HUMPHREY POLEPOLE ABDALLAH HANGA MWINGINE

 


Adeladius Makwega-MBAGALA.

Kwa muda wa siku mbili, tangu kutekwa aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Kuba, ndugu yetu Humphrey Polepole MwAnAkWeTu amekuwa na tafakari kubwa juu ya hali ya siasa za Tanzania kwa sasa, akijiuliza Mwenyezi Mungu ananini na sie Watanganyika?

“Jamani Tumefanya kosa gani katika hii ardhi ambayo hatukuomba kuzaliwa juu yake?”

Ukimya huu ulifanya hata ndugu yangu yake mmoja wa karibu kuwasiliana na huyu mwana wa Mbagala na kumueleza kwa kifupi juu ya hali hii anayoiona kwa Tanganyika iliyounga na Zanzibar mwaka 1964.

Akiwa katika tafakari hii binafsi MwAnAkWeTu alikumbuka makala moja aliyoisoma miaka mingi nyuma yaani mwaka 2012 akiwa chumba cha habari cha Shirika la Utangazaji la Ujerumani ambayo ilikuwa inaandikwa na mtu maarufu sana mwenye asili ya Zanzibar juu ya Zanzibar na Tanganyika muda mfupi baada ya kuungana Ahmed Rajabu , ambapo sehemu ya makala haya yalisema maneno haya;

“Ninavokumbuka mimi, Oscar Kambona akatuwambia, ‘Sikilizeni bwana, mimi nimekuiteni hapa mje mzungumze na ndugu yenu, huyu ndugu yenu na huyu mzee wenu, Abdallah Kassimu Hanga, amekuja hapa na anataka kurudi nyumbani Tanzania, nyumbani kwao Zanzibar. Hajawambia mtu bali bali mimi tu , namimi nimemkataza. Nimemwambia huu siyo wakati mzuri wa kurudi nyumbani, ni bora yeye asiende. Ama angelibaki huko huko West Africa anaokotoka kwa mkewe, au abaki hapa London lakini kakataa katakata anataka kurudi nyumbani kwa lazima na mie nina hofu na maisha yake kuwa akifika kule hatoweza kupata salama. Kwanza kwa kuwa yeye amefikia kwangu, anajulikana na inafahamika wazi kuwa yeye na mimi ni rafiki, Julius Nyerere atajua tu zaidi/uzuri hayo kuwa mimi tangu zamani tukiwa Tanzania tunaelewana sana  Abdallah Kassimu Hanga ndugu yenu, tunasikilizana mimi na ndugu huyu… Kwa hali hiyo mimi namwambia hapa na yeye Abdallah Hanga anasema hana ugomvi na Julius Nyerere amekata shauri ya kurudi nyumbani Tanzania…Sasa mimi nimekwiteni mzungumze naye, mseme naye.’ Akatuchukua akatupeleka kwenye chumba alipo Abadallah Kassimu Hanga…”

 

Kwa uhakika Abdallah Kassimu Hanga ni jina geni kwa sasa nchini Tanzania lakini ni miongoni mwa Watanzania makini akiwa na taalumu ya ualimu ambaye alikuwa Makamu wa Rais wa Zanzibar tangu mwaka 1964 hadi mwaka 1967 ambapo baadaye alichaguliwa kuwa Balozi wa Tanzania huko Afrika Magharibi na baadaye kurudi nchini Tanzania alikutana na Mwalimu Julius Nyerere na baadaye kukabidhiwa kwa mamlaka ya Zanzibar ya Abeid Karume na haijulikana kama alinyongwa wala nini maana hata kaburi lake halijulikani lilipo , kukiwa na madaia kuwa aliuwawa kwa tuhuma za kutaka kumpindua Sheikh Abeid Amani Karume, huku ikidaiwa kuwa mauwaji haya yalifanyika bila ya kupelekwa mahakama yoyote ile.

 

Maelezo ya Ahmed Rajabu yanaonesha namna walivyoiona hataria ya  maisha Abdallah Kassimu Hanga kurudi Tanzania baada ya kuisiwa kuwa alikuwa akifanya njama hiyo na ndiyo maana aliyekuwa Katibu Mkuu wa TANU ambaye baadaye akilimbilia uhamishoni Uingereza Oscar Kambona aliona mashaka makubwa ya Abdallah Kassimu Hanga kurudi nyumbani Tanzania na kweli ilikuwa hivyo.

 


 

Mwanakwetu siku ya leo anasema nini?

 

Ukitazama vizuri kisa cha Abadallah Kassimu Hanga kabla ya kukabidhiwa kwa mamlaka ya Zanzibar ya Abeid Karume uliitishwa Mkutano Viwanja vya Jangwani ambapo Julius Nyerere alisema maneno kadha dhidi ya Abdallah Kassimu Hanga ambapo badaye inadaiwa kuwa alikabidhiwa kwa Karume na ndipo ulipokuwa mwisho wake.

 

Huku baadhi Wakatoliki wakimlaumu mno Julius Nyerere kwa kumkabidhi Abadallah Kassimu Hanga kwa upande ambao ulikuwa wa mahasimu wake, akijua  fika kuwa Hanga anaugomvi na Karume. Wakatoliki hawa wakitumia picha hii anayoonekana Hanga kama yu chini ya ulinzi ya jukwaa analoongelea Nyerere wanahoja hili,

 

“Mwalimu Nyerere hakuwa analinda uhai wa binadamu wezake, wakiamini kuwa kifo cha Hanga ni mambo yanatazamwa kama kutia doa safari ya Mwalimu Julius Nyerere kutangazwa Mtakatifu.”

 

Jambo la Pili ni juu ya namna Abadallah Kassimu Hanga alivyopotea huku MwAnAkWeTu akilitaza jambo hili kuwa Abdallah Kassimu Hanga ndiye kiongozi wa Juu wa Tanzania ambaye aliwa kupotea katika mazingira ya kutatasha hadi kesho hakuna anayelifahamu kaburi lake lilipo.


 

 

Swali ubaoni ni kuwa katika hili la sasa  la kutekwa kwa aliyekuwa Balozi wa Tanzania huko Kuba ndugu Humphrey Polepole je yaweza kuwa muelekeo ule ule Abdallah Kassimu Hanga?

 

Kama mambo yatakuwa hayo hayo Je Tanzania inaandika historia gani juu ya usalama wa Watanzania wote?

Je watoto wetu wa Kitanzania na vijana wanaotaka kufanya siasa wanapaswa kuwa waitikiaji w akila jambo linalosemwa na mkubwa? Je Tanganyika na Zanzibar zilipigania uhuru kwa madhumni gani kama siyo kutoa nafasi ya kila mmoja kutoa mawazo yake kwa uhuru? Swali la mwisho ni Je Humphrey Polepole ni Abdallah Kassimu Hanga Miwngine?

Mwanakwetu upo?Kumbuka;

“Humprey Polepole Abdallah Kassimu Hanga Mwingine.”

Nakutakia Siku Njema

 

makwadeladius@gmail.com

0717649257

 











0/Post a Comment/Comments