KAKA NIMESOMA VETA

 



Adeladius Makwega-Musoma MARA

VETA mkoa wa Mara, Oktoba 2, 2025 imesema kuwa ajali za vyombo vya moto huhusani bodaboda zinapungua kutokana na sasa vijana wengi wa kanda ya ziwa wanapata mafunzo kutoka taasisi hii ya umma, hiyo basi VETA imesaidia mno kuokoa uhai wa abiria, uhai wa watembea kwa miguu na wengine wengi wanaotumia vyombo mbalimbali vya moto.

“Vijana wetu wasibakie vijiweni, waje kujifunza VETA, majengo yale ni kwa ajili yenu, nawaombeni nyinyi kama wazazi, nyinyi kama walezi, nyinyi kama vijana VETA milango yetu ipo wazi ili vijana wetu waweze kupata mafunzo waje kujiajili.”

Haya yanasemwa na Martini Samingo Moleli Mkuu wa Chuo cha VETA mkoa wa Mara katika kongamano la Wafanyabiashara ndogo hapa Musoma Mjini ambalo limehudhuliwa na wafanyabiashara karibu 200.

“Kwa sasa VETA inaendelea na mapambano makubwa ya kuipa jamii ujuzi wa aina mbalimbali ambapo unamuwezesha Mtanzania kuweza kuendesha maisha yake na kujiingizia kipato kwa kozi za aina mbalimbali ambazo kwa mtazamo wa kaiwada zilikuwa zinachukuliwa kuwa siyo kazi muhimu mathalani ususi, upishi, upambaji na ushonaji lakini sasa VETA imezipa uhai mkubwa shughuli hizi katika jamii zetu.

Ukitazama huu ukumbi umepambwa vizuri kwa rangi nzuri na mpambaji wetu ambaye amesoma VETA hapa hapa Musoma, tazama hili bango mbele limesainifiwa na msanifu aliyesoma VETA hapa hapa Musoma, huu ni ushahidi tosha kuwa VETA sasa ndiyo kinara wa vijana wa Kitanzania kujiajili.”

Kongamano hili lilitoa upendeleo maalumu kwa mkufunzi Faraja Shugha Mwampashi pia kutoka VETA kutoa mada maalumu juu ya shughuli zao.

“VETA sasa ndilo kimbilio langu mimi na wewe, kikubwa tunawakaribisha kufika chuoni kwetu ili muweze kujua vijana wetu wanaweza kujifunza nini, VETA tuna kozi za aina mbalimbali.”

Akizungumza kandoni mwa Kongomano hili Afisa Vijana Mkoa wa Mara Fidel Balaghaye alisema kuwa anawashukuru mno taasisi zote zilizomo mkoa wa Mara ambazo zinashiriki makongamano haya ya Wafanyabiashara ndondogo mkoani Mara wakiwamo TRA, VETA, benki kadhaa na taasisi zingine zinazoshiriki Kongamano hili ambalo limekuwa linafanyika katika wilaya zote za mkoa wa Mara kwa majuma mawili sasa.


 

Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?

Mtayarishaji wa makala haya wakati alipokuwa anatoka katika kongomano alipanda bodaboda ambapo umbali kama wa mita 50 hivi alikutana taswira ya karakana ya vijana wakichomelea milango, madirisha ya nyumba kadhaa, alipoona hili akasema moyoni kuwa kuchomelea huko mageti haya kulionesha kuwa VETA inaendelea kushamiri kwa kutoa ujuzi kwa vijana wetu wa Kitanzania. Mwandishi alimuuliza dereva wa bodaboda aliyopanda,

“Kaka umesoma VETA?”

Kijana huyu maarufu kama DKT DREI alijibu ;

Kama nimesoma VETA udereva wa bodaboda na nilitumie juma moja na gharama ilikuwa ni shlingi 20,000/ tu.”

Jambo zuri ambalo Mwanakwetu anapenda kuwajulisha wasomaji wa makala haya kuwa Bi Faraja Shugha Mwampashi ni dada wa Mwanakwetu na makala haya yameandikwa kwa heshima zote kwa VETA Tanzania na kwa Bi Faraja Shugha Mwampashi dada wa MwAnAkWeTu, Mwanakwetu tajiri wa madada.

Mwanakwetu upo? Kumbuka

“KAKA NIMESOMA VETA.”

Nakutakia siku njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257






 



























 

0/Post a Comment/Comments