Adeladius Makwega-MBAGALA
“Unajua MwAnAkWeTu! Haya mambo nilikuwa siyafahamu, lakini siku nilipobaini kuwa wanaoitakia mema Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni wachache nilibadilisha kabisa mwenendo wangu.
Nakwambia wengi tunaowaona hawaitakii mema hii nchi, bali wanajitakia mema wao wenyewe.”
Mwanakwetu hapa yupo makini anamsikiliza ndugu huyu hatua kwa hatua;
“Pale unapojaribu kueleza ukweli wa hali ilivyo ili mambo yabadilike wao wanachofanya, wataanza kukufuatilia, utasikia puuu hadi Musoma, pruuu mpaka Lindi, tiii mpaka Rukwa bila kujali familia yako ipo wapi. Huku kote ni Tanzania lakini wale wengine hawaguswi. Au utasikia huyu jamaa ukimpigia simu hapokei, huyu jamaa haji kazini. Utasikia wanakwambia huyu jamaa ni mlevi.
Utakuta mtu safi atapigwa mizengwe sana, hata watakwimbia huyu jamaa amechanganyikiwa. Kumbe kwa ukweli wa Mungu wao ndiyo wamechanganyikiwa na hawajali maslahi ya walio wengi, pengine huyu anayeambiwa maneno hata pombe hanywi.
Sasa wenye ngozi laini wanakaa kimya na kuungana nao.”
MwAnAkWeTu ndugu yangu mimi nina mifano mingi;
“Kuna wakati halmashauri fulani ilikuwa inajenga OPD katika Hospitali ya Wilaya, anayefanya kazi hii ni Kiongozi wa chama tawala, kazi haifanywi kwa ubora, kelele zikawa nyingi sana.
Kamati ya Bunge ikafika, ikakubali kuwa hali hiyo ni tete, baadaye wakabaini nafasi ya mhusika katika chama, yaani hata kulijadili jambo hilo baada ya kazi ilikuwa vigumu, walikuwa wazito, mjadala ulihamishiwa wilaya nyingine.
Kweli mkataba ulivyunjwa lakini baadaye mhusika akagombea uenyekiti wa chama tawala ngazi ya Mkoa. Watu wakawa na mjadala jina hili linarudi halirudi? Mjadala ukawa mrefu lakini mwisho wa siku chama taifa ikarejesha jina na jamaa na jamaa huyu akashinda akawa mwenyekliti wa Chama Tawala Mkoa. Ndiyo maana nasema wanoitakia mema nchi hii wachache.”
Mwanakwetu unataka nikuongezeee? Hii ni dozi kubwa kama sindan basi ni Kilistapeni.
Mwanakwetu aliagana na huyu ndugu nayeye kwenda zake na kuamua kukuandikia Makala haya.
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
“Tanzania ya Mwalimu Julius Nyerere ilikuwa na kiongozi mwema, mwadilifu aliyewapenda Watanzania nyae ni Edward Moringe Sokoine lakini alifariki kwa ajali ya gari gafla bini vuu, ambapo Moringe Alifariki nikiwa darasa la pili, kubwa hakuweza kudumu nafasini, ama kweli wema hawana maisha.
Tanzania ya Ali Hassan Mwinyi alikuwepo ndugu yetu Augustine Lyatonga Mrema ambapo kipindi hiki Mwanakwetu anakumbuka mno alikuwa ni mwanafunzi wa sekondari, ndugu Mrema alipata changamoto na kuondolewa Uwazirini ati kwamba hakuwa na Colletive Responsibility kisha Mrema na yeye kwenda zake upinzani hasira…Watanzania wakishangaa.
Tanzania ya John Pombe Magufuli ilimpata Rais kabisa na awamu yake ya tano lakini hakumaliza vipindi viwili na kisha kufariki akiwa madarakani…Mungu ana jambo gani na sisi Watanzania? Mungu anataka Watanzania tujifunze nini…? Au ni kweli Ama Kweli Wema Hana Maisha?”
Mwanakwetu anapoandika makala haya je anawajibu wa kuamini kuwa wanaoitakia mema nchi hii ni wachache? Vipi wewe unayeyasoma makala haya je unaitakia mema nchi hii?Au tuendelee kumuomba Mungu aingilie kati? Je wengine waogope kuwa wema kisa wema hawana maisha? Kwa Hakika ninaamini kuwa Wanaoitakia Mema Nchi hii Wachache. Maisha ya binadamu yapo ya duniani na yapo baada ya kuondoka dunia,ninaamini wema wanayo maisha mazuri tena sana baada ya kuondoka duniani.
Mwanakwetu Upo?
Kumbuka
“Wanaoitakia Mema Nchi Hii Wachache.”
Nakutakia siku Njema.
0717649257
Post a Comment