Adeladius Makwega
Oktoba 29, 2025 ilikuwa ni siku ya Kupiga Kura nchini Tanzania ambapo ni tukioa lililoambatana na madhara makubwa huku maandamano na vurugu zikitamalaki katika taifa hili la Afrika Mashariki.
Macho ya Watanzania walioandamana na maeneo jirani walishambuliwa kwa risasi na kusababisha majeruhi na vifo kadhaa ambapo idadi kamili ya vifo na majeruhi haijatajwa mpaka sasa.
Ndani ya Kanisa Katoliki ulimwenguni siku hii iliangukia katikati ya Dominika mbili, Dominika 30 na ile Dominika ya 31 ya mwaka Chee wa Kanisa.
Kwa hakika wapo Wakristo waliosali dominika ya 30 lakini hawakubahatika kuiona dominika ya 31 huku wakiwa wamefariki katika kadhia hii.
Jumapili ya 31 ilifika huku waamini waliokuwa salama walifika kanisani kusali kwa uchache mno huku taratibu za Ibada hii ya misa zikiendelea kama kawaida, mahubiri hayakuonesha kama kuna tukio limetokea lakini hali mioyoni mwa waamini ilikuwa na jambo.
Wakati wa sadaka ulifika huku waamini wakaionga kutoa sadaka zao, miongoni mwa walitoa sadaka katika Kanisa moja Katoliki la Mitume alikuwa Mkatoliki mmoja ambaye ofisi yake ndiyo iliyokuwa inasimamia uchaguzi huo pahala hapo.
Wakatoliki Kanisani wakawa wanakonyezana, huku wangine wakigunia mioyoni. Baadaye ulifika wasaa wa kukomunika Mkatoliki huyu alisimama na kwenda kukomunika huku miguno ya na kukonyeza kuendelea. Ndugu huyu alikomunika na kisha kurudi kuketi katika benchi ambalo halikuwa na mbali na benchi machache yasiyozidi matano ya kutoka la mwisho wa upande alioketi.
Waamini hao wakikumbuka mengi ya Oktoba 29, 2025, Baada ya Ibada hii mjadala ulikuwa mzuri sana, hawa jamaa wanatuletea shida sasa ameshafanya kitubio? Mwingine akajibu kuwa inawezekana amefanya kitubio maana tangu Jumatato hadi Jumapili ni mwendo wa siku tano, pengine Paroko ameshamuungamisha. Jamaa mwingine kando akasema unajua wizi wa kura na vifo vya vijana hawa dhambi zake haziwezi kufutika wakati wa Sala ya Nakuungamia Mungu mwenyezi nanyi ndugu zangu, Kwani nimekosa mno, kwa mawazo , kwa matendo na kwa kutokutimia wajibu…Nmekosa mimi, nimekosa mimi , nimekosa sana.
Msomaji wangu kumbuka watu wanatoka kanisa , dada mmoja akasema maneno haya;
“Unajua sote tuna dhambi, mimi binafsi yangu dhambi inayonitesa ni UZINZI, lakini napambana nayo, japokuwa katika dhambi hii nimepata watoto, sijaolewa nafanyaje na umri unaenda? Hili namuacha Mungu, yeye mwenyewe ataamua katika hili, lakini siyo dhambi ya kuiba kura na kuuwa watu huko mimi simo…”
Baadaye kila mmoja kuchukua njia yake.
Wakati Mwanakwetu anatafakari haya yote baadaye alikumbuka simulizi hii katika Biblia.
“Hadithi ya Mfalme
Daudi na Absalomu ni simulizi la kimaandiko linaloeleza mgogoro kati ya baba na mwana ambao uliishia kuwa uasi na vita ya wenyewe kwa wenyewe. Inaanza na hasira ya Absalomu baada ya dada yake Tamari kubakwa na ndugu yao wa kambo, Amnoni, ambaye baadaye Absalomu alimuua ili kulipiza kisasi. Tukio hili lilisababisha Absalomu kukimbilia uhamishoni na kuleta mpasuko mkubwa kati yake na Daudi. Baada ya muda, Absalomu alirudi, akapata umaarufu mkubwa, na hatimaye akamvua Daudi ufalme, jambo lililomlazimisha Daudi kukimbia Yerusalemu.Vita vya mwisho vilipiganwa kati ya majeshi yao, ambapo Absalomu aliuawa na jemadari wa Daudi, Yoabu, licha ya amri ya Daudi kwamba asiuawe. Daudi alihuzunika sana kwa kifo cha mwanawe, ingawa Absalomu alikuwa adui aliyekuwa amejaribu kumpokonya ufalme.Simulizi hii inaanza na ubakaji wa Tamari na ndugu yake wa kambo, Amnoni. Miaka miwili baadaye, Absalomu anamwua Amnoni ili kulipiza kisasi kwa dada yake. Baada ya mauaji hayo, Absalomu anakimbilia Geshu.
Baada ya muda, Daudi anamruhusu kurudi Yerusalemu, lakini hawapatani ipasavyo, na Absalomu anakaa miaka mingi bila kumwona baba yake akiwa amejawa na tamaa na kinyongo, Absalomu anapanga njama za kuasi dhidi ya Daudi hapa anapata uungwaji mkono wa watu wengi na kujitangaza kuwa mfalme huko Hebroni, jambo linalomlazimisha Daudi kuondoka Yerusalemu. Daudi anakusanya jeshi lake na kutoa amri kwamba wamfanyie Absalomu upole. Majeshi yanakutana vitani katika msitu wa Efraimu. Wakati wa mapambano, nywele ndefu za Absalomu zinanasa kwenye mti, na ananing’inia hewani.
Yoabu, jemadari wa Daudi, anamchoma kwa mikuki mitatu na kumuua, licha ya amri ya Daudi ya kumwachia hai. Ingawa Absalomu alikuwa adui yake na mpinzani wa kifalme, Daudi anaugua sana kwa kifo cha mwanawe. Analia kwa huzuni kuu akisema:‘Ee mwanangu Absalomu, mwanangu, mwanangu Absalomu! Laiti ningalikufa mimi badala yako, ee Absalomu, mwanangu, mwanangu!’
Kwa kifupi hiki ndicho kisa hiki.”
Mwanakwetu akiwa katika haya yote ya MFALME DAUD na baadaye kutambua kuwa hata VATICAN na wao walitoa neno juu ya hali hii iliyotokea nchini Tanzania tangu Oktoba 29 na siku zilizofuata mwaka wa 2025 huku Baba Mtakatifu LEO XIV kuyasema haya;
“Jamani tuliombee taifa la Tanzania, Vurugu baada ya uchaguzi Mkuu wa madiwani , wabunge na rais kumetokea maandamano, vurugu, mauwaji na vifo vingi. Ninawaomba nyote kuepuka aina yoyote ya makabiliano na njia ya kufuata ni MAZUNGUMZO tu. Mchana huu nitakita kambi katika makaburi ya VERANO nitaadhimisha misa ya EKARIST TAKATIFU kwa ajli ya watu wote waliofariki. Kimsingi nitatembelea hadi katika makaburi ya wapendwa wetu na kuombea wafu ambao hawana mtu yoyote anayewakumbuka.Baba yetu wa mbinguni anajua na anapenda kila mmoja wetu afahamu kuwa hajamsahau mtu.
Tukio la kutembelea makaburi haya ambapo hupambwa ukimya uliotamalaki unaovunja msongamano wa shughuli zote kwetu, huu ni mwaliko wa kukumbuka na kuwa tayari tayari. Hivyo basi nasisi tuyasahau yaliyopita tungoje yajayo, kuepuka kuwa wafungwa wa yaliyotokea awali. Mariamu mama wa sabato takatifu atufundishe kujiamini na kuwa watu wa matumaini.”
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
Kwa kifupi makala haya yanaeleza kwa kifupi kile kilichotokea huku muktadha wa makala haya ya Mwanakwetu ukitazama mazingira ya kanisa naye Baba Mtakatifu Leo XIV anasema anatuombea.
Mwanakwetu anakubali ni kweli Baba Mtakatifu anatuombea hili ni jambo zuri lakini kuna wakati yapo mambo yanayohitaji kutenda kwa mwanadamu na ndiyo maana Kadinali Francis Arinze aliwahi kusisitiza sala na matendo, Baba Mtakatifu mioyo yetu ina vidonda vingi katika hili, adua alinza kuteka, kubaka, kulawiti kuuwawa wachache na sasa anaua wengi.
Mwanakwetu upo? Kumbuka;
“Wakati wa Kutenda ”
Nakutakia Siku Njema.
0717649257













Post a Comment