JICHO LISILO NA RETINA

Adeladius Makwega-MBAGALA

“Wanaoitazama hali hii wanakwenda mbali sana huku wanatilia mashaka hata uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri DART David Kafulila, wanaipiga mbiu ya mgambo kuwa Kafulila hana uwezo wa kuifanya kazi hiyo, huku ikipitiwa kwa kina namna alivyokuwa Katibu Tawala na Mkuu wa Mkoa ameonesha umahiri gani? Huo umahiri utajwe hadharani. Nani kamdanganya Rais Samia kwamba Davidi Kafulila ana uwezo wa kuishauri chochote juu ya mwendokasi?

Hapa angetafutwa mwana Dar es salaam anayelijua jiji hili aifanye KAZI hii, siyo Kafulula. Binafsi nimefanya KAZI na huyu ndugu anatabia ya kuwatisha watumishi na kukimbiia kushitaki ngazi za juu. Nakumbuka visa viwili vya madaktari wa binadamu nasema uteuzi wa Kafulila tunekosea na kutukosea sisi watu wa DSM.

Mradi wetu wa mabasi hauwezi kufanya vizuri chini ya ushauri wa mwenyekiti Kafulula KAZI hii imemzidi kimo…Kwa hakika Rais Samia Suluhu Hassan ili aweze kuyafikia malengo ya utawala wake inaonekana wazi kuwa mlango wake mmoja umefungwa, hasa wenye jicho la watu walio chini.”

Haya ni maelezo katika makala iliyopewa anuani Tunazaa Mbumbumbu Mzungu wa Reli. Kwa hakika siku ya leo ni vizuri msomaji wangu afahamu BODI ya Ushauri ni nini? 

Kwa mujibu wa Msajili wa Hazina wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia anasema maneno haya;

“Kila taasisi ya umma inatakiwa kuwa na Bodi ya Wakurugenzi au Bodi ya Ushauri ambayo ndiyo JICHO la Mwenye Hisa (Serikali).

Bodi hizo zipo kwa mujibu wa Sheria zilizounda taasisi au mashirika hayo.”

Maelezo haya ni ya Msajili wa Hazina, yako wazi na hakuna hata haja ya kwenda kwenye sheria ya kuunda taasisi yoyote ile. Kikubwa mimi na wewe kwanza tufahamu kazi ya jicho ni nini? Je elimu ya Viumbe hai inasema nini?

“Kazi za macho ya kiume hai chochte kile ni kutoa uwezo wa kuona kwa kugundua mwanga, jambo linalotuwezesha kuona maumbo, rangi, mwendo na kina. Macho pia husaidia katika kujielekeza kwenye mazingira yetu, kutambua vitu, na hata kuchangia katika kudhibiti mzunguko wa usingizi (circadian rhythm) na usawa wa mwili. Macho, yakishirikiana na ubongo, hushughulikia taarifa hizi za kuona ili kutengeneza taswira kamili ya ulimwengu unaotuzunguka.

Jinsi Jicho Linavyofanya Kazi;

Kwanza kuna Utambuzi wa Mwanga: Mwanga huakisiwa kutoka kwa vitu na kuingia kwenye jicho kupitia kornea. Pili ni Uelekezaji wa Mwanga: Kornea na lenzi huuelekeza mwanga huu kwenye retina, ambayo ipo nyuma ya jicho. Tatu ni Ubadilishaji wa Ishara, hapa Retina ina seli nyeti kwa mwanga ambazo hubadilisha mwanga kuwa ishara za umeme. Mwisho Usafirishaji wa Ishara hapa Ishara hizi za umeme husafiri kupitia neva ya macho (optic nerve) kuelekea kwenye ubongo ndipo hapa binadamu uona kile alichokitazama.”

Msomaji wangu kumbuka maneno ya Msajili wa Hazina kuwa bodi hiyo Ndiyo Jicho la mwenye hisa, maana yake ni serikali ambapo ni mimi na wewe, huyu rais wetu anafanya uteuzi kwa niaba ya Watu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yaani mimi na wewe.

 


Swali hili la leo ambalo ndilo linaloyajenga makala haya ni moja, Je Uteuzi wa Davidi Kafulila kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Mwendokasi ni sahihi? Bila ya kuyauma maneno uteuzi wa Kafulila kuiongoza bodi hii haukuwa sahihi. Mwanakwetu ninasema haya kwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa taasisi ni sawa na RETINA ya jicho la binadamu ambao kazi yake ni hii;

“Kazi kuu ya retina ni kubadilisha mwanga kuwa ishara za neva, ikifanya kazi kama filamu katika kamera. Ina seli maalum nyeti kwa mwanga zinazoitwa vipokezi vya mwanga (rods na cones) ambavyo hubadilisha nishati ya mwanga kuwa ishara za umeme. Ishara hizi huchakatwa na seli nyingine za neva za retina na kisha hutumwa kwenye ubongo kupitia neva ya macho (optic nerve), ambako hutafsiriwa kuwa picha, na hivyo kutuwezesha kuona rangi, maumbo, na mwendo.”

Kwa maelezo haya hasa wale walisoma elimu ya viumbe hai ambalo ni somo la lazima kidato cha kwanza hadi cha nne wanaelewa vizuri na hata wale waliosoma Photo Journalism wanaelewa sana. Kumbukeni hili/watambue kuwa RETINA inafanya kazi kama FILAMU, ndiyo kusema retina ikiwa na shida ni changamoto kubwa kwa binadamu kuweza kuona na sawa na kamera isiyo filamu ambapo hakuna picha. 


 

Swali la pili Je ndani ya Mwendokasi Filamu/Retina yetu ikoje? Mwanakwetu alikiokota kisa hiki cha kweli juu ya FILAMU BIN RETINA YA MWENDOKASI.

“Halmashauri moja mkoani Songwe ilikuwa Mganga Mkuu wa Wilaya anayefahamika kama Dokta Abdul Mshana mwenye asili ya Mkoa wa Kilimanjaro, kijana huyu alikuwa mchapakazi sana, daktari mbingwa akiwa wilayani humo aliweza kujenga vituo vingi vya afya enzi ya Rais John Pombe Magufuli. Baadaye Mkurugenzi Mtendaji akapokea barua kutoka TAMISEMI ikumujulisha kuwa Dkt. Abdul Mshana amepangiwa majukumu mengine huko Kilimanjaro na siyo tena Mganga Mkuu wa Wilaya kurudi kuwa daktari wa kawaida. Mkurugenzi Mtendaji akahoji wa Afisa Utumishi -Wilaya kuna nini kimetokea? Halikupatikana jibu/ Wakuu wa idara wakawa wanashangaa hapa mwenzetu kafanya nini? Mbona Dkt Mshana anajituma sana? Watumishi wamepata taharuki. Dkt Mshana akawa anafanya makabidhiano, akamuachia ofisi mama mmoja Daktari anayeshugulikia KIFUA KIKUU kisha yeye kuondoka zake.

Mkurugenzi Mtendaji akamfuata Mganga Mkuu wa Mkoa –Kijana Kagera , akumuuliza kulikoni? Wewe ndiye unayesimamia amsauala ya afya Mkoa huu? Mganga Mkuu wa Mkoa hakuwa na majibu nay eye akawa anashangaa. Mkurugenzi akaenda kwa Katiba Tawala akamuuliza unatambua chochote juu ya maamuzi ya Wizara dhidi ya Dkt Abdul Mshana? Katibu Tawala alijibu ; ‘Ndiyo, yule mimi nilienda kutembelea kituo cha afya Isansa, nimefika pale namuuliza maswali akawa hanijibu vizuri…’ Mkurugenzi akasema ‘Mkuu sawa lakini ulikuwa na wajibu wa kutuambia na sisi, haya mambo, unaweza kuona Abdul Mshana siyo mzuri katika kuongea sana, lakini lakini yeye ni Daktari Bingwa na mahiri wa masuala ya afya, kuongea siyo kigezo pekee vipi vingine vingine? Tunawakatisha tamaa watumishi wa umma. Anapoondoka Dokta Mshana tambua Bingwa ameondoka baadhi ya kesi za wagonjwa tulizokuwa tunamtumia huduma hii tutaikosa. Mkuu tushirikishane haya mambo ya watu.’

Katibu Tawala akasema nchini hii ina wenyewe wewe unaongea kama nani? Mkurugenzi Mtendaji akasema, ‘Nchi hii ni watu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo ni mimi na wewe au hao wenyewe kina nani? Kama wapo waje kutibu badala Dkt Abdul Mshana?’ Palikuwa na tmbu za maneno lakini baadaye Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Songwe Mzee Mkola aliingilia kati lakini tayari Dkt Abdul Mshana alishashushwa cheo. Baadaye Halmashauari hii ilipata Daktari mwingine. Mkrugenzi Mtendaji hakuishia hapo alikwenda Kwa Katibu Mkuu TAMISEMI, Katibu Mkuu TAMISEMI akasema masuala ya Afya anayeyasimamia vizuri ni Dkt. Zainab Chaula Naibu Katibu TAMISEMI anashughulikia Afya. Mkurugenzi  kigulu na njia hadi hodi kwa Dkt Zainab Chaula na majibu ya Dkt Chaula yalikuwa haya, ‘Haya mambo Mkurugenzi wangu ninayekufahamu y anatoka huko huko kwenu, hawa akina Abdul na hata yule Mganga Mkuu wa Mkoa ni madaktari wezangu natambua umahiri wao hasa yule RMO wenu na Songwe mna bahati nzuri sana sijui shida ni nini? Mganga Mkuu wa Mkoa ni kijana mchapakazi kwa kuwa Mkurugenzi Umekuja na haujawahi kuja ofisini kwangu kwa suala lolote lile muache Dkt Mshana aende akaripoti huko Kilimanjaro lakini nitajua la kufanya baadaye…”

Haikupita muda, hata huyu Mganga Mkuu wa Mkoa ambaye Dkt Zainabu Chaula alimtaji kuwa RMO (Kijana Kutoka Kagera) makini alishushwa cheo yale yale yaliyomkuta Dkt .Abdul Mshana, kwa maamuzi ya Katibu Tawala ,yote haya msomaji wangu ni ya Bwana RETINA BIN FILAMU. Baadaye Dk Zainab Chaula mama mmoja muuungwana najua alibaini shida ipo wapi katika mkoa ule.


 

Anayesimulia kisa hiki anasema Dkt Abdul sasa ni Mganga Mkuu wa Wilaya na hata yule Mganga Mkuu wa Mkoa aliyeshushwa Cheo sasa ni Mganga Mkuu wa Mkoa huko Kusini mwa Tanzania.

Mwanakwetu anasema nini sIku ya leo?

Hii ndiyo Retina ya jicho letu Filamu ya Kamera yetu. Retina Bin Filamu nzuri lazima iwe tabia kulea, tabia ya huruma , tabia ya ubaba kwa wale walio chini, siyo kumpigia magoti aliyekuchagua tu na kumpa shikamoo , shikamoo ya kweli ni kuwaheshimu wenye mamlaka yao ambao ni wananchi.

Mwenyekiti wa Bodi ya ushauri ya Mwendokasi anapaswa kuwa mtu maybe amewahi kuishi maisha Dar es Salaam kama mwanafunzi kama mtumishi, kama diwani, Kama Meya, kama mbunge kama Katibu Tawala , Kam Mkuu wa Mkoa ambaye Dar es Salaam au Mkoa wa Pwani ni nyumbani kwao.Vinginevyo Mwendokasi Inapelekwa Machakani.


 

Mwanakwetu Upo?

Je Makala haya yaotwaje? Mwendokasi Yapelekwa Machakani? Filamu Bin Retina? au Kamera Isiyo Filamu Jicho Lisilo na Retina? Mwanakwetu anachagua Jicho Lisilo na Retina.

Nakutakia Siku Njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257
















 



0/Post a Comment/Comments