

Adeladius Makwega-MBAGALA.
Mara baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 29, 2025wa Tanzania, taifa la Afrika ya Mashariki kutokana na kuibuka kwa maandamano, vurugu kukidaiwa watu kupigwa risasi, waandamanaji na watu walioo majumbani mwao kuumia na kuuwawa. Kwa sasa kumekuwa na matamshi ya watu kadhaa nchini Tanzania juu ya mahakama ya ICC, huku kumekuwa na kusontana vidole kuwa fulani anahusika kwa haya yote, fulani mbaya na fulani kayafanya haya. Wengine wakiwa kimya wakijifanya hawajui kilichotokea, lakini lakini lakini dhamiri zao wakiwa wenyewe na Mungu wanatambua kilichotokea.
Awali matumaini ya Watanzania yalikuwa kwa JWTZ lakini sasa matumaini haya yamehamia kwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wakiona pengine inaweza kuwa jawabu ya yote yaliyotokea na pengine inaweza kuzuia haya mambo yasijirudie tena.
Swali la kujiuliza je Mahakama ya ICC ni nini?
“Hii ni Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu yenye makao yake mjini The Hague, Uholanzi. Ilianzishwa mwaka 2002 chini ya Mkataba wa Roma wa mataifa mengi. Hii ni mahakama ya kwanza na pekee ya kudumu ya kimataifa yenye mamlaka ya kuwafungulia mashtaka watu binafsi kwa uhalifu wa kimataifa wa mauaji ya kimbari, uhalifu dhidi ya ubinadamu, uhalifu wa kivita, na uhalifu wa uchokozi. Mahakama hii ni tofauti na Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), chombo cha Umoja wa Mataifa kinachosikiliza migogoro kati ya mataifa. Mahakama hii ya ICC imekusudiwa kuwa nyongeza, si mbadala, wa mifumo ya kitaifa ya mahakama; inaweza kutumia mamlaka yake yakumfungulia mtu/kikundi kesi ikiwa pale ambapo mahakama za kitaifa hazina uwezo au haziko tayari kuwafungulia mashtaka kwa watuhumiwa wa uhalifu hao.
Nakuomba msomaji wangu yakumbuke sana maelezo haya;
“Mahakama hii ya ICC imekusudiwa kuwa nyongeza, si mbadala, wa mifumo ya kitaifa ya mahakama; inaweza kutumia mamlaka yake yakumfungulia mtu/kikundi kesi ikiwa pale ambapo mahakama za kitaifa hazina uwezo au haziko tayari kuwafungulia mashtaka kwa watuhumiwa wa uhalifu huo."
Matumaini haya yanaeleza picha ya wazi juu ya mahakama za ndani ya taifa hili,wapo wanaoamini kuwa haya mambo ni mazito , haya mambo yameizidi kimo Mahakama Kuu ya Tanzania chini ya Jaji Mkuu wa Tanzania George Mcheche Masaju, wapo wanaona kuwa Mahakama ya Tanzania kwa hili ni kibogoyo hawezi kuamua lolote, huku Jaji Masaju bado ameonesha utulivu kiasi.
“Jaji George Masaju amejaa mcheche(wasiwasi) kama jina la Baba yake, huko kwa tabia ataendelea kutafuta nyama zilisosangwa tu kutoka Tanganyika Parkers bila kujua kuwa nyama hizo nyingi zitakuwa haramu kwake ajiandae kuikosa pepo na akhere hapo kesho.”
Wadau wana mashaka na Mahakama ya Tanzania.
Kwa ujumla wake ICC inaweza kutumia mamlaka yake pale ambapo mtuhumiwa ni raia wa nchi mwanachama, uhalifu unaodaiwa umetokea katika eneo la nchi mwanachama, au hali fulani imepelekwa mbele ya Mahakama na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Katika hili siye wenye makao Makuu Dodoma ni wanachama huku takwimu zinadokeza kuwa hadi Oktoba 2024, kuna nchi wanachama 125 wa Mkataba wa Roma, ambazo zinawakilishwa katika chombo kinachosimamia mahakama hiyo, Bunge la Nchi Wanachama.
“Zipo nchi ambazo si wanachama wa Mkataba wa Roma na ambazo hazitambui mamlaka ya mahakama hiii ni pamoja na China, India, Urusi, na Marekani.”
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa mahakama hiiya ICC imeanzisha uchunguzi katika zaidi ya matukio kumi na mawili na imefanya uchunguzi wa awali kadhaa. Mahakama hii ilitoa hati zake za kwanza za kukamatwa watu kadhaa tangu mwaka 2005, na kutoa hukumu yake ya kwanza mwaka 2012. Watu waliotiwa hatiani wamejumuisha marais na maafisa wakuu wa serikali
“Kwa walio wengi wanadhani kuwa shauri dhidi ya Charles Taylor lilikuwa mezani ICC, hili siyo kweli bali ndugu Taylor alihukumiwa na mahakama maalumu ya Sierra Leone-Special Court for Sierra Leone (SCSL)”
Kwa kuyatazama makosa unaweza kuona yanalingana lakini mahakama tofauti.
Katika hili naomba nikukumushe msomaji wangu kuwa hali ilivyokokuwa siku ya hukumu wa Charles Taylor ;
“Ndugu Taylor tafadhali unaweza kusimama kwa ajili ya kusomewa hukumu ya Mahakama....
‘Bw Taylor kwa hayo yaliyotangulia hapa mahakamani sababu ya kesi yako, kwa kauli moja unakuhukumu kwa muda mmoja wa kifungo cha miaka 50 kwa makosa yote ambayo umepatikana na hatia, nafuu itatolewa kwako kwa muda unaoanzia Machi 29,2006, ambapo ulizuiliwa ukisubiri kesi hii, asante unaweza kuketi .’
Bwana Taylor hukumu iliyotolewa leo haichukui nafasi ya viungo vilivyokatwa, haiwarudishi maisha wale waliouawa, haiponia majeraha ya wahasiriwa wa unyanyasaji wa kijinsia na haiondoi makovu ya kudumu ya kihisia na kisaikolojia na kimwili ya watumwa wanaajiriwa kama askari watoto lakini hukumu kwa uhalifu huu inaleta kiasi fulani cha haki kwa makosa haya mabaya. Jumuiya ya Kimataifa imeridhika kwamba Charles Taylor atakufa gerezani swali ni je kiasi gani wanataka zaidi au ni kiasi gani wanahitaji ili kutuliza kiu hii ya Kimataifa ya damu.
Kama una hoja unafuata utaratibu kama awali...”
Katika miaka ya hivi karibuni, kesi mashuhuri zimejumuisha hati za kukamatwa zilizotolewa kwa Rais wa Urusi Vladimir Putin kuhusiana na uvamizi wa Ukraine, na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Waziri wa Ulinzi Yoav Gallant, pamoja na viongozi kadhaa wa Hamas kuhusiana na vita vya Gaza.
Tangu kuanzishwa kwake, ICC imekabiliwa na ukosoaji mkubwa. Wapinzani wake, wakiwemo mataifa makubwa ambayo hayajiungi na mahakama hiyo, wamehoji uhalali wake, wakitoa wasiwasi kuhusu uhuru wa kitaifa na kudai uwezekano wa kuathiriwa kisiasa. Mahakama pia imekosolewa kwa upendeleo na kwa kulenga zaidi viongozi wa Kiafrika. Wengine wamehoji ufanisi wa mahakama hiyo, wakieleza utegemezi wake kwa ushirikiano wa mataifa katika kukamatwa kwa watuhumiwa, idadi ndogo ya hukumu zilizotolewa, na gharama kubwa za mchakato wake wa kesi.
“Uanzishwaji wa mahakama ya kimataifa ya kushughulikia viongozi wa kisiasa wanaoshutumiwa kwa uhalifu wa kimataifa ulipendekezwa kwa mara ya kwanza katika Mkutano wa Amani wa Paris mwaka 1919, baada ya Vita vya Kwanza vya Dunia, na Tume ya Uwajibikaji.
Hoja hiyo ilijadiliwa tena katika mkutano uliofanyika Geneva chini ya usimamizi wa Jumuiya ya Mataifa mwaka 1937, ambapo ulisababisha kuhitimishwa kwa mkataba wa kwanza uliotaka kuanzishwa kwa mahakama ya kudumu ya kimataifa ya kushughulikia vitendo vya ugaidi wa kimataifa.”
ICC ilianza rasmi shughuli zake Julai 1, 2002, baada ya kuanza kutumika kwa Mkataba wa Roma — mkataba wa kimataifa wa mataifa mengi unaohudumu kama katiba na nyaraka kuu ya uendeshaji wa mahakama hiyo. Mataifa yanayoridhia na kuwa wanachama wa Mkataba wa Roma yanakuwa wanachama wa ICC na hushiriki katika Bunge la Nchi Wanachama linalosimamia shughuli za mahakama. Kufikia Januari 2025, kuna nchi wanachama 125 wa ICC, huku mataifa 29 yakiwa yametia saini lakini hayajaridhia Mkataba wa Roma (yakiwemo manne yaliyofuta saini zao), na mataifa 41 hayajatia saini wala kuwa wanachama wa mkataba huo. Mahakama hii imekusudiwa kuwa mahakama ya mwisho ya kutolea haki, ikimaanisha kuwa ICC inakamilisha kazi za mifumo ya kitaifa ya mahakama na inaweza kutumia mamlaka yake tu pale ambapo mahakama za kitaifa hazina uwezo au haziko tayari kuwafungulia mashtaka wahalifu. ICC haina mamlaka ya kimataifa ya kijiografia (universal territorial jurisdiction); hivyo, inaweza kuchunguza na kushitaki uhalifu uliotokea ndani ya nchi wanachama, uhalifu uliotendwa na raia wa nchi wanachama, au uhalifu katika hali zilizorejelewa kwake na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
ICC ilifanya kikao chake cha kwanza mwaka 2006, kuhusu mashitaka ya uhalifu wa kivita dhidi ya Thomas Lubanga Dyilo, kiongozi wa waasi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo aliyeshutumiwa kwa kuandikisha watoto askari. Hukumu yake ya hatia mwaka 2012 ilikuwa ndiyo ya kwanza katika historia ya mahakama hiyo. Ofisi ya Mwendesha Mashtaka imefungua uchunguzi rasmi katika kesi kumi na mbili na inaendelea kufanya uchunguzi wa awali katika kesi tisa nyingine.
Mwendesha Mashtaka anaweza kufungua uchunguzi chini ya hali tatu: hali inapotumwa na chama cha serikali; hali inapotumwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, likifanya kazi kushughulikia tishio kwa amani na usalama wa kimataifa; au wakati Chumba cha Utangulizi kinamruhusu mwendesha mashtaka kufungua uchunguzi kwa msingi wa taarifa zilizopokelewa kutoka kwa vyanzo vingine, kama vile watu binafsi au mashirika yasiyo ya kiserikali.
Mtu yeyote anayechunguzwa au kufunguliwa mashitaka anaweza kuomba kuondolewa kwa mwendesha mashtaka katika kesi yoyote , ibara ya 42 Maombi ya kuondolewa kwa waendesha mashtaka yataamuliwa na Chumba cha Rufaa. Kwako ndugu yangu Jaji Mkuu GeorgeMCHECHE Masaju naomba nikwambie hili,Unaposikia raia wanaposema jambo juu ya mahakama ya mbali ya makosa ya halaiki ambayo inashughulikia makosa ya wakubwa wakubwa wakubwa tambua kengele ya ishalia, mwalimu yu darasani na somo linakaribia kumalizika na wewe mwanafunzi umechelewa kipindi hicho.
Kwa hili la Tanzania ndugu yangu Jaji Masaju hii kama ni nyama haijapiia Tanganyika Parkers... ndugu yangu tambua kuwa hapa sukurubu ya injini ya gari ushapotea, -siyo imelegea sukurubu ishachomoka na kupotea kabisa na kinu cha kuichonga sukurubu hiyo hakipo....hakipo, hakipooo na hakipooooo Mahakama Kuu bali ICC... maskini wa Mungu.
Mahakama Kuu ya Tanzania kuweni makini.Hapa Jaji Masaju ndugu yangu hizi nyama kutoka pale Tanganyika Parkers kuwa nazo makini. Maelezo ya katika kopo la nyama hayatoshi, nenda mbali zaidi ili kuipa Mahakama ya Tanzania heshima.
Hapa hapa Jaji Masaju mwenzako naukumbuka ule mchezo wa utotoni pale kwetu Mbagala, pale Mbagala Mbuyuni Mchezo wa NYAMAAAAAA-Nyamaaa... ya ng’ombe- NYAMAAAA, ya Mbuzi -Nyamaaa ya Kenge Siyo Nyamaaa hiyoooo. Ya NGURUWE Hapa jaji Mkuu majibu majibu yanakuwa mara mbili wapo wanaosema nyama na wapo wanaosem hiyo siyo nyamaaaa.....Katika hili hata mdogo wangu Wasabato wa kwele Mafulu Mjalifu, Joseph Burra, Christopher Ungani watasema hiyo siyo nyama.
Hii ni Kengele ya Hatari kwa Mahakama ya Tanzania, Watanzania wanafikirilia ICC, Je vitendo vya viongozi vikoje? Vinatiliwa mashaka . Hata hawa majaji kutoka Mahakama Kuu wakipewa kazi nje ya Mahakama ya Tanzania kazi zao wanazifanyaje? Je wanacheza kwa umahiri na kwa umakini kama walinzi wa haki?
Jaji Mkuu Ongea na majaji wenzako maana inaposemwa juu ya ICC lazima mahakama itambue kuwa Majaji wetu miongozi ya taifa letu ni vigumu kushitakiwa, lakini je kwa ICC wataweza kubaki salama?Jaji Mkuu zungumza na Majaji wenzako zungumza na wanasiasa. Huku MAJAJI wote wakiwa nje ya Mahakama wakipewa kazi wasikubali kubatizwa na kuwa WANASIASA au kuwa Wasaidizi wa WANASIASA.
Mkumbuke mahakama ya Uhalifu wa Dujail kule Iraki baada ya vita vya Ghuba vya pili Jaji Mkuu alishitakiwa na balaa walilopata wanasiasa na yeye lilimkuta.Wakubwa kwa wadogo walinde uhai wa binadamu na siyo vinginevyo.
Mwanakwetu upo?
Kumbuka;
"Alama Hatari Kwa Mahakama ya Tanzania."
Nakutakia Siku Njema.
makwadeladius@gmail.com
0717649357

























Post a Comment