Adeladius Makwega-MBAGALA
Siku hii palikuwa na na Kikao cha Uchaguzi wa Viongozi wa Jumuiya ya Mtakatifu Sesilia ambayo ilikuwa Jumuiya kubwa kidogo katika Parokia hii.
Parokia husika ilimtuma Katibu wa Parokia kusimamia uchaguzi huu, huku Jumamosi moja kabla ya Jumamosi hii ya uchaguzi wa jumuiya hii Paroko wa Parokia kusika alifika na kufanya misa katika nyumba ya mama mmoja Mkatoliki mzuri ambaye alikuwa ni Askari Mstaafu wa Jeshi la Polisi ambayo nyumba hii hata siku hii ya uchaguzi wa viongozi unafanyika hapa hapa kwa hoja kuwa alikuwa na eneo kubwa na hili lilikuwa sahihi kabisa. Siku hii ambayo Paroko anafanya misa katika Jumuiya ya Mtakatifu Sesilia Paroko wetu baada ya misa alisema maneno haya;
“Hii jumuiya yenu ni kubwa, hivyo tumeamua kuigawa mara mbili kaya hizi za hapa zinabaki Jumuiya ya Mtakatifu Sesilia na zile kaya za kule zitakuwa Jumuiya mpya ya Mtakatifu Biligita. Ebu niwaulize swali siku ya leo, hapa jumuiyani ni kaya ngapi ambazo zinatarajiwa kuwa katika Jumuiya ya Mtakatifu Biligita zimefika? Nawaombeni msimame.”
Hapa alisimama mama mmoja ambaye alikuwa pia ni kiongozi katika jumuiya ya Mtakatifu Sesilia ,huku Padri Msukuma akasema maneno haya;
“Mama upo mwenyewe tu? Lo salale! Mmeomba jumuiya lakini hamsali jumuiya, maana yake hamji kusali hata dominika, mama sasa kweli peke yake utaweza kumuwakilisha vizuri Mtakatifu Biligita?Naombeni mpeni Mikrofoni aseme shida ni nini?”
Baba Parokia asante;
“Pale tupo Wakatoliki wengi, ninawafuata mara nyingi majumbani mwao lakini wezagu lakini hawatoi ushirikiano. “
Paroko akauliza ni Wakatoliki? Mama akajiby ndiyo. Paroko akasema maneno haya kwa ukali;
“Nawapeni tahadhari, katika parokia hii sitaki hizo tabia, kutaneni haraka na wenzako huko mlipo, waambie Padri kasema mbadilike na msipobadilika hii jumuiya mpya haitoanzishwa, kawaambie wenzako Paroko anasema kwanza washiriki shughuli zote za jumuiya, waje kanisani kusali huku watoe michango yote inayotakiwa na Kanisa. Hivi nyinyi ule ukanda wote si mnafanya kazi kutoka Vyombo Vyetu vya Ulinzi na Usalama ?(Ndiyo Baba Paroko) Kwanini hamuwi mfano kwa jamii inayowazunguka? Hii jamii ya Watanzania masikini Wakulima na Wafugaji inawaonaje? Kwani kulipa zaka ni kiasi gani? Kusali Jumapili unatumia siku ngapi? Kujumuika na Wakristo wenzako shida nini? Ni kiasi gani? Nawaombeni muwe mfano kwa hii jamii watendeeni mema hii jamii nyinyi ni mawakala wa Kanisa popote milip... Binafsi mimi kama Paroko natoka katika jamii hii hii na hata nyinyi huku kwenu mnatoka katika jamii hizi hizi. Si mmebatizwa, si mmepata Komuniyo ya kwanza na si mmpata Kipaimara na wengine hadi na ndoa. Nawaombeni mjirekebishe.”
Msomaji wangu kumbuka hii Jumamosi ya siku aliyokuja Paroko, Padri Msukuma aliondoka zake na siku ya Uchaguzi wa Viongozi wa Jumuiya Kongwe ya Mtakatifu Sesilia ilifika na alikuja Katibu wa Parokia hii kuusimamia uchaguzi husika. Katibu Parokia alisema kuwa Padri aliwasamehe wale jamaa wa jumuiya mpya na uchaguzi wa viongozi wao utafanyika Jumamosi inayofuata , huku zile kaya zinazogawanywa katika Jumuiya ya Mpya zikishiriki lakini hazitopiga kura. Kabla ya uchaguzi huu Changamoto ya Jumuiya hii ilikuwa ni moja,
Mwenyekiti aliyekuwa anamaliza muda wake alikuwa Mwalimu wa Sekondari kidogo alikuwa anashindwa kuwadhibiti vijana Wakatoliki kutoka Vyombo vya Ulinzi na Usalama wakimuona kama mwalimu.
Uchaguzi unafanyika kwa ngazi zote sasa nafasi ya Mwenyekiti imefika majina yalipendekezwa ni haya jina la kwanza la Mwalimu yule yule wa Sekondari ili kuendelea. Katibu wa Parokia akasema hapana pendekezeni na jina lingine ili kura zipigiwe majina mawili maana Kanisa Siyo Fukara Wa Walei kisha muungwana mwingine akapendekeza jina la kijana mmoja wa Kihaya ambaye alikuwa nafasi ya Mkurugenzi wa Idara Moja ya Sera na Mipango , haya majina mawili yakapigiwa kura na huyu Kijana wa Kihaya akashinda na yeye kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya hii. Katibu wa Parokia akasema kuna nafasi imebaki kiporo kunakaka mmoja yule mweusi nyuma nampendekeza na yeye na jina linguine wagombee nafasi ya mwenyekiti wa UWAKA wa Jumuiya hii, Jumuiya ikakubali, kura zikapigwa kaka Mweusi akashinda ambaye ndiye Mwanakwetu.Uchaguzi ulikamilika vizuri na juma lililofuata zamu ikawa kwa Jumuiya ya Mtakatifu Biligita nayo ikapata viongozi wao.
Mwanakwetu anasema nini Siku ya leo?
Kanisa la Tanzania lina mchango mkubwa katika kuhakikisha waamini wake bila kujalia kazi zao wanazofanya wanaishije katika maisha yao ya kila siku, kikubwa kama siye waamini tunachepuka kanisa lazima lijitahidi kutuuidisha katika kundi na hilo ni jukumu kubwa la Kanisa la Tanzania kwa sasa.Kwa hakika tangu mwaka wa 2016 Vyombo vya Ulinzi vya Tanzania vinalalamikiwa mno na hali imekuwa tete Oktoba 29, 2025 na siku zilizofuata. Kanisa kwa sasa lina jukumu kubwa la kujua wale waamini wake katika kila linalotokea mikono yao imeshiriki kufanya nini katika haya yalitokea? Kama yupo MKRISTO aliyekengeuka lazima KANISA lihakikishe anarudishwa kundini, hapa tangu kwa aliyemdogo hadi Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi za Usalama ambao ni WAKRISTO ambapo tumeshuhudia Watanzania wakidunguliwa na kupopolewa kwa risasi,mwaka wa 2025 WATANZANIA wamekuwa ndege? Kinyangarika Gani Hiki Kimefanya Huu Ufedhuli? Kwa hakika wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama lazima wawajibike hakuna kuficha katika hili. Kisha ndipo tuje kwa walio wadogo mmoja baada ya mwingine.Kumbuka maneno yale, yale yale ya Parokia ile yenye jumuiya kadhaaa zikiwamo Jumuiya za Mtakatifu Sesilia na Biligita zilizotajwa katika kisa hiki;
“… katika parokia hii sitaki hizo tabia, kutana na wenzako huko mlipo, waambie wabadilike na msipobadilika hii jumuiya mpya haitoanzishwa, kawaambie wenzako Paroko kasema …washiriki shughuli zote za jumuiya, waje kanisani kusali huku watoe michango yote inayotakiwa na Kanisa, nyinyi ule ukanda wote si mnafanya kazi kutoka Vyombo Vyetu vya Ulinzi na Usalama ? Kwanini hamuwi mfano kwa jamii inayowazunguka? Hii jamii ya Watanzania masikini Wakulima na Wafugaji? Kwani kulipa zaka ni kiasi gani? Kusali Jumapili unatumia siku ngapi? Kujumuika na Wakristo wenzako shida nini?Ni kiasi gani? Nawaombeni muwe mfano kwa hii jamii, watendeeni mema hii jamii maana Nyinyi ni Mawakala wa Kanisa Popote Mlipo .
Mimi huko kwetu natoka katika jamii kama hii hii na hata nyinyi huku kwenu mnatoka katika jamii hizi hizi. Si mmebatizwa, si mmepata Komuniyo ya kwanza na si mmpata Kipaimara na wengine na ndoa .Nawaombeni mjirekebishe.”
Haya yalikuwa maneno makali na maneno sahihi kwa wahusika siku hiyo na ujumbe ulifika.
Kwa hakika yanayosemwa ni mengi ikiwamo utekaji, utesaji,ubakaji, ulawiti , baadhi ya jamii zinalalamikiwa kuhasiwa, kubwa zaidi kudunguliwa, kupata vilema na wengine wameuwawa wapo waliopata mili na wafu wao na wapo pao wanaoitafuta miili hiyo hadi sasa na wengine kuzika nguo.Mwanakwetu anaamini kuwa katika ufedhuli huu wapo WAKRISTO na Wapo WAISILAMU kutoka katika taasisi hizi zinazolalamikiwa wameshiriki kuufanya utovu huu wa nidhamu lazima hapa lazima Kanisa liwaadhibu, tangu viongozi hadi wadogo kinyume chake vijana wadogo katika vyombo vya Ulinzi na Usalama ambao ndiyo kwanza wameanza kazi wanajifunza nini? Hapo baadaye wanaweza kufanya matukio zaidi ya haya ya aibu.
Ebu tujiulize hii hoja ya baadhi ya watu kuasiwa pata picha hii;
“Wewe unayewahasi wenzako kama baba yako angehasiwa, je ungeweza kuzaliwa katika huu ulimwengu? Kama babu yako, babu yako hakuhasiwa na wewe usiwhasi wengine.”
Kwa hakika kwa leo inatosha sana.
Mwanakwetu upo? Kumbuka;
“KANISA SIYO FUKARA LA WALEI”
Nakutakia Siku Njema.
0717649257
















Post a Comment