Adeladius Makwega
Kwa hakika siku ya Oktoba 29, 2025 ilikuwa bado na haya yalikuwa majira ya tangu saa Moja usiku hadi Sita usiku kuyamaliza yale masaa 24.
Mwanakwetu alikuwa nyumbani kwake, huku akifuatilia kinachoendelea kupitia macho na masikio yake, kwa hakika nyumba aliyolala mageti yalifungwa mapema mno, taa zikiwa zimezimwa.
Nyumba hii ilikuwa kimya, japokuwa nje kuna barabara kubwa mbili lakini hakukusikika milio yoyote ile, iwe ya bodaboda au magari.
Saa ya kimwekumweku ya Mwanakwetu ilikuwa inakimbia kwa kasi kubwa na majira ya kati ya saa tatu hadi nne kulikisikika vishindo vikubwa ambavyo vilimshitua mno Mwanakwetu lakini hakuweza kufahamu ni nini lakini masiko ya Mwanakwetu yatabaki kuwa shahidi wa kusikia KISHINDO HICHO mithili ya bomu.
Mwanakwetu akiwa kwake alitaka kujua hali ikoje kwa maeneo mengine?Mwanakwetu alitaka kujua hali ikoje maeneo mengine ya Tanzania.Kutoka Dar es Salaam, Tanga, na Morogoro kwanza yalisemwa haya;
“Nimezunguka vituo kadhaa vya kupiga kura Watumishi wa Tume Huru hadi wananasinzia, watu hakuna. Hata hao tume wanapotangaza wajitafakri wasije wakaingia katika shida.
Watu wamekaa katika majumb a yao wanahesabu idadi ya wapiga kura wanakwenda kupiga kura huku wakiwekeana zamu ya kuhesabu,
‘…wewe umehesabu hadi ngapi? Mim hadi 13 haya naanza na 14 sawa sawa…’
Mathalani kituo kina wapiga kura 400 wanaojitokeza 40 kisha wewe tume utangaze mshinde kapata kura 390 umezitoa wapi?
Wewe uliyesimamie ukisema uitwe mbele ya eneo la kituo uoneshe walijitokeza na mtaa mzima uje utakuwa salama? Tume huru ya uchaguzi haitakuwa salama?
‘Unajua CCM ilifanya kosa kutoka kura za maoni ,watu walipewa rushwa kubwa tangu 50,000/- hadi shilingi 500,000/= kwa mjumbe mmoja, kwa kila mjumbe kwa kura za Diwani na Mbunge.
Baada ya jamaa kushinda kura za maoni walitakiwa kumalizia kiasi hicho hicho kwa wahusika, hilo halikufanyika, Wajumbe wa CCM wakawa na kinyongo.
Wamedanganywa, nakwambia hata wenyewe CCM hawakupiga kura na hata wananchi wengine hawajajitokeza kabisa.’
Ukisema matokeo haya yachunguzwe wasimamizi wa mwaka 2025 wote watafungwa mchana kweupe, wapo waliokataa kazi ya kusimamia uchaguzi huu shida katika kazi hii ni haya mambo ya kuhusishwa na udanyanyifu.
Wako vijana walikataa hii kazi ya kusimamia uchaguzi na hata kuwa mawakala wa CCM kuhofia haya yaliyotokea.
Jambo la kushangaza hata wanawake hawajajitokeza kabisa kupiga kura ambalo hilo ni jambo la ajabu mno kwa Tanzania, hapa kwetu alikuja Makamu wa Rais, Mkutano wako haukuwa na watu , tumehangaika kuzunguka mashleni na kuwavisha nguo za CCM wanafunzi wakati mwaka wa 2020 hapa alikuja Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa Majaliwa hadi ngazi ya Kata kuwaombea/ kumuombea kura diwani watu walijaa, kwanini hali sasa ni tete?”
Ndugu mwingine aliyasema haya;
“Haya mambo yalipaswa kuwekewa udhibiti tangu mwazo, wewe umepata bahati ya kuongoza hiyo miaka mitano, sijui minne inatosha sana, Watanzania hawajakuweka akilini wewe kuongoza zaidi, hivyo angeelewa hili.
Unafanya mabadiliko kila mara, unamtoa kiongozi mzuri unamuweka kiongozi mbaya, mtu unamtoa kwao unamuhamishia mbali! Huko ataweza kufanya kazi na hata kufanya maendeleo yake?”
Mwanakwetu ana ndugu wengi hata ACT WAZALENDO wapo, huku walioshiriki uchaguzi huu na sasa wakijuta kiranga kilichofanya washiriki.
“Viongozi wa ACT wametuchuuza sana, heri tisingeshiriki uchaguzi huu wa mwaka wa 2025 maana hali ni mbaya , mimi nimewakuta walimu wangu walionifundisha wakifanya udanganyfu wa kura, nimewarekodi hawakuwana na kusema hii hali haifai ni mbaya sana na haikubaliliki.”
Unajua hata hili la kusema wananchi walale saa 12 ya jioni ni kosa , hili linavipa nafasi vikundi vya vurugu kuratibu vizuri mambo yao hili ni kosa sana.
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
Msomaji wangu haya yote ni ya saa moja hadi saa sita usiku wa Oktoba 29, 2025 na bila ya shaka na wewe msomaji wangu unayo mengi uliyoyaona, kuyashuhdia na hata kusimuliwa hapo ulipo juu ya siku hii nchini Tanzania.
Mwanakwetu upo?Kumbuka.
“MITANO SIJUI MINNE MIAKA ILIMTOSHA.”
Nakutakia siku njema.
0717649257
Post a Comment