Adeladius Makwega-MBAGALA
“Wakati wa hatari ya moja kwa moja au wakati wa kukabiliana kifo kilicho karibu, sala mara nyingi huzingatia kumwomba Mungu ulinzi,nguvu, amani, na rehema, pamoja na kukabidhi roho katika utunzaji Wake.Huku Zaburi 91 na Zaburi ya 23 huzingatiwa.”
Haya ni maelezo ya ndugu mmoja kutoka mkoani Kigoma ambaye alikutana na Mwanakwetu na kuzungumza naye katikati ya Novemba 10-18, 2025 Mkoani Mara. Ndugu huyu akasema yeye kama Mkatoliki pia hutumia sala hii,
“Nakukimbilia Ulinzi Wako, Mzazi Mtakatifu Mama wa Mungu , Nilinde Nikiomba Katika Shida Zangu, Niopoe Kila Niingiapo Hatarini, Ewee Bikira Mtukufu Mwenye Baraka-Amina.”
Mazungumzo haya yanaendelea huku ndugu huyu akasema kuwa kwa sasa Kanisa la Tanzania linatakiwa kufanya kazi ya ziada dhidi ya WAKRISTO wanaofanya kazi katika vyombo vya Ulinzi na Usalama nafasi yao katika kulinda uhai wa binadamu wenzao ikoje? Je Wakristo hawa katika vyombo vya Ulinzi na Usalama na mawakala wa uhai wa binadamu au mawakala wa kutokomeza uhai wa binadamu?
“Mfano mzuri katika hili ni wajibu wa Kanisa katika kupambana na wenye kushika silaha na kulinda uhai wa binadamu wengine ulikuwa ni kutengwa na Kanisa kwa Mfalme Victor Emmanuel wa II ambaye alikuwa mfalme wa Italia, Jeshi lake dhalimu lilifanya vituko vingi na mauwaji na hata baadaye kudiliki kuyavamia makazi ya Baba Mtakatifu Pius wa IX mwaka 1861 hata watu kadhaa katika makazi haya ya Baba Mtakatifu Walifariki na hapo hapo Kanisa lilimtengwa huku alipewa nafuu wakati akizikwa mwaka 1878.”
Ndugu huyu alisema kisa cha Victor Emmanuel wa II kikubwa si kuyavamia makazi ya kanisa hilo tu n akuvunja milango na matofari bali kitendo cha mauwaji ya Wakristo katika makazi haya nacho ni kile kile kulivamia kanisa maana kanisa siyo majengo, siyo milango siyo matofali tu bali ni waamini hawa hawa wanaoshambuliwa kwa risasi popote walipo.
Ndugu huyu akasema haya;
“Jamii imekata tamaa, kila mmoja hajui hatima yake maana wanaopaswa kumlinda binadamu wamebaba mzigo mkubwa na kutoaminiwa. Imani ya mtu imebaki kuwa hata kama nikifa basi huko niendapo nibaki kuwa salama maana huku dunia sijakuwa salama.”
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
Kwa sasa tumeshuhudia watu wakipotea na huku vyombo vya Ulinzi na Usalama na vyenyewe vinajibu kuwa hata vyenyewe havijui mtu huyo yupo wapi. Mfano mzuri ni Balozi wa zamani wa Kuba Humphrey Polepole Jamii inamtafuta, ndugu zake wanamtafuta, navyo vyombo vya dola hivyo hivyo.Tukiuliuza mpaka sasa uchunguzi wenu umefikia wapi itakuwa ni kosa? Tukisema hamjatimiza wajibu wenu itakosa?Je tukiomba Kanisa kuwawajibisha Wakristo wote waliomo katika vyombo hivi vya dola kwa kuwatenga kama alivyofanyiwa Mfalme Victor Emmanuel wa Pili itakuwa kosa?
Katika hali kama hii Mwanakwetu anaamni kuwa hata yule anayetekwa akishakuwa mikononi mwa watekaji anajua kuwa mwisho wake umefika, hawezi kupona na muda tu aliyopanga Mwenyeezi Mungu ndiyo utaamua atakuwa mikono mwa mwake au la.
Kwa hawa watekaji iwe chakula, iwe maji iwe maneno kutoka kwa kwao vyote hivi kifo tu mbele ya aliyetekwa, aliyetekwa anaweza kugoma kula akafa kwa njaa, anaweza kupewa chakula chenye sumu akafa, anaweza kupewa maji yenye sumu akafa, anaweza kuuwawa kwa risasi na anaweza kutupwa baharini au kwa wanyama wakali wakamla yote haya kimoja kinaweza kutokea lakini lakini lakini wewe unayefanya hivyo unadhani utakaa duniani milele? Kwa hiyo Sala Katika Hatari ya Kufa ni muhimu.
Mwanakwetu Upo?Je Makala haya yaitwaje? Sala Kabla ya Kufa au Kama Victor Emmanuel Wa Pili? Mwanakwetu anachagua Kama Victor Emmanuel Wa Pili
Nakutakia Siku Njema.
0717649257













Post a Comment