MTIHANI WA UPIMAJI DARASA LA PILI NI KUPOTEZA PESA ZA UMMA

 


 Adeladius Makwega-MBAGALA

Asubuhi ya Novemba 17, 2025 nilipigiwa simu juu ya kijana wangu anayefahamika kama Adrian Adeladius Makwega anayesoma darasa pili kuwa;

“Huyu mswahili anakwenda kufanya Mtihani wake wa taifa unayofahamika kuwa Mtihani wa Upimaji wa Darasa la Pili, naomba mtakie heri.”

Kwanza majibu ya Mwanakwetu yalikuwa ya mshangao sana; Nayeye aliyepiga simu akasema;

“Eeeeh wana mtihani! Nadhani yeye ni miongoni mwa wale wanaoishia darasa la sita…”

Jukumu la kumtakia heri mtahiniwa huyu lilifanyika vizuri kisha Mwanakwetu kuendelea na ratiba yake. Kwa kuwa alipita jirani na Ofisi ya Elimu ya Mkoa alipo aliwatafuta Maafisa Elimu Mkoa huo na kwa bahati mbaya hakuwapata pengine walikuwa bize na mtihani huu. Baadaye Mwanakwetu alipotafiti alitambua kuwa ni kweli mtihani huu upo kukiwa na maelezo mengi miongoni mwao ni haya;

“Usimamizi wa Upimaji wa Darasa la Pili ufanyike kwa kuzingatia Mwongozo wa Upimaji wa Kitaifa wa Stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu Darasa la Pili Ngazi ya Shule unaopatikana kwenye tovuti ya Baraza la Mitihani la Tanzania.”

Mwanakwetu kwa kuwa ni mwalimu kwa TAALUMA na ni kazi yake ya kwanza kuisoma na kuifanya ni hii akiwa amefundisha elimu ya msingi na Sekondari nchini Tanzania kwa miaka karibu kumi aliamua kufanya utafiti mdogo juu ya hali ilivyokuwa chumba cha mtihani wakati mtihani huu unafanyika na hali ilikuwa hii;

“Kwa Shule za ENGLISH MEDIUM wataendelea kufanya vizuri kila siku, mimi sikuona haja ya Serikali ya Tanzania kukimbilia hili suala la kumaliza Shule ya Msingi Darasa la Sita , Kama nia hii ilikuwa nzuri ilikuwaje Rais John Pombe Magufuli alilikataa? Ilikuwaje baada ya kifo chake suala hili likarejeshwa?”

Mwanakwetu alibaini kuwa kwa hali ilivyokuwa vyumba vya mtihani wanafunzi wa shule za umma namna walivyokuwa wakijibu maswali inaonesha kuwa bado wana uwezo mdogo wa kuweza kuzimudu stadi za KUSOMA, KUANDIKA na KUHESABU.

“Kwa shule zetu za kawaida kulikuwa na imla ya maneno ya Kiingereza wanafunzi wengi nimegundua wameweza kuandika na kujibu vizuri neno moja tu la BANANA maana linaandikwa kama neno la KISWAHILI mathalani kwa maneno mengine ya Kiingereza kama TIE –Walijibu TAI, BY-Wamejibu BAI,ONE-Wamejibu WANI, TEACHER -Wamejibu TICHA, CAT-Wamejibu KATI...”

Haya ni kwa mujibu wa uchunguzi wa Mwanakwetu kama mwalimu na kama mzazi na hiki ni kilio kwa shule zetu za umma. Kwa hakika hali kwa masomo mengine mawili kidogo ilikuwa na nafuu kwa mujibu wa utafiti wa Mwanakwetu.

 

“Ifahamike wazi Shule za Serikali ndizo Shule wanasoma watoto wengi wa Watanzania, mitihani hii ni migumu sana, mitihani hii ni kupoteza pesa za umma. Huku wingi wa wanafunzi nayo ni shida nyingine darasa moja lina wanafunzi hadi 300, mitihani hii ni kwa wanafunzi ambao ni hawazidi 20 wa shule binafsi tu. Mwalimu shule za umma ana wanafunzi 200 anafundishaje darasa lake?Hapo darasani utakuwa wengine wanasikiliza,wengine wamelala, wengine wanaruka juu wengine wamekaa hivi,wengine wanapigani, wengine wanaumwa, mwingine hajakula chakulajana…

hii mitihani ni shida sana.

Watoto hawa wa darasa la pili wangeecha waingie darasa la tatu nawaje kufanya mitihani wa upimaji darasa la la nne kama zamani.”

 

Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?

Kwa hakika ukifanya thathimni ya mitihani hii na hata wale walioamua kurejesha elimu ya msingi kuishia darasa la sita wengi wao waliofanya maamuzi haya watoto wao hawasomi katika shule hizi za umma , watoto wao wanasoma shule binafsi huku watoto wa Watanzania wengi wanasoma shule za umma. Shida ambayo Mwanakwetu anaiona ya Tanzania ya leo ni hii;

“Wanaofanya maamuzi ya mambo mengi huwa wao siyo walaji wa yale matokeo ya maamuzi yao.”

Mwanakwetu anaamini haya;

“Watoto wa Kitanzania waliofanya mtihani wa darasa la pili mwaka wa 2025 hasa wale wa shule za umma hawakuhitaji kufanya mtihani huu wa upimaji, bali Tanzania tuendelee na ule ule utaratibu wa elimu wa zamani wa miaka mwili chekechea, miaka saba msingi, miaka minne sekondari, miaka miwili kidato cha tano na cha sita na miaka mitatu/minne ya chuo kikuu Shahada ya Kwanza, miaka miwili ya Shahada ya Uzamili na miaka mitatu/minne/mitano ya Shahada ya Uzamivu.”

Mwanakwetu Upo? Kumbuka;

“Upimaji Darasa la Pili Kupoteza Pesa Za Umma.”

Nakutakia Siku Njema.

makwadeladius@gmail.com

 0717649257

 


 

 

 

 

 












 


 

 

 










0/Post a Comment/Comments