
Adeladius Makwega-MBAGALA.
“Habari za leo Mkuu!
Vipi umesafiri? Sijakuona leo…?
Duu kaka asante sana, leo nilidhani Jumamosi kumbe…
Kukiwa na chochote kipya nijulishee…”
Huo ni mjadala wa wazee wa wawili wa Kitanzania wanaongea kupitia ujumbe mfupi wa simu za mkononi ,asubuhi moja. Wazee hawa wanawajibika pamoja katika mraba mmoja, mmoja kapitiwa na Ijumaa kadhani Jumamosi, mzee mwenzake anauliza vipi mbona sikuooni?
Mzee huyu kagafilika, yote hiyo ni uzee tu. Wewe kama kijana ngoja uzee uje utayajua haya yanayosimuliwa, unaweza ukajidaia mjanja na nguvu za leo baba zitakwisha ole wako umfanyia mtu mabaya ,kumbuke tenda mema maishani mwako nguvu zitakwisha, yupo mmoja tu ambaye nguvu zake hazichakai naye ni MUNGU Wa MBINGUNI.
Baada ya mjadala huo mzee aliyegafilika Ijumaa kuwa Jumamosi yu kitandani kwake, akafungua ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, akakutana na ujumbe huu;
“Hatupaswi kumuogopa adui maana huyo adui anakuja kwetu kutufuata ili nasi tuoneshe zile TALANTA tulizopewa na Mwenyeenzi Mungu tusizifutike, zionekane na ndiyo maana anapokuja adui watu wengi wa karibu wanatuacha.”
Haya yakiwa maelezo ya Dkt. Vernon Fernandes, Askofu na Mwenyekiti wa Taifa wa Makanisa ya Kipentekost Tanzania (CPCT).
Huyu mzee aliyegafilika akiwa kwake akayakumbuka maneno ya Askofu Fernandes ya hivi karibuni mbele ya taifa la Tanzania katika kipindi kigumu linalopitia tangu Oktoba 29, 2025.
“Kama mwenyekiti wa CPCT Taifa naomba niseme kidogo…Taifa limegawanyika na mioyo ya yawatu imejeruhiwa.. Mungu Baba ulilete taifa kuponya mioyo hii. Mungu Baba sisi Watanzanaa tupo hapa… hakuna mwanadamu mwenye haki… tunaomba uuasamehee makosa yetu tuliyoyafanya katika nchi hii…”
Huyu mzee aliyegafilika nyumbani kwake akakumbuka kisa hiki cha kweli kabisa cha Mchungaji Vernon Fernandes akiwa kijana kabisa mwaka 1993ambapo alifika Katik Kanisa la WALOKOLE MBAGALA KIZUIANI kukafanya mkutano wa Injili nje ya uwanja wa kanisa hili kwa siku kadhaa, wakati huo MBAGALA ni kijijini sana.
Kwa mujibu wa msimuliaji anasema kuwa Mkutano huo ulikwa na waamini wengi wa Kilokole na kutoka madhehebu menginem mchungaji Fernandes alihubiri kisha ukaja wakati wa kuwaombea wale wenye shida zao. Wakatoka mbele nawalikaa katika mistari mirefu wa kwanza wa pili wa tatu huku mistari inaendelea. Vijana wadogo wawili wa sekondari walikuwa kando wanabishana, mabishano yalikuwa juu ya ukweli wa miujiza na mahubiri yao. Wakabishani weee huku Mchungaji Fernandes yeye anaendelea kuwaombea wale waliojipanga foleni. Mabishano ya hawa vijana wadogo yalikuwa makubwa mno.
Kijana mmoja akasema maneno haya;
“Mimi nakwenda katika foleni kisha akija huyu mchungaji kuniombea nitamwambia kuwa mimi navuta bangi na nakula madawa ya kulevya nataka nipime kama atajua hili? Kupima kama huyu mtumishi ni kweli anao upako wa Mungu au laaa?”
Kijana yule akaingia katika foleni vizuri nayeye Mchungaji Fernandes na wenzake wakafika kwa kijana huyu, wakamuombea mapepo ya hayakulipuka, Mchungaji akauliza kijana una shida nini? Kijana akajibu kama alivyowaambia rafiki zake anatumia madawa ua kulevya. Mchungaji Fernandes akasikitika mno, kijana akaombewa sana hakukuwa na mepepo yaliyomtoka, alipomaliza sala hiyo kijana akarudi kwa wenzake na kusema maneno hawa hawa hawa wachungaji waongo sana mbona hakuna kilichotokea?.
Kwa mujibu wa msimuliaji ilikuwa ni siku ya mwisho ya mahubiri hayo yaani Jumapili Jioni na mwanafunzi mmoja alikuwa anasoma Shule ya Mtakatifu Antony wa Padua anaitwa Matias Bernad sasa yeye ni mfamasia na wenzake kadhaa wakisoma shule kadhaa za Dar es Salaam. Jumatatu wakaenda shuleni, Jumatatu ikapita salama, Jumanne salama ,Jumatano salama lakini alhamisi jioni ndugu yule ambaye jina linafichwa alipokea barua ya Oktoba 20, 1993 akifukuzwa kabisa shule kwa kosa ambalo alituhumiwa kufanya zamani, miezi karibu minne nyuma, huku walishaadhibiwa darasa zima, kosa hakufanya na kwake ikawa Adhabu Mara Mbili.
Kwa hakika Martias Bernad aliyetajwa ambaye alikuwa anabishana na ndugu huyu yupo hai na vijana wote karibu watano wapo hai lakini sasa ni wazee wana mvi.
Kumbuka huyu anayeasimulia alikuwa nyumbani kwake, baadaye akamsimulia Mwanakwetu kisa hiki nayeye Mwanakwetu kukiweka katika makala haya unayoyasoma leo hii kama kilivyo.
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
Jamani eeee ! Hawa viongozi wa dini wakisema jambo msiwadhihaki hata kidogo, wasikilizwe kwa heshima zote hata kama siyo wa Imani yako, msiwadhiaki, msitumie kigezo cha kujua madhaifu yao iwe kwa kutazama mawasilianoayao au lolote lile,hawa ni binadamu kama mlivyo viongozi wa siasa maana hata viongozi wa siasa mnavyo madhaifu mengi. Hakuna aliye mkamilifu katika hii dunia sote, sote na sote tuko katika jitihada tu za kutaka kuufikia mji uleeeee...
Mwanakwetu ameipata hii simulizi kwa bahati tu ameiandika kwa heshima na kwa heshima ya CPCT hususani Askofu Vernon Fernandes mwenyewe na familia yake kwa msimamo wake kwa hali ya Tanzania tangu Oktoba 29, 2025.
“Kwako baba Askofu Fernandes Kwanza SHIKAMOO. Tambua kuwa tunakukubali mno. Siku yoyote Mungu akitujalie uhai nitakuletea huyu jamaa aje kukusalimu Baba Askofu. Akikiona unavyongea na hasa juu haki anakumbuka haya yote yanayosimuliwa sasa, mwenyewe anakuita GOA MLOKOLE maana mara nyingi MAGOA wengi ni WAKATOLIKI.”
Shauri ni Lenu Wanasiasa wa Tanzania.
Mwanakwetu upo?
Je makala haya yaitwaje ? Shauri Lenu Wanasiasa wa Watanzania? Mzee Aliyegafilika? Adhabu Mara Mbili ? au GOA Mlokole? Mwanakwetu vichwa vyote vinne kavipenda lakini wewe msomaji wanguchagua kimoja huku ukikumbuka ile, ile , ile na ile ya Adhabu Mara Mbili.
Nakutakia Siku Njema.
0717649257















Post a Comment