Adeladius Makwega-Musoma MARA
Katibu Tawala Mkoa wa Mara Mwalimu Gerald Musabila Kusaya Novemba 27, 2025 ameipongeza Idara ya Miundombinu husasani Injinia Baraka Mwashambwa ambaye ni Meneja Mradi wa Ukarabati na Ujenzi wa Ofisi ya Hazina Ndogo iliyopo mkabala na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mara ambayo inafanyiwa ukarabati mkubwa ambapo sasa wamefikia asilimia 95 na kazi inafikia ukiongoni.
“Nawapongeza watumishi wangu wote na kamati nzima kwa kuisimamia kazi hii vizuri sana na inakamilika kwa wakati, kikubwa nawaagiza muikamilishe mapema ili Hazina Ndogo warudi jengoni waendeleee kutuhudumia.”
Katibu Tawala Mkoa wa Mara awali alikagua mradi huu hatua kwa hatua huku akiyabaini mapungufu kidogo na akiagiza yakamilike haraka.
Katika ziara hii Katibu Tawala Mkoa wa Mara alimbatana na Wakuu wa Idara kadhaa katika ukaguzi wa ujenzi wa jengo hili unatumia karibu shilingi milioni 100 na ushehe.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Mipango na Uratibu Emmanuel P. Mazengo akiwa katika msafara huu alisema kuwa jengo hilo limejengwa vizuri na linakamilika kwa wakati , huku ukiwa mradi wa kupigiwa mfano.
“Mimi ni mtaalamu wa Mipango na Uratibu nilikuwa naangalia ujenzi wa jengo hili, nimebaini linafuata taratibu zote, hatua zote zimefuatwa vizuri na linakamilika kwa muda sahihi, huku changamoto chache zipo pia nimeona zinatatuliwa kwa wakati.
Nadhani mradi huu sasa ni mradi wa mfano, wenzetu kwa ngazi za Halmashauri ya Wilaya wanaweza kuja kujifunza namna mradi huu unavyotekelezwa tangu awali.”
Wakuu wengine wa Vitengo waliokuwepo ni Jonathan Kimaro-Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini na Timoti Kimaro Mkuu wa Kitengo Ugavi na Manunuzi, kwa upande wake Timoni Kimaro ambapo ziarani pale lilipotajawa jina KIMARO wote walishituka hivyo ilibidi anayemtaja Kimaro alitaja KIMARO wa Manunuzi au KIMARO wa Tathmini, huku watumishi wengine wakitumia KIMARO mkubwa na KIMARO mdogo.
Akizungumzia kukamilika kwa kazi hiyo ambayo tano asilimia imesalia KIMARO wa Manunuzi ambaye ndiye KIMARO mdogo alisema kuwa WAZABUNI ndiyo wamekwamisha asilimia hizo lakini sasa limeshapatiwa ufumbizi, vifaa wa umeme na TEHAMA vitafika na kazi itakamilika;
“Tulipata WAZABUNI wawili wakatuangusha walituletea vifaa vinavyapata kutu havikuwa na ubora tukavikata, tukavikata kabisa lakini sasa tumepata mzabuni makini na vifaa vitafika na kazi itakamilika hivi punde.”
Nyuma ya pazia ya ziara hii ya Katibu Tawala Mkoa wa Mara , wajumbe wa Kamati ya Ujenzi walikuwa wakinong’ona kuwa watamuomba Katibu Tawala Mkoa wa Mara Mwalimu Gerald Musabila Kusaya atoe angalau BAKISHISI kwa kamati hiyo kama pongezi kwa kazi nzuri iliyokamilika.
Wakati wanajadili chini kwa chini , Mwanakwetu aliwasikia walipobaini hili wakasema hapa Mwanakwetu tunafanyaje? Mwanakwetu akawajibu;
“Muandikieni barua ya kukamilika mradi, kisha pachikeni neno lenu katika aya ya mwisho ya waraka wenu wa kukabidhi mradi huu, lakini mkipata BAKISHISI hiyo na mie msinisahau.”
Msomaji wangu haya ni mradini hapa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Wakati haya yakiendelea, hali ya hewa ya Mji wa Musoma ni nyuzi joto 27 sentigredi , upepo ukivuma kwa KM 14 kwa saa, unyevunyevu ni wa asilimia sufuri na ujirani na mvua ni wa asilimia 54 huku mitaani Mjini Musoma wachuuzi wa Dagaa Mitaani wakiendelea kuanika dagaa zao.
0717649257
Post a Comment