
Adeladius Makwega MBAGALA&
Debora Kitundu- Univesity of Iringa (UoI).
Unapofika Mbagala iwe Mangaya, Kizuiani na hata Sabasaba zipo koo nyingi za zamani ambazo uzao wao upo hadi leo, mojawapo wa koo hizo za zamani ni ukoo LILINGANI.
Kwa waliosoma Shule ya Msingi MBAGALA zamani watakumbuka hili;
“Tangu darasa la Kwanza hadi la Saba na hata kama mikondo A, B, C au D katika kila darasa na Kila mkondo wakati huo alikuwepo MKINA LILINGANI. Hawa MKINA LILINGANI wana asili ya Mikoa ya Kusini na Mwa Tanzania na pia huko Mkoani TABORA.
Huko Tabora ni kwa bibi aliyewazaa akina Lilingani wa miaka 1945 hadi 1970.”
Kwenda mbali zaidi nakuomba msomaji wangu utambue hili, katika haya madarasa yalikuwa na mikondo minne pia ndani yake kulikuwa na kitu kingine cha ziada kutoka kwa akina Lilingani; Hawa mabinti Lilingani wa wakati huo walikuwa hodari mno wa kuzaa watoto wengi ambao walikuwepo pia katika madarasa haya lakini majina yao yalikuwa na ubini wa baba za maana akina Lilingani ni ujombani tu, msomaji wangu tambue kuwa UKOO HUU ULIKUWA NI JESHI KUBWA.
Pale shule ya MSINGI MBAGALA zilikuwepo koo zingine zenye sifa kama hii mathalani UNGAUNGA nayenyewe ilikuwa hodari sana, huku akina MAKWEGA na wao walikuwa hodari pia wa kuzaa.Katika hili bila kuzisahahu koo zingine ambazo zilikuwa na uzao mchache ambao wengi wao walikuwa wahamiaji kutoka KURASINI, TANDIKA, TEMEKE KARIAKOO baada ya kuuza majumba yao.
Ukoo mmojawapo ambao ulikuwa na uzao mchache ulikuwa wa akina SAMATTA huu huu anapozaliwa MBWANA SAMATTA mchezaji wa soka la KIMATAIFA ambao walikuwa na nyumba zao kama mbili MBAGALA MAKUKA sasa Maarufu kama MBAGALA KWA KIPATI ambapo ilikuwepo mashine kubwa sana ya KUSAGA NA KUKOBOA YA MTU ANAYEITWA KIPATI KWA KIPATI (MBAGALA KIPATI).Nadhani akina SAMATTA nyumba hizo wamezipeleka sokoni na sasa kuna BONGE la sheli.
Haya msomaji wangu nakupa kama zawadi kutoka kwentu sisi wenye Darisalaama yetu.
Hii msomaji wangu ni MBAGALA ya miaka ya 1970-1995.
Mwanakwetu ni mwingi wa simulizi sasa siku ya leo msomaji wangu nataka nikupe kisa kimoja cha kweli kabisa kilichohusisha koo tatu SAMMATTA, MAKWEGA na LILINGANI.
“Ukoo wa LILINGANI ulikuwa na vijana watanashati na mabinti Warembo sana , huku walikuwa hodari wa kuzaa mapacha. Vijana wa Mbagala walikuwa na msemo kuwa ukitaka kupata mapacha kaoe kwa akina LILINGANI .
Nako kwa akina MAKWEGA na akina SAMATTA kulikuwa na vijana wapole sana.
Vijana wa kina LILINGANI walikuwa na kaka yao mmoja alikuwa mwalimu Kareti KUNG FUU. Katika pitapita ikabainika kuwa Kijana mmoja kutoka kwa akina SAMATTA yu jirani na binti wa LILINGANI huku Kijana mmoja kutoka kwa akina MAKWEGA na yeye yu jirani na binti wa LILINGANI. Vijana wababe wa akina LILINGANI wakaamua sasa hawa jamaa wanaofanya uharibifu kwa dada zetu lazima tuwaozeshe NDOA ya MKEKA, vijana wa akina LILINGANI ambao ukoo mkubwa wameamua kukata shauri kulikamilisha hili.”
Kwa wasomaji ambao hawafahamu NDOA YA MKEKA ni nini naomba nieleze kidogo maana ya ndoa hii.
“Hii ni ndoa ambayo ilikuwa inafanyika hasa maeneo ya PWANI YA TANZANIA mara baada ya ndugu kubaini kuwa dada yao, mtoto wao anaishi kinyumba na mtu ambaye si mumewe bila uhalali wa wazazi, ndugu wa binti husika wanajipanga kisha kumuandaa SHEKHE ambaye ni kijana wanavamia katika makazi husika walipo siku hiyo wapendanao hao, wanabeba ubani, wakishavamia makazi wanatoa ilani kwamba wewe fulani bini fulani unaishi kinyumba na dada yetu sasa leo tunakufungisha ndoa.
Shehe wa dini ya KIISILAMU anapiga dua choma ubani mambo yanakwisha, anafungisha ndoa KIBABE baadaye anarudi na kundi lake na ndoa huwa imekamilika, jamii iliyshuhudia huwa inashangilia. Kesho asubuhi unasikia kuwa fulani kafungisha NDOA ya MKEKA. Baada ya hapo maisha ya pika pakua yanaendelea.”
Kumbuka Koo tatu zinahusisha na kisa hiki SAMATTA, MAKWEGA na LILINGANI, huku akina MAKWEGA na akina SAMATTA wanao pia wana dada zao warembo na vijana tanashati ,jamaa wanajipanga kuwafungisha ndoa za MKEKA vijana wa akina MAKWEGA na SAMATTA.
Wakati mpango unasukwa Mwanakwetu akakutana na hii habari... Makwega ndugu yako tunajipanga kumuozesha ndoa ya MKEKA kisa anaishi kinyumba na dada yetu, si unajua tunacheza Kareti sasa, mwambie ndugu yako aachane na huyu dada mara moja.
Mwanakwetu ngumu anazijua , karate ni hodari. siyo mtu wa mcheomchezo akawa njia panda anamwambiaje ndugu yake juu ya kumuacha huyu binti ili awe salama? Mwanakwetu akawa anaogopa maana ni mtu anayemuheshimu sana, kusema anataka lakini hawezi akilini mwake akawa anajiuliza;
“NDOA YA MKEKA inahusishwa ubani na shekhe, hii ni kama ndoa ya KIISILAMU hawa jamaa na ndoa yao ya MKEKA watawezaje kumuingiza huko NDOANI, HUYU NDUGU YANGU MKATOLIKI? Lakini hawa jamaa wakishasema wamemfungisha ndugu yangu NDOA YA MKEKA HILO TU LINAKUWA FEDHEA maana waningia ndani ya nyumba ka fujo wakikukuta na VIP na Khanga wao twende kazini, sasa nafanyaje?”
Mwanakwetu kijana akawa anajiuliuza maswali mengi.
Kwa hakika kwa utaratibu wa NDOA YA MKEKA wapo baadhi ya watu waliozihusudu ndoa hizi maana zilikuwa ndoa za kushitukiza lakini zilisaidia baadhi ya watu kupata wake na hata watoto maana NDOA YA MKEKA HAINA MAARI.
Katika hili Mwanakwetu ana hakika wapo watoto wengi katika JIJI LA DAR ES SALAAM waliozaliwa kwa NDOA ZA MKEKA na pengine hata wewe unayeyasoma makala haya umezaliwa kwa NDOA YA MKEKA.
Jamaa wakaanza kumsaka mkina SAMATTA saka saka na wewe saka, saka na wewe hadi mwisho wa siku hawakuwapata. Zamu ikahamia kwa mkina MAKWEGA, msako wa ndoa ya Mkeka unaendelea saka saka na wewe saka saka na wewe. Wakati huo Mwanakwetu yupo Sekondari akahamishiwa Same huku jamaa wanaendelea kumsaka ndugu wa Mwanakwetu ili kumfungisha ndoa ya Mkeka. Jamaa wakiwa katika harakati hizo Disemba moja ya wakati huo Mwanakwetu yu likioz akawaambia hawa ndugu;
“Nyinyii ebu achene ujinga wenu tambueni hili NDOA YA MKEKA ni batili kwa dini ya KIISILAMU sasa mtawezaje kumfungisha ndoa hii MKRISTO na binti yenu Isilamu? Hapa mtakuwa mnapoteza muda tu. Kama BATILI KWA MUISILAMU KWA UKRISTO NI HARAMU. Jamaa hawa wakacheka sana msako wao uliendelea.”
Kwa hakika hadi tamati siyo mkina SAMATTA wala mkina MAKWEGA hakuna aliyefungishwa NDOA YA MKEKA japokuwa mahusiano haya ya ndugu wa Mwanakwetu yaliweza kuzaa matunda.
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
Kwa hakika shabaha za makala haya zipo nyingi kubwa ni mahuisiano mazuri baina ya UKRISTO na UISILAMU ni jambo la enzi, kuna kuoleana na hata kama hakuna kuoleana kuna kuzaliana, hata kama hakuna kuzaliana lakini pia mliwahi kuishi pamoja maishani maana na huu pia ni udugu.
Hiki ni kisa cha kweli cha MBAGALA, natambua wewe msomaji wangu unavyo visa vingi unavyovifahamu juu na maelewano na maisha baina ya WAKRISTO na WAISILAMU hapo ulipo naomba na wewe msimulie aliye jirani yako siku ya leo.
Mwanakwetu upo?
Je makala haya yaitwaje? Wakristo na Waisilamu wa Mbagala? Ndoa ya Mkeka?Au Muisilamu Batili Mkristo Haramu?
Mwanakwetu anachagua Muisilamu Batili Mkristo Haramu.
Nakutakia Siku Njema.
0717649257








Ndoa ya Mkeka MHARI IKO PALE PALE ISIPOKUWA Muoaji Kwa wakati anatamkiwa kiwango cha mahari kama anacho kiasi anatoa na kama Hana Wanampatia kidogo na Kingine atammalizia Mkewe taratibu huko baadae.
ReplyDeleteHiyo ni Ndoa Halali japo izingatie Mashahidi ,makubaliano (Muoaji na muolewaji) pia Mahari ni vitu Muhimu
Ndoa hii inaepusha Kuendelea Kufanya machafu miongoni mwa hao wenza nakupelekea Kuchuma Madhambi
Post a Comment