Adeladius Makwega-SERENGETI MARA
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Alfred Mtambi, Septemba 30, 2025 amekabidhi mabasi madogo matatu kwa shule tatu za Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti mkoani hapa yenye thamani ya karibu shilingi milioni 370 huku akisisistiza vyombo hivi vya moto vitumike vizuri .
Akizungumza katika hadhara hiyo iliyowakutanisha wadau mbalimbali wa maendeleo Wilayani Serengeti Mhe. Kanali Mtambi alitumia wasaa huu pia kumpongeza mfadhili aliyafanikisha ununuzi wa mabasi haya kwa kuwa na moyo huu.
“Nawaombeni wananchi wa Wilaya ya Serengeti muwe na moyo kama wa huyu ndugu yenu, vinginevyo nitamuhamishia Arusha.”
Wakati Mkuu wa Mkoa wa Mara akisema maneno haya wananchi wa Serengeti wakisema hapana, hapana hapana kwa sauti ya juu kabisa. Sambamba na Taasisi ya Nyasaho kutoka mabasi haya matatu pia alijitokeza hadharani mdau mwinegine kutoa mafuta ya dizeli yenye thamana ya shilingi milioni 10 ambayo yatatumikaa kama kianzio cha mabasi hayo na mara moja kuanza kutoa hudumu kwa shule hizo tatu ambazo ni NGOREMO, MACHOCHWE na NATTA.
Jambo la pili lililomvutia Mwanakwetu ni namna wanaunzi wa NATTA Sekondari walivyochuku basi lao na kushangilia huku wakilifuata nyuma hadi likafika shuleni kwao kwa shangwe kubwa.
Huku wakiimba wimbo huu;
“Shule Yetu, Kwa Sasa , Ina Basi.”
Mwanakwetu siku ya leo anasema nini?
Mwanakwetu mara baada ya hafla hii alikumbuka mambo mengi juu ya miradi hii ya mabasi/magari ya shule.
“Mwaka 1990 Umoja wa Vijana Mkoa wa Dar es Salaam na Umoja wa Vijana CCM Tanzania ulianzisha Mradi wa mabasi ya wanafunzi Jijini Dar es Salaam ambapo yanunuliwa mabasi kadhaa aina ya TATA, chini viongozi wa UVCCM wakati huo William Lukuvu na marehemeu John Gudinita ambapo mabasi haya yanunuliw akutokana na michango kadhaa kutoka kwa wazazi/ walezi na wadau jijini humo wakati huo.”
Mradi huu kwanza ulifanya kazi kwaakubeba wanafunzi majira ya asubuhi, mchana na jioni kisha muda mwingine kubeba abiria lakini baadaye ulishindwa kujiendesha kibiashara huu ni mradi wa huduma ma mabasi ya wanafunzi ukafa.
Kwa sasa kwa taifa la Tanzania Shule binafsi zinawabeba wanafuzni wake katika mabasi ya wanafunzi kwa utaratibu wa wazazi wenyewe kwa kila mzazi kuchangia kati ya shilingi 25,000-40,000 na kulingana na umbali anaotokea mwanafunzi ambapo pesa hiyo inakuwa kando kabisa na karo ya mwanafunzi.
Hali hii ndivyo ilivyo kwa shule za umma kama vile Arusha School, Bunge Primary School, Olimpio Primary School na hata International School of Tanganyika(IST). Kwa mabasi haya ya umma Mwanakwetu anaona kuwa Halmashauri ya Serengeti inapaswa kuwa makini ya namna ya kuyatunza tangu kupatikana kwa madereva ambaye ataendesha mabasi haya kila siku, kufanyiwa service kwa wakati ili kuweza kutoa huduma hii muda mrefu kwa wanafunzi wetu.
Kumbuka;
“Kwa Sasa Shule Yetu Ina Basi.”
Nakutakia Siku Njema.
0717649257


Post a Comment