Majira ya jioni, Mwanakwetu yupo Mjini Musoma Mkoani mARA, hii ikiwa ni Novemba ya mwaka wa 2025, anarudi nyumbani kwake. Akiwa njiani akamuomba bodaboda amshushe tu pahala ambapo kunauzwa viazi na bucha ya nyam, ili anunue kisha akachemshe hivyo vikiwa vyakula vyake vya siku mbili.
Kijana wa bodaboda akashukuru sana maana analipwa pesa ya safari ndefu na kumbe safari ni fupi, bodaboda kamshusha mteja na bodaboda akarudi alipotoka.
Kando ya eneo aliposhuka Mwanakwetu kulikuwa maduka kadhaa huku garandinga na POLISI la Rangi BLUU likiwa kando. Asakari mmoja yupo chini kaegemea kichwa cha karandinga hili kwa mbele kwenye boneti kama kachoka hivi , huku vijana wengine polisi wakiwa kando mikononi wana mitutu.
Mwanakwetu akanunua viazi vya shilingi 2,000/ huku yakiwa mafungu mawili, fungu moja msomaji wangu bei yake ni shilingi 1000/-, kisha kununua nyama kilo shilingi 12,000/- Alipomaliza manunuzi haya akaanza kutembea kwa miguu kurudi kwake huku huu ukiwa umbali kama wa KM 1.
Mwanakwetu anatembea kushoto kulia, shoto kulia, gafla akasikia saut inaita baba…. Babaaa…. Babaaaaa… mara anayeita baba yu miguuni mwa Mwanakwetu.
Huyu nivmtoto wa kiume akamsalimia Mwanakwetu Shikamo! Mwanakwetu akajibu marahaba. Akili ya Mwanakwetu ikachuma dhambi akijua wale wale watoto wanaosalimia kisa Shikamoo Naomba Mia.
Huyu mtoto mdogo wa kiume akawa anayasema maneno huku Mwanakwetu hayasikii vizuri.
Kisha akamuuliza unasemaje?
Kijana huyu mdgo akauliza, unanikumbuka? Mwanakwetu akajibu hapana.
Kijana huyu akasema;
“Mimi naitwa ….. Istambuli, nasoma darasa la pili Shule ya Kimataifa…wewe tulikaa wote kulee. Tulikaa na wewe vizuri sana, tulikuwa tunachangia mita ya umeme na maji, wakati mwingine umeme ananunua mama na wakati mwingine umeme unanunua wewe. Yule mdogo wangu mdogo sasa hivi mkubwa, anatembea, amekuwa mkubwa sasa…Unamkumbuka ? Yule mweupeee kama mzungu… mimi ni mweupe lakini yeye mweupe zaidi yangu.”
Mwanakwetu anamsikiliza huyu kijana mdogo kisha Mwanakweu anakumbuka kuwa haya yanasemwa ni ya kweli yakiwa ni tukio la miezi karibu 11 nyuma.
Kijana mdogo anaendelea kuongea;
“Pale sisi tulihama, mama alipata nyumba nyingine, pale kwenye geti jeusi kila siku tunakuona unapita , mimi , mama , dada na wadogo zangu tunakukumbuka na tunakuona mara nyingi unapita…”
Mwanakwetu akasema sasa Istambuli kumbe kila siku mnaniona mbona hamniiti? Jamani Vibaya hivyo?Kwanza mmehama hata kuniaga?Nakuja kujua baadaye baada ya mwalimu kuniambia. Instambuli akajibu -Tunakuita sana lakini unakuwa mbali mno, wakati mwingine unapita na bodaboda. Leo tumekutana nikasema lazima nikwambie.
Kijana huyu mdogo anaongea vizuri sana na Istambuli kashika usukani wa mazungumzo.
“Kumbe wewe umeshaanza kwenda kazini ? Mama bado, Mama badoo… hajaanza kwenda kazini,n asikiwa watu wamepigwa mabunduki, watu wamepigwa bundukiii….wamekufaa...wamekufaa. Hata mimi sijaanza kwenda shuleni…
Watazikwa makaburi hayaaa eheeee…?
Haya baba kwa heri, mimi nimefika kwetu dada alinituma nikaweke nyimbo katika flashi yake , kwa heri eeeee….”
Yule kijana akaingia ile nyumba yeye ukutwa mkubwa nyumba kadhaa na geti jeusi nayeye Mwanakwetu kuendelea na safari.
Mwanakwetu akiwa njiani alikumbuka mambo makubwa matatu kwanza umri wa Istambuli ulikuwa ni miaka tisa na anasoma darasa la pili, huku akitambua kilichokea mara baada ya uchaguzi mkuu wa Tanzania Oktoba 29, 2025.
Hapa hapa Mwanakwetu alikumbuka kuwa na yeye akiwa na umri huu huu wa Istambuli mwaka 1984 anakumbuka vifo viwili kwanza cha rafiki yao waliokuwa wanasoma naye darasa la pili, darasa zima walicharwazwa bakora nyingi na mwalimu mmoja aliyekuwa mjamzito, kisha shule kufungwa na shule ilipofunguliwa walijulishwa kuwa mwenzao mmoja aliumwa sana likizoni na kufariki wakati wa likizo.
Jambo la pili ni kifo cha pili anachokikukumbuka ni cha Edward Moringe Sokone ambaye aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati huo.
Jambo la tatu ambalo Mwanakwetu alilikumbuka na jina ISLAMBULI likiwa ni jina la kiarabu ambalo limepewa mji na mitaa kadhaa kama vile INSTAMBUL UTURUKI huku likifanana na jina la askari wa kiarabu wa Misri mwanamgambo wa Udugu wa Kisilamu Khalid al-IslambulI aliyemdungua kwa risasi Rais wa tatu wa Misri Anwar Sadat Oktoba 6, 1981.
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
Naomba msomaji wangu siku ya leo niseme kwa kifupi mno hasa juu ya kijana Istambuli ambaye ameshuhudia haya yaliyotokea mwaka wa 2025 kwa hakika hali hii haiwezi kuondoka akilini mwake ataishi nayo milele fikiria tu Mwanakwetu anavikumbuka vifo viwili vya mwaka 1984 kile cha rafiki yake na hiki cha Edward Moringe Sokoine, tangu mwaka 1984 hadi mwaka 2025 ni miaka 41. Hii misiba inaishi na Mwanakwetu akilini. Nakuomba msomaji wangu chukua mwaka wa 2025 jumlisha miaka 41 jibu lake itakupa mwaka 2066.
Naomba viongozi wote duniani wazingatie haya;
“Ukiwa kiongozi usifikirie tu hata siku moja kuagiza watu wadunguliwe kwa risasi tu, fikiria madhara ya hilo tukio kwa taifa la watu zaidi milioni 100-150 hapo kesho.”
Mwanakwetu upo ?
Je makala haya yaitwaje? Dada Alinituma Nikaweke Nyimbo Katika Flashi, Shikamoo Naomba Mia, Istambuli Jirani wa Mwanakwetu? MADHARA YA KILE ULICHOAMUA ? Wewe msomaji wangu chagua kichwa kimoja kati hivyo lakini wewe kumbuka yale Madhara ya Kile Ulichoamua .
Nakutakia Siku Njema.
0717649257



















Post a Comment