Adeladius Makwega-Musoma MARA.
Ni majira ya jioni ya siku ya Jumanne ya Oktoba 7, 2025 Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Alfred Mtambi anapokea ugeni kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ofisini kwake ukiongoza na Meja Jenerali Fadhili Omari Nondo, Mkuu wa Komandi ya Nchi Kavu huku akipongezwa kwa kuwawakilisha vema.
Akizungumza mara baada ya utambulisho wa kina miongoni mwa wapigania dazeni moja wa JWTZ Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Mtambi alisema;
“Mkoa wa Mara upo shwari, mipaka ipo salama, ninanashirikiana vizuri na vikosi vyote vya JWTZ vilivyopo katika mkoa huu.”
Akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mara naye Mkuu wa Kamandi ya Nchi Kavu Meja Jenerali Nondo ambaye ni mrefu na mtu miraba minn , mweupe kidogo akiwa na sura ya duara , mtulivu sana alisema;
“Kwanza pokea salaam za pongezi kutoka kwa Afande CDF anakupongeza kwa kazi nzuri unazofanya hapa mkoani Mara na unatuwakilisha vizuri, Hongera kutuwakilisha vema siye maafande wenzako.”
Kikao hiki cha karibu nusu saa kiliyadili mambo mengi ikiwamo hali ya usalama, changamoto za wavuvi Ziwa Victoria na namna nzuri za kuzitatua.
Kikao hiki pia kilihudhuliwa na Katibu Tawala Mkoa wa Mara Mwalimu Gerald Musabila Kusaya ambapo wakati anakaribisha Mkuu wa Kamandi ya nchi Kavu katika viunga vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Mtambi alisema maneno haya;
“Huyu ndiye Katibu Tawala Mkoa wa Mara, anaitwa Mwalimu Gerald Musabila Kusaya, nayeye ni afande mwenzetu alikuwa Mkuu wa Kikosi cha Kupambana na Dawa za Kulevya lakini yeye hodari sana kumtambua mtu mwenye vifurushi vya dawa za kulevya .”
Meja Jenerali Nondo akacheka sana kisha kuingia katika kikao hiki kilichodumu kwa dakika 27 tu, nayeye Mwanakwetu alikuwa shahidi kuona na shahidi kusikiliza.
0717649257
Post a Comment