Adeladius Makwega-MBAGALA
Novemba 18, 2025 Mwanakwetu alipita pahala fulani Musoma Mjini ambapo aliwapiga picha jamaa wawili Ester Musa Mwangaza na Switbert Sigisbert Mwasumira.
Picha hii kuipiga haikumvutia Mwanakwetu tu kwa sababu ya wajihi wa ndugu hawa la hasha bali kutokana na sababu moja muhimu sana juu ya mhusika mmoja pichani.
“Ester Musa Mhangaza ni Karani wa Idara ya Mipango na Uratibu Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Ester Mhangaza ana sifa moja ya kuwa ni Karani Mkarimu kwa kila anayefika ofisini kwake kumuona Mkuu wa Idara hii anayeitwa Emmanuel Mazengo.”
Mara nyingi Mwanakwetu akiwa na maswali juu ya Idara ya Mipango na Uratibu huwa Mkuu wa Idara hii Emmanuel Mazengo huwa anamtania Mwanakwetu akisema;
“Mwanakwetu nakuonaaa… upooo… na Ester?”
Mwanakwetu nayeye hujibu ,
“Ndiyo Bosi Emmanuel Mazengo, Leo Nipo na KARANI wako MKARIMU.”
Najua msomaji wangu itakuwa busara kama ukamfahamu zaidi Ester Mhangaza ni nani?.
“Ester anazaliwa na baba anayeitwa Musa Mhangaza Senguyumva na mama Rozalia Paul Birabamo kutoka Kijiji cha Mkididili , Kata ya Ngara Mjini , Wilaya ya Ngara Mkoa wa Kagera. Kidato cha kwanza hadi cha nne amesoma Ngara Sekondari na baadaye kujiunga na Chuo cha Utumishi wa Umma Tabora huku aliajiliwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara mwaka 2018.”
Swali la Mwanakwetu kwa Ester siku hiii lilikuwa ni moja tu, inakuwaje unaitwa Ester Mhangaza na wakati pia kabila lako ni Mhangaza?
Majibu ya Ester Musa Binti Mhangaza yalikuwa haya;
“Hili ni jina tu la Babu alikuwa akiitwa Mhangaza.Sifahamu sababu yake ya kuitwa hivyo, ndilo jina letu la ukoo.”
Msomaji wangu haya ni picha hii ya Novemba 18, 2025.
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
Mwanakwetu alipokuwa mdogo sana nyumbani kwao Mbagala Sabasaba miaka 1980 mwanzoni alihamia Mzee Mmoja Mpare aliyekuwa Katibu wa CCM wa Kijiji cha Mbagala anaitwa SAKAPALA akitokea Chuo cha CCM Lushoto ambacho sasa ni Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA).
Mzee huyu alikuwa na familia ya watoto wengi wa kike kwa wakiume, miongoni mwao ni Binti aliyeitwa HADIJA. Tukiwa wadogo mtaani kulikuwa na HADIJA wengi sasa tukiwa tunacheza michezo ya Kula Mbakizie Baba, Baba Kasema, Mchezo wa Kombolela, Michezo ya Kujificha,KWIKWIDE, Hodi HODI KARIBU na NYAMANYAMA,
Tukawa na changamoto ya kuwatafautisha HADIJA MINANGU, HADIJA MANDWANGA na HADIJA SAKAPALA Tunafanyaje?
Tukaamua kuwapa majina ya Koo zao ya utani;
“HADIJA MINANGU tukamuita HADIJA TAKSI maana baba yake alikuwa anamiliki motokaa, Hadija Mandwanga tukamuita HADIJA MTUMBWI maana baba yake alikuwa anamiliki Ngalawa na huku HADIJA SAKAPALA tukamuita HADIJA MPARE kwa kuwa alizawa na mama Msambaa na Baba yake Mpare.”
Ndiyo kusema inawezekana Babu wa Ester Musa Mhangaza aliitwa jina la kabila lake ili kumtafautisha na watu wengine wenye majina yanayofanana kijijini kwao.
Mwanakwetu Upo? Kumbuka
“KARANI WAKO MKARIMU.”
Nakutakia Siku Njema.
0717649257
Post a Comment