KAGENDA KUKAYA KWA MBUI

 

Adeladius Makwega.

Wapogolo ni miongoni mwa makabila mengi ya Tanzania yanayohofiwa sana uchawi (USHIRIKINA), Wakitenda mema kuogopa kufanya mbaya na matokeo yake lazima utalogwa.

Katika hilo la kuloga na kulogani kuna misemo mingi.

“Mchawi mpe mtoto alee, Mchawi hana sababu na Mchawi akimaliza kuloga kijiji, Kahamia nyumbani kwake.”

Hizi ni tungo chache kati ya nyingi katika lugha ya Kiswahili na kibantu ambazo Mwanakwetu anazikumbuka wakati akiandika makala haya.

Huku tungo kubwa anayoipenda ni hii ya mchawi keshamaliza kazi ya kikiloga kijiji sasa Mchawi yu kazini nyumbani kwake kuloga jamaa zake.

Hizi ni habari zetu siye WASWAHILI hasa Mwanakwetu MSWAHILI WA MBAGALA.

 

Tungo hii kwa Wapogolo huwa inatamkwa hivi;

“Mganga Kamaliza Kaya Kumloga, Kagenda Kukaya Kwa Mbui.”

Kwa Waswahili tungo ya tafsiri huwa hii;

“Mchawi Kamaliza Kuloga Kijiji/Mtaa, Sasa Kahamia Nyumbani Kwake.”

Tungo hii ya Wapogolo unaweza kuizungumza kwa lugha yoyote ile lakini wenye mali ni Wapogolo.

 

Sasa msomaji wangu ebu tuitazame Tungo hii KISARUFI na KIMAANTIKI.

Kwa kupiga jalanda la Sarufi tungo hii ya KISWAHILI na KIPOGOLO inaundwa hivi;

“Mchawi-Mganga, Kamaliza –Kamaliza, Kuloga-Kuloga, Kijiji/Mtaa-Kaya, Anakwenda-Kagenda, Nyumbani Kwake-Kukaya kwa Mbui.”

Kwa upande wa jalife la Kimaantiki tungo hii unaweza kuitazama hivi;

“Hapa pana pande mbili kwanza Mchawi kamaliza kuloga kijiji Chake, maana yake mchawi alikuwa anafanya ulozi wa wanakijiji wote, hivi ikiwa kazi kubwa kabisa na sasa keshawamaliza kwa ndugu hao kijijini.

Hapa Kwa Imani ya Kiafrika mchawi huwa anamloga mtu anakufa kisha anamla nyama.Kula ni jambo endelevu, kama wanakijiji wote wameliwa nyama na mlozi, sasa ni lazima mlozi ahamie nyumbani kwake. Hapa inaonekana mchawi huyu anakwenda kumaliza kazi ya kuwaloga jamaa yake.”

Maantiki ya sentensi hii ni kubwa sana maana kazi kubwa ilikuwa kuloga kijiji na kuwala ambayo imemalizika kazi ya kuloga jamaa ni nyepesi lakini ugumu wake huwa ni huruma ya mchawi tu lakini ule ukatili wa kuloga kijiji ndiyo utakao muongoza mchawi kuloga jamaa zake na kisha kuwala nyama.

 

Kazi ya kuloga jamaa nyepasi sana maana wapo katika himaya yako pia wako wachache, hauwezi kushinda kuikamilsiha maana ni wachache tu kama umeweza kuloga kijiji hushindwe jamaa? Umeloga kijiji umeloga jamaa mwisho wasiku ni hatima yake wewe maana lazima utaliwa nyama wewe.

Mwanakwetu upo? Kumbuka

“Mchawi Kamaliza Kuloga Kijiji Kahamia kwa Jamaa Zake.

Nakutakia Siku Njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257

Makala haya ni maalumu kwa walioumia na kufariki katika maandamano ya Oktoba 29, 2025.











 





0/Post a Comment/Comments