WASOMI TANZANIA WANATOA TASWIRA GANI KATIKA KUSIMAMIA MIRADI YA UMMA?

 

Adeladius Makwega-Butiama MARA

Majira ya saa nne na ushehe ya Jumanne ya Septemba 23, 2025 Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Alfred Mtambi anakanyaga ardhi ya Butiama akiwa amevalia suti yake samawati na kofia kichwani. Hapa anashuhudiwa akitoa onyo kali kwa wakandarasi wazawa wanaotekelewza miradi ya umma mkoani Mara wabadilike mara moja, vinginevyo hatokuwa na huruma kwa yoyote yule atakayashindwa kukamilisha miradi ya umma kwa wakati ndani ya mkoa wake.

 

Haya yanatokana na hali ya ujenzi katika Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Julius K Nyerere cha Tekinolojia na Kilimo kilichopo Butiama umbali mchache na kaburi la Mwalimu Julius Nyerere huku baadhi ya ujenzi wa majengo ya taasisi hii kusuasua.

“Hapa ni kuleta utani wa kazi za umma, naagiza RPC awachukue hawa walipo na huyu aliyepo mbali ndani ya saa 48 awe ameshafika ofisini kwangu ili nijue pa kumuhifadhi.”

Kwa hakika mwandishi wa makala haya amewashuhudia Wakuu wa Mikoa wengi ambao wanatokana na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mathalani Kapteni Mstaafu Chiku Galawa pale Songwe, katika ziara zake ilikuwa lazima mtu alale ndani lakini Kanali Mtambi Mpiganaji Mwana Diplomasi na katika kipindi cha mwaka wa 2024- 2025 hajawahi kutoa kauli ya kumtaka RPC awachukue jamaa na kuwaweka ndani lakini Septemba 23, 2025 ametoa kauli hiyo kutokana na hali halisi ilivyokuwa katika taasisi hii ya Elimu ya Juu nchini Tanzania. 

 

Mungu bahati, baadaye wale waliokuwa chini ya ulinzi walimpigia mkurugenzi wao na kutoa ahadi ndani ya saa 48 atakuwa amefika Musoma kuripo katika vyombo vya ulinzi na Usalama na Mkuu wa Mkoa aambiwe.

Katikz ziara hii kidogo Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Mtambi alilidhishwa na hali ya ujenzi wa majengo mengine ya chuo hiki kwa makampuni yanayotoka nchini China ambapo yalikuwa yamefanya kazi nzuri;

“Hapa Makamu Mkuu wa chuo anasema kampuni ya Ujenzi ya CHC imeomba kuongezewa muda kwa siku 75, CHC tena wameomba siku 75 kwa majengo mengine, nao M/S Comfix& Engineering wameomba kuongezwa muda, M/S Shandong Hi Speed wameomba siku 75 na M/S Shandong Hi Speed wameomba tena siku 70 kuongezewa muda kwa mejengo mengine. Kuongezewa muda ni utani na huu ni utani siutaki hapa Mkoani Mara maana najua hata makampuni ya nje huko kwao wanafanya hivyo? Hapa Mkoa wa Mara Sitaki Kuchezwa Shere.”

Akiwa katika ukaguzi huu wa majengo ya taasisi hii ya umma, majengo yanayojengwa ambayo ni ya utawala , mikahawa na mabweni yamepewa utambulisho wa Lot 1, Lot 2, Lot3, Lot 4, Lot 5. 

 

Hali ya ujezni ya mradi huu ambao ni mali ya Wizara ya Elimu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuchelewa kukamilika na wakandarasi hao kuomba muda wa kuongezewa lililibua masuala mengi mjadala kwa walikuwapo katika ziara hii ya Mkuu wa Mkoa wa Mara yakitajwa mambo makuu mawili.

“Kwa sasa Wilayani na Mikoani ipo miradi ya Wizara kadhaa ambayo inatekelezwa na Wizara husika. Miradi hii inahitajika kufuatilia kwa karibu na Wakuu wa Wilaya sambamba na Wakuu wa Mikoa maana hizi ni fedha za wananchi, wasiachiwe watendaji wa wizara, Makatibu Wakuu na Mawaziri peke yao,mfano Bilioni 101 ni mkopo kutoka Benki ya Dunia na lazima utarejeshwa kwa makubaliano yaliyowekwa. Tunakipongeza mno kitendo alichofanya Kanali Mtambi na kuwa mkali katika mradi huu.”

Jambo la pili ambalo lilitajwa ni hili;

“Miradi kutoka kutoka Serikali Kuu mathalani Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Julius K Nyerere inasimamiwa na wasomi,Madaktari wa Falsafa na Maprofesa huku chuo hiki bado hakijakusanya kundi la wanachuo wengi kazi inapaswa kukamilika kwa wakati ili wanafunzi waje kusoma lakini na hawa wasomi wetu hawa walipaswa kuufuatilia mradi huu kwa karibu kila siku inayokwenda kwa Mungu maana wapo jirani na mradi.

Madhaifu haya ya Wakandarassi wazawa yalipaswa kuonwa na Makamu Mkuu wa Chuo, akishirikiana na Mkandarasi Mshauri na maamuzi kufanyika kwa haraka kabla ya Kanali Mtambi kufika katika taasisi hii ya umma.Mathalani MESS n ahata MEMKWA ni miradi ya elimu ilisimamiwa na walimu wa shule za ssingi na sekondari na jamii husika ni ilifanyika vizuri, vipi wasomi wetu wa elimu ya juu?”

Kwa uhakika mwandishi wa makala haya alibaini kuwa;

“Katika yale majengo yanayojengwa na wazara yalikuwa na wafanyakazi wasioozidi dazeni moja huku kukiwa na milio ya vifaa vya ujenzi ya aina moja kama mlio wa nyundo ni nyundo tu; huku majengo yanayojengwa na wakandarasi wageni kulikuwa wafanyakzi wengi, milio kadhaa vifaa vya ujenzi vya aina tofauti, huku kando malori yakishusha vifaa kadhaa vya ujenzi, maana yake watu wako kazini , watu hawako likizo ambapo ilionesha wazi wazi kazi zinafanyika.”

Mjadala huu ulifungwa kwa kusema kuwa wasomi lazima wajitathimini katika miradi yao inanyoendelea kujengwa, Wasomi Tanzania Wanatoa Taswira Gani Katika Kusimamia Miradi ya Umma? Vinginevyo hali itakua mbaya zaidi kama kile kinachoonekana kwa miradi mingine.

 

Mwanakwetu upo ?

 Kumbuka

“Wasomi Tanzania Wanatoa Taswira Gani Katika Kusimamia Miradi ya Umma?”

Nakutakia Siku Njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257

NB Makala haya ya uchambuzi yameandikwa na Adeladius Francis Makwega kama lilivyoandikwa hapo juu ambaye aliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Mara katika ziara hii , akitokea  Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara.






































 

0/Post a Comment/Comments