TUDUMU KATIKA SALA

 



Adeladius Makwega-MUSOMA TANZANIA

Siku ya Oktoba 19, 2025 ilikucha tulivu, upepo ukivuma kwa KM 10 kwa saa, unyevunyevu wa 20% huku ujirani na mvua ni wa 70% na  hali ya joto ni nyuzi joto 24% nalo anga la mji huu likiwa na mawingu majira ya asubuhi likisadifu 70% ya ujirani na mvua.

Siku hii ilikuwa ya dominika ya 29 ya mwaka C wa Kanisa, Mwanakwetu yu mkoani Mar nchni Tanzania, kigulu na njia hadi Kanisa la Mtakatifu Agustine-Parokia ya Mwisenge Jimbo Katoliki la Musoma nchini Tanzania, ibada ya misa ya kwanza ya saa 12. 30 asubuhi inaanza, misa hii ikiongozwa na Padri Julius Ogolla ambaye pia ni Paroko husika anaiogoza misa yote ;

“Ndugu zangu Wakristo wapendwa masomo ya dominika hii yana mambo makubwa matatu; kwanza HAKI, pili UMISIONARI na tatu SALA. 

Iwe haki na iwe umisionari ili uweze kufanyika vizuri unahitaji mno SALA.”

Padri Ogolla alielezea kwa kina namna bora ya kuufanya umisionari tangu kwa viongozi wa dini wawe makasisi, watawa na Maaskofu na bila kuwasahau WALEI kila mmoja akisema ni mmisionari wa KRISTO katika ulimwengu huu. 

Padri Ogolla alitolea mfano wa Maisha ya SOCRATE mwanafalsafa mahiri wa Ugiriki ya kale kuwa wakati alifungwa kwa sababu ya haki, alipokuwa gerezani askari JELA alimwambia maneno haya;

“SOCRATE unateseka na nini hapa, mimi nitakufungulia GEREZA uondoke zako.”

SOCRATE alisema sawa kwa mawazo haya lakini alimwambia jambo moja tu huyu askari jela;

“Mimi nimezaliwa katika taifa hili hili la wanasiasa hawa hawa madhalimu, wanasiasa hawa hawa dhalimu ndiyo waliyonifunga, hapa hapa katika ardhi ya wanasiasa dhalimu ndipo kilipozikwa kitovu changu, ntabakia hapa hapa hadi pumzi yangu ya mwisho.”

Haya ni Parokia ya Mwisenge hapa Tanzania, je yepi ni Vatikani? 

Hapa kando ni mahubiri ya Kadinali Luis Antonie Tagle Mkuu wa Propaganda Fide ya Kanisa Katoliki inayojihusisha na Uinjilishaji wa watu Ulimwenguni.

“Yesu katika Injili ya leo anatuhakikishia kwamba Mungu husikiliza maombi yetu. Yesu anawaambia wanafunzi wake juu ya kadhi mmoja ambaye hakuwa na hofu ya Mungu wala hakuwa na heshima kwa binadamu yeyote na kadhi huyo alikuwa akiombwa na mjane atoe hukumu ya haki kwa ajili yake dhidi ya adui yake.

Kadhi huyo dhalimu hakutaka kufanya hivyo, akaahirisha jambo hilo kwa muda mrefu, hadi siku moja akaamua kutoa hukumu ya haki kwa ajili ya mjane huyo kwa sababu alikuwa amechoshwa na kusumbuliwa naye.

Yesu anamwelezea kadhi huyo kuwa mtu dhalimu. Lakini tofauti na kadhi huyo mwovu, Mungu hachoki na wale wanaomlilia mchana na usiku.

Yeye hachelewi kuwajibu na atahakikisha kwamba haki inatendeka kwao upesi kabisa. Ikiwa kadhi mwovu anaweza kutenda haki kwa nia isiyo sahihi, basi Mungu mwema na wa haki hujibu kwa upendo ili haki itendeke na itolewe. Lakini je, tutakuwa watu watakaodumu katika sala na imani kwa Mungu na katika haki yake?”

Msomaji wangu hayo yote ni dominika hii sehemu ya Parokia ya Mwisenge na sehemu ni ya Vatikani.

Msomaji wangu siku ya leo natamani nikuume sikio ya jambo hili;

“Mwanakwetu alipokuwa kanisa la Mtakatifu Augusine Parokia ya Mwisenge Hapoa Musoma Oktoba 19, 2025 wakati wa sadaka ziliimbwa nyimbo tatu za matoleo na wakati wa kukomunika ziliimbwa nyimbo mbili tu.

Mara nyingi Kanisani kama kuna idadi kubwa ya waaminii wanaotoa sadaka au kukomunika inasababisha kuimbwa nyimbo nyingi wakati wa haya matukio .I

Ile misafala inakuwa mirefu sana kwa hiyo kwaya inaweza kuimba nyimbo nyingi na idadi ndogo katika misafara hii wimbo unaweza ukaimbwa kipande kidogo tu.

Mwanakwetu pia amebaini kuwa mara nyingi idadi ya waamini wanatoa sadaka huwani robo ya tatu ya waamini wote waliofika Kanisa kusali. Kwa hiyo ukihesabu waamini walitoa sadaka ukagawanya kwa tatu, ile robo yao ukajumlisha na walitoa sadaka unaweza kupata idadi ya waamini wote waliosala ibada hiyo.”

Haya ni mahesabu ya Mwanakwetu.


 

Kisa ambacho Mwanakwetu anakumbuka ikatika hili ilikuwa ni cha mwaka 2014 Katika Kanisa la Mtakatifu Peter Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam ilikuwa Ibada ya Mkesha wa Noeli. Mwanakwetu alikuwa miongoni mwawatumishi wa kikosi cha TBC kilichokuwa kinarusha hewani matangazo ya moja kwa moja ya mkesha huo wa NOELI Misa iliyoongonzwa na Maaskofu Wasaidizi wawili wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, huku Padri wa St Peter wakati huo alikuwa Padri Stephern Kaombwe.ambae ni Padri mzee lakini kwa kumtazama waweza kudhani ni Padii kijana.

Shangazi yangu mmoja alinidokeza kuwa  Padri Stephern Kaombwe utadhani ni kijana mdogo nimetoka kuchukua cheti cha ubatizo wakati huo akiwa  Saint Joseph lakini ni mzee na alisoma na Francis Fidelis Makwega (Baba wa Mwanakwetu) 

;

"Kikosi cha TBC Taifa waliyokuwepo walikuwa wafuatao Watangazaji; Jene Lutaserwa na Adeladius Makwega, Mainjia ni Josephy Masanja na Steven Basheka huku madereva walikuwa wawili Ali Makawila na huyu dereva wa pili jina limesaulika, pia akiwepo mtangazaji ambaye alikuwa anajifunza kutangaza matangazo ya moja kwa moja akiwa ndiyo amepata kazi naye Hamis David Holela.

Parokia hii iliwapokea vizuri sana nakumbuka Mwanakwetu alikuwa na chupa ya Chakula cha kula usiku huo na soda ambavyo alitoka nacho nyumbani kwao Mbagala. Vifaa vya mtangazo ya moja kwa moja vlifungwa vizuri hadi saa mbili usiku kazi ilikuwa imekamilika. Mwanakwetu akatoka ili ale chakula chake katika FOOD FLASK na soda yake.

Padri Kaombe akamkuta Mwanakwetu amekaa katika ngazi za kanisa hili ndiyo anafungua chupa yake ale. Padri Kaombe akasema wewe si mtangazaji tumeandaa chakula na vinywaji kwa ajili yenu, twendeni katika nyumba ya Paroko.

Mwanakwetu na wenzake wakaelekea kula chakula cha Parokia hii, alipomaliza kula alichukua chakula chake ndani chupa yake na soda na kuwapa vijana walizogaa kando ya Parokia hii kabla ya misa hii kuanza saa tatu kamili ya usiku, huku ibadani nyimbo sita za sadaka ziliimbwa.”

Msomaji wangu siku nikifurahi nitasimulia vituko vya Watangazaji , Mainjini wa sauti na madereva wa  TBC tulipokuwa katika meza ya chakula ya Baba Paroko wa Osterbay Disemba 24, 2014  kabla ya Ibada ya Misa kuanza lakini kumbuka sana Padri Kaombe ni Padri mkalimu sana, leo baada ya miaka 11 tukio lile la mwaka 2014 nimelikumbuka. Wewe Mkristo mwezangu Parokia yako ni ya WAKALIMU? 

Mwanakwetu upo? 


 

Kumbuka

“Tudumu Katika Sala.”

Nakutakia Siku Njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257

 













 

0/Post a Comment/Comments