MAANA YA MARIDHIANO NA MWELEKEO WAKE KATIKA SIASA ZA TANZANIA

 


Timothy Lugembe,

Mwanakwetu blog.

Katika lugha ya kisiasa, maridhiano hurejea mchakato wa kukubaliana na kusameheana kati ya pande zilizotofautiana ili kurejesha mshikamano, kuondoa msuguano na kujenga uhusiano mpya wa kuaminiana.

Ni hatua ya kuzungumza, kutambua makosa ya nyuma, na kuweka msingi wa kufanya siasa kwa amani , uwazi na haki.

Kwa upande wa Tanzania, dhana ya maridhiano imeibuka upya kufuatia sintofahamu za kisiasa zilizotokana na malalamiko ya ukiukwaji wa haki wakati wa chaguzi, kukamatwa kwa watu, migogoro baina ya vyama na hisia za mgawanyiko katika jamii.

Majukwaa ya kisiasa, taasisi za kiraia na viongozi wa dini wametumia muda mwingi kusisitiza uhitaji wa kukaa meza moja ili kujenga taifa lisiloendeshwa na hofu na mivutano.

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan siku chache zilizopita ameitisha maridhiano lengo likiwa ni kujenga taifa lenye umoja na mshikamano na kusahau dosari zilizotokea kabla na baada ya uchaguzi wa oktoba 29 mwaka huu.

Bado maridhiano hayajafanyika ila serikali ya Tanzania inafanya jubudi kubwa kuhakikisha maridhiano yanafanyika na taifa linarudi kwenye Hali yake ya amani na upendo.

Kwa kifupi, maridhiano nchini Tanzania ni juhudi za kurejesha imani ya kisiasa, kuponya majeraha ya nyuma na kuunda mazingira ya demokrasia yenye ushirikishwaji, amani na haki kwa wote.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments