Adeladius Makwega-Musmoma MARA
“Ninahitaji madereva wawe wanakaa sehemu salama, ofisi yao iwe na runinga kubwa, hii runinga ndogo iondolewe mara moja, wawekeeni jokofu la kuweka maji na vyakula vyao, Nataka kuona chumba hiki kipo maridadi na chumba hiki kipakwe rangi vizuri.
Kuna wakati nakuta kuna vitu vinahifadhiwa hapa, hili silitaki, naagiza pajengwe chumba cha kuhifadhi vitu vyao na siyo hapa. Madereva wetu tunawakabidhi magari yenye thamani kubwa lazima mazingira yao ya kazi yawe bora na yalingane na thamani na mali za umma wanazokabidhiwa”
Haya ni maelezo ya Katibu Tawala Mkoa wa Mara Mwalimu Gerald Musabila Kusaya akiyatoa kwa idara ya Utawala na Rasilimali Watu ofisi ya Mkoa wa Mara Novemba 27, 2025 majira ya mchana wakati akikagua ofisi maalumu ambayo Maafisa Usafirishaji wa Ofisi ya Mkoa wa Mara hukaa wakati wakiwangoja viongozi wao kuelekea katika shughuli mbalimbali.
Mwalimu Kusaya alisema kuwa anahitaji maafisa hawa wafanye kazi vizuri, hivyo mazingira ya kazi zao lazima yawe yakuvutia.
“Magari yao wanayatunzwa vizuri, mazingira ya ndani ya magari yapo safi na salama, wanatuendesha vizuri na ndiyo maana maafisa na viongozi wote Mkoa wa Mara tunachapa kazi vizuri, ndiyo maana leo nimeamua kutembelea ofisi yao yao.”
Akimalizia ukaguzi huu Katibu Tawala Mkoa wa Mara alisema kuwa kwa sasa ofisi yake ina madereva wanaokaribia 18, huku wakiwa na magari zaidi na wakitarajia kupokea basi jipya lenye thamani ya karibu milioni 300 ambalo linabeba abiria kati ya 40-50 ambalo litawasaidia watumishi katika shughuli mbalimbali za kazi, za kijamii na za kimichezo.
Akipokea maagizo haya Afisa Usafirishaji Mkuu Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara Bi. Maisha Binti Mwaisengela alisema kuwa ameyapokea maagizo haya na yatatekelezwa haraka iwezekanavyo.
Wakati haya yakiendelea ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, hali ya hewa ya Mji wa Musoma jua kali likiwaka, huku mitaani wananchi wakiendelea kuanika dagaa zao kutoka Ziwa Victoria.
0717649257
Post a Comment