Oktoba 31, 2025 majira ya saa nane Mchana Mwanakwetu alijulishwa kuwa mwanahabari Asha Shabaan kuwa alipata ajali akiwa anatoka katika harakati za kufunga Kampeni ya uchaguzi mwishoni mwa Oktoba, 2025 wakati akitokea Bunda mkoani Mara.
Mwanakwetu alikwenda kumuona Asha Shaaban ambaye aliyekuwa amelazwa hospitali ya Manispaa ya Musoma wodi namba moja.
“Asha Shabaan ni mwakilishi wa ZBC na East Africa TV hapa Mkoani Mara.”
Mwanakwetu akiwa hapa Hospitali ya Manispaa ya Musoma alikutana na Mchungaji mmoja aliyekwenda kumuona mwanahabari huyu aliyefika kumuona Asha Shaaban, huku Mchungaji huyu alimtania Asha Shaaban kuwa kama upo mzima na kiuno chako hakijapata itilafu hilo siyo tatizo, siwezi kukupa talaka.
Walikuwepo hapa walicheka sana na hata Asha Shabaan mwenyewe alicheka sana nayeye mchungaji kusalisha kidogo kisha kusema mgonjwa wetu anaendelea vizuri.Kisha Mwanakwetu kubeba kilichochake na kuanza kurudi zake kwake.Mwanakwetu akiwa njiani aliwoana Vijana wa Jeshi la Wananchi Tanzania JWTZ.
Baadaye Mwanakwetu alifanya mawasiliano na wadau kadhaa juu ya maandamano katika mikoa mbalimbali ya Tanzania.Kwanza alilipokea jambo hili na hapa Mwanakwetu analileta kama lilivyo;
“…tukiupenda ukweli utatuweka huru, Tume Huru ya Uchaguzi inacheza ngoma ambayo haieleweki na mtu yoyote yule, katika vituo watu hawajajitokeza na vituo vingi katika kitabu cha kura 50, havikuweza kumalizika, haya matokeo yanayotangazwa yanatoka wapi? Madaraka ni mali ya jamii nzima tujifunze kushare madaraka(tujifunze kuchangia madaraka) na wengine hilo ndilo la msingi kwa sasa vinginevyo ni hatari…”
Ndugu huyu aliitazama hali hii na haya ni baadhi ya maoni yake juu ya hali ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka wa 2025 huku akisema Tume Huru ya Uchaguzi Yenyewe Imejiloga.
Mdau mwingine alikuwa huyu;
“Mabomu ni mengi sana hali ni mbaya na jana kuna Mjumbe wa CCM na wengine wawili waliuwawa, sasa leo tunataka kuzika wakasema hapana maiti hizi hazizikwi na sisi raia wanazika wao wenyewe, jana Aljazeera wamesema watu mia saba wamekufa. Yaani hii ya Oktoba 30, 2025 huyu mjumbe na wenzake hapo hawajahesabiwa toba ilahi ,yaani nje ukisikia gari tambua ni ya polisi. Unajua sisi Watanzania hatujazoea kuishi maisha haya.
Hauwezi hata kuchungulia dirishani, jeshi watufanyie msamaha katika hili. Shida ya wananchi ni kuendelea CCM lakini Jeshi likisema linachukua nchi wananchi wengine watatoka na nguo moja nje kushangilia. Sasa naona Mkuu wa Majeshi yupo upande ule ule! Masafu Namtume!, Mkuu wa Majeshi Simuelewi kabisa. Huko Arusha nasikia Paul Makonda kakabwa koo watu hawamtaki. Unajua tatizo mama na timu yake na huyu Kikwete, tatizo wala siyo CCM…”
Mama huyu aliongeza mengi juu ya hali .Kwa hakika Watanzania wanaipenda nchi yao na ndiyo maana wanayatoa haya ya moyoni mwao;
“Nasikia Mlongazila wanawatibia vizuri wale majeruhi katika haya maandamano, hili ni jambo zuri maana shida zetu ndizo zinazosababisha haya yote…mtu anaandamana haioni nafuu ya leo wala ya jana wala ya kesho, watoto wamesoma hawana kazi…”
Msomaji wangu haya ni machache tu kati ya mengi ya jioni ya Oktoba 31, 2025 ambapo Mwanakwetu alijaliwa kuyakusanya tu.
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
Kwa leo Mwanakwetu hana la kuongeza bali ni kile alichojaliwa kukiokota tu pande kadhaa za Tanzania. Kwa kuwa Mwanakwetu amemtaja mwanahabri Asha Shabaan aliyeumiwa katika ajali huko Mara na wale wote wanaomua katika kadhia hii anawaombea Mungu wapate taafifu mapema, huku wale walifariki Mungu awajalie pumziko la milele.
Mwanakwetu upo ?Kumbuka;
“Nasikia Mlonganzila Wanawatibu Vizuri Majeruhi.”
Nakutakia Siku Njema.
0717649257






Post a Comment