe ili hii;
“Kwanza alitoka nyumba kwa Babu yake Mzee Fidelis Kazimbaya Makwega, huku akimuaga Bibi yake Mzaa Baba Edwiki Omari Binti Mkomangi, wakati anaagana na bibi yake huyu alimwambia maneno haya;
‘Bibi mimi kesho nasafiri, naomba nikaangie karanga kilo mbili ili zinisaidie huko niendapo safarini.’
Mwanakwetu ndotoni akatoka nyumba kwa Binti Omari Mkomangi ambaye alikuwa maarufu kama Bibi Mkomangi, Wengine wakimuita Bibi Tulauke, Nyamakwega au Bibi Makwega. huku Mkomangi na Tulauke yakiwa majina ya wajukuu wa huyu bibi.
Kumbuka hapa ni nyumbani kwa Nyamakwega Mbagala Sabasaba, hapa hapa Mwanakwetu akavuka Bonde na kufika Mbagala Mangaya hapa akaingia nyumbani wa Binti Masikini huyu alikuwa mama wa Kipogolo aliyeolewa na Profesa Robert Mfugale, wengine wakimuita Mama Mfugale, wakati huo mama hyu alikuwa mwalimu wa Shule ya Msingi Gerezani Katikati ya Jiji la Dar es Salaam.
Mwanakwetu ndotoni akamsalimia Mama Mfugale na kutoka nje akiwa hapo nje, akiwa mwenyewe akakutana na akina mama wanatoka Msikitini Kusali Salaat Ijumaa akiwamo Bi Mbwembwe. Bibi Mbwembwe akamsalimia Mwanakwetu na huku akisema maneno haya ‘Wewe mkina Makwega hujambo?Njoo jirani yangu mbona unatembea tumbo wazi na kikaptura ? Vaa shati lako bwana utakosa wachumba. Si unajua kwangu kuna mabinti wengi wazuri? Yupo Pili, yupo Amina, Mie Bibi waPwani Nikukupenda Nakutunuku Binti yangu, wewe unamtaka nani?’ Bibi Mbwembwe kamuuliza swali Mwanakwetu, nayeye Mwanakwetu akajibu,
‘Mimi nampenda Pili kwa kuwa Pili ni Mweupe.’
Bbi Mbwembwe akamvisha shati vizuri Mwanakwetu huku akimfungwa vifungo vya chawa vya shati, naye Bibi Mbwembwe na akina mama wale waliokuwa wanatoka kusalia Salaat Ijumaa Masijidi Sinina wakaeenda zao majumbani kwao.”
Majira ya saa tisa usiku (0318)ya Novemba 18, 2025 Mwanakwetu akashituka usingizini akijiuliza inakuwaje Mwanakwetu siku ya leo anamuota Bibi Mbwembwe;
‘Wewe mkina Makwega mbona unatembea tumbo wazi na kikaptura chako cha dengrizi? Vaa shati lako bwana utakosa wachumba. Si unajua kwangu kuna mabinti wengi wazuri ? Yupo Pili yupo Amina, Mimi Bibi Pwani Nikukupenda Nakutunuku Binti yangu wewe unamtaka nani?’ Bibi Mbwembe akamuuliza swali Mwanakwetu, nayeye Mwanakwetu akajibu,
‘Mimi nampenda Pili kwa kuwa Pili ni Mweupe’….”
Kumbuka msomaji wangu Mwanakwetu yupo macho, huku sasa akimkumbuka Bibi Mbwembwe ambaye alikuwa Mwanamke wa Kiisilamu anayesali sala tano za dini hii na tukio hili ni kama la mwaka 1988/1989 miaka 36 nyuma kwa mwaka wa 2025.
Kwa hakika msomaji wangu nadhani itakuwa vizuri kama nitaeleza kwa kina juu ya Bi Mbwembwe alikuwaje katika maisha yake kipindi hicho;
“Bibi Mbembwe alikuwa anamiliki nyumba yake moja ya kawaida Mbagala kwa Mangaya ambayo ilikuwa na wapangaji kadhaa, huku vyumba vya mbele akiishi na watoto wa kaka zake wa kike na wakiume. Watoto wa kaka zake wa Kike alikuwepo Pili na Amina, Amina alikuwa mkubwa rika moja na Mwanakwetu huku Pili alikuwa mdogo nadhani darasa la Pili wakati huo.
Kwa bahati mbaya Bi Mbwembwe hakujaliwa watoto hata mmoja na ndiyo maana alikuwa anaishi na watoto wa kaka zake na hata baadaye Bibi Mbwembwe alipofariki wale watoto wa kaka zake ndiyo walibaki na nyuma hii huku Pili na Amina walishaolewa.
Taarifa za watu wa Mbagala Kwa Mbagaya zinadai kuwa mwaka 2025 wameiuza nyumba hii kwa Mwarabu na niliambiwa kuwa nyumba hii sasa kuna Bonge la Kituo cha Mafuta kinajengwa.”
Mwanakwetu anasema nini Siku ya leo?
Kwa hakika hii ni ndoto lakini pia ni sehemu ya maisha ya kweli ya Bi Mbwembwe ambaye akiwa hai Mwanakwetu alimfahamu.
Kwa hakika Mwanakwetu ndotoni alitunukiwa Binti wa Bi Mbwembwe anayeitwa Pili, Mwanakwetu ndotoni alimchagua Pili kwa kuwa alikuwa binti mweupe.
Msomaji wangu kumbuka mtu kabla ya kukutunukia kitu unapewa sharti na sharti hili kwa Mwanakwetu kutoka kwa Bibi Mbwembwe;
“…mkina Makwega mbona unatembea tumbo wazi na kikaptura chako cha dengrizi? Vaa shati lako bwana utakosa wachumba. Si unajua kwangu kuna mabinti wengi wazuri ? Yupo Pili yupo Amina…”
Mwanakwetu ndotoni aliona Bibi Mbwembwe akimvisha shati na kumfunga vifungo chawa…
Haya ni ndotoni tu, je kwa uhalisia Mwanakwetu namna alivyo angeweza kukubaliana na Bibi Mbwembwe kisa atunukiwe Binti Mweupe Pili?
Haya ni ndotoni tu siku ya leo.
Mwanakwetu upo? Kumbuka
“NIMETUNUKIWA BINTI MWEUPE.”
Nakutakia Siku Njema.
0717649257









Post a Comment