MWANASOKA WA TANZANIA ALIYEBATIZWA KABILA

 



Adeladius Makwega- MBAGALA

Oktoba 11, 2025 katika mtandao wa kijamii kulipachikwa picha ya mzee mmoja na bintiye, huku binti huyu akisema HBD Baba. Ujumbe huu ulipoutazama vizuri Mwanakwetu alimtambua binti huyu na pia alimtambua mzee kando yake ambaye anafahamika kama King Abdallah Kibadeni Mputa huku jina lake halisi ni Abdallah Othuman Seifu , mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars na timu ya Simba ya Dar es Salaam. Wadau wa mtandao huo walikuwa na maneno ya uchokozi mengi, wengine hasa wale wa Timu ya Yanga wakisema maneno kadhaa ya vijembe,

“Baba Mkwe katimiza miaka mingapi?”

Majina ya haya ya Mchezaji huyu kubadilika hadi kuwa King Abdallah Kipadeni Mputa yana historia ndefu ndani ya makuzi yake pale Ilala jijini Dar es Salaam baada ya kuzaliwa Mbagala  mwaka 1949 na hadi kucheza soka Simba na kuhamia Majimaji ya Songea chni ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma wakati huo Laurence Gamba.

“Mzee Gama kasema nyini kuanzia leo ni machifu wa Kingoni hivyo akaweka majina ya machifu ya Kingoni katika kitunga kisha sote kuchangua mia na wezangu ndipo mimi na kuchagua jina la MPUTA ambaye ndiye Chifu Mkubwa wa Kingoni tangu enzi hadi sasa nina bangili ya KICHIFU na sasa mimi ni MNGONI.”

Haya ni maelezo ya King Kibadeni mwenyewe, mzaliwa wa Mbagala alipokuwa akiongea na nduguye Mwanakwetu mapema Oktoba 11, 2025. Huku Kibadeni mwenyewe anasema watoto wa madrasa pale ilala ndiyo walimpa jina la KIBADENI maana hata maana yake haifahamu walikuwa wakiimba wimbo huu;

“Shule nimesoma Habibu Punja Muslim School, watoto wezangu shuleni walikuwa wananiimba ashakumu si matusi...

Abdallah Kibadeni, Kanya Mavi Mtendeni, Kasingizia Wageni.  Sifahamau maana ya neon hili KIBADENI lakini ndivyo nilivyoilipa jina hilo.”

Msomaji wangu kumbuka jamaa wengine mtandaoni wakisema  maneno mengi tambo nyingi ati Yanga wameshaanza balaa lao, maali kwa King Abdallah Kibadeni lini kapokea hadi wanamuita Baba Mkwe?

“Atake asitake, yeye ni Baba Mkwe tu, iwe hiari iwe lazima Kibadeni Baba Mkwe wetu, Mbona yeye alioa kwa Rashid Kawawa mbona hatusemi neno?”

Simba nao hawakuwa mbali, wengine wakiuliza maswali inbox na majibu kupatiwa huko huko;

“Latifa Kibadeni Msalimie King Kibadeni, Kiboko ya Yanga miaka nenda miaka rudi , waambie Yanga kama wanaweza wavunje rekodi yake!”

Mwanakwetu hakujua kama Latifa Kibadeni  ni Yanga au Simba lakini historia baba yake  ambaye mwanamichezo  kutoka Afrika ya Mashariki inadokeza mengi ikiwamo haya;

“Abdallah Kibadeni, anayejulikana kama Mfalme Kibadeni Mputa, ni mchezaji wa zamani wa soka na kocha kutoka Tanzania aliyejulikana sana kwa kipindi chake akiwa na Simba SC. Msimbazi Dar es Salaam, anatambuliwa kwa rekodi yake ya kihistoria ya kufunga mabao matatu (hat-trick) katika mechi ya watani wa jadi mwaka 1977 dhidi ya Yanga — rekodi ambayo haijavunjwa hadi leo. Kibadeni pia aliichezea timu ya taifa Tanzania na baadaye kuwa kocha wa Simba pamoja na timu ya taifa, Taifa Stars, na anasifika kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya soka la Tanzania.

Kibadeni alianza kucheza soka akiwa Yanga, ingawa hakupata nafasi ya kuonyesha uwezo wake licha ya kufanya mazoezi na timu hiyo. Baadaye alijiunga na Simba SC, ambako aling’ara kama mshambuliaji hatari aliyejulikana kwa umbo dogo na kasi kubwa.

Mafanikio yake makubwa zaidi yalikuwa yanabaki kileleni ni kufunga mabao matatu katika ushindi wa 6–0 dhidi ya Yanga mwaka 1977. Ushinde unawakera mno Yanga hadi kesho.

Baada ya kustaafu kucheza, Kibadeni aliugeukia ukocha na kufundisha Simba SC.

Pia alihudumu kama kocha wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars. anakumbukwa kama mmoja wa wanasoka mashuhuri zaidi nchini Tanzania, huku rekodi yake ya hat-trick ikibaki kuwa alama ya hadhi yake ya kifahari.

Anaendelea kuwa sura maarufu NAMBA MOJA katika tasnia ya soka la Tanzania, mara nyingi akishiriki kwenye mahojiano na mijadala kuhusu mchezo huo.”

Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?



 

Kwa kuwa makala haya yamemtaja pia Latifa Kibadeni ni vizuri kidogo Mwanakwetu akaeleza Latifa Kibadeni ni nani?

“Latifa Kibadeni ni binti wa Abdallah Kibadeni, Latifa ni mtumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya pia ni miongoni mwa wanafunzi wa Mwanakwetu aliowahi kuwafundisha somo la KISWAHILI ngazi ya Sekondari mapema mwaka 2003 pale Sinza Tower Secondary School pamoja na Dar es Salaam Intenational School.  

Mwanakwetu kama mwalimu wa Kiswahili wakati huo alikuwa anatumia Jina la Abdallah Kibadeni katika matini zake kadhaa kufundishia somo hili.

Kwa mfan; Abdallah Kibadeni mwaka 1977 alifunga mabao matatu peke yake dhidi ya Yanga, Abdallah Kibadeni sasa anafundisha Mpira wa Miguu… NK.

Wanafunzi wakawa  wanacheka wanasema Mwalimu Makwega ni Simba, mbona hata siku moja hamtaji Charles Bonifase Mkwasa?

Ndipo wanafunzi wa Sinza Tower Secondary Agosti 2003 wakati wanaigiza sehemu ya mchezo wa kuigiza wa ZIZIMO ambapo Mwanakwetu na wanafunzi wa SINZA TOWER wakiwa miongoni mwa washiriki walimwambia Mwanakwetu kuwa huyu Latifa Kibadeni ni binti Abdallah Kibadeni King Mputa.”

Msomaji haya makala ni Oktoba 10 na Oktoba 11, 2025

Nina hakika msomaji wangu umejifunza kitu juu ya Mwanasoka huyu wa Tanzania na familia yake . Makala haya yanampa pongezi na Hongera Sana Abdallah Kibadeni mzaliwa wa Mbagala kwa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa Oktoba 11 ya kila mwaka.

Mwanakwetu upo?

 Abdalla Kibadeni Mngindo Aliyebatizwa Ungoni

Nakutakia siku njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257

NB. MAKALA HAYA NI MAALUMU KWA WAKAZI WA ASILI WA MBAGAL NA  YAKIANDIKWA PIA KWA HESHIMA YA NDUGU YETU ABDALLAH KIBADENI. KING MPUTA.

 
























NYERERE NA RASHIDI KAWAWA


SOFIA KAWAWA

0/Post a Comment/Comments