Adeladius Makwega-MBAGALA.
Mwaka wa 2016 mwishoni mwishoni Mwanakwetu alifanya ziara katika Kijijji kimoja ambacho kipo katika Kilimani sana,walifika Lunguza Mjini kisha kuanza kupanda mlima mmoja mkali huku njiani Nissan Prado mali ya Halmashauaria ay Lushoto ambayo ilikuw ana KM chache tangu kununulia kutoka JAPAN ikashindwa kupanda milima huku moshi ukitoka.
Tulishuka ndani ya Motokaa hii kisha kutembea kwa mguu mwendo wa karibu saa nzima. Tulipofika kijijini hapo majira ya jioni wananchi wameshakata tamaa kuwa kama ugeni unafika. Hapo hapo wananchi hawa wapo katika makundi makundi. Faraja ya matumaini iliibuka baada ya kuwaona wageni wanaingia mashati begani yameloana jasho la kupanda mlima.
Kabla ya yote ilitembelewa Zahanati ya Kijiji ambapo ilikuwa na vifaa vyote vya kisasa na magodoro kadhaa ya kulala wagonjwa huku kukiwa na muuguzi mmoja aliyefika hapo kwa miaka mingi nyuma. Akiwa anaishi kama na yeye mzaliwa wa kijiji hiki.
Nikiwa pale zahanati mzee mmoja akaniita kando akaniambia maneno haya,
“Bwaa shemeji! wewe umeo kwetu, hapa shida yetu ni watumishi wa Idara ya Afya yupo mmoja, huku ni mbali, si umeona kilima chetu kilivyo kigumu, gari lako mpya linashindwa kupanda vipi kwa magari yetu mabovu? Tunaomba uongoze watumishi hata wawili. Huyu mama aliyeopa hapa alikuja mdogo, binti kigoli. Akawa kila mara anaomba ruhusa anaondoka anarudi kwao wiki, muda mwingine anaondoka anakwenda Lushoto kuchukua mshahara anakaa huku wiki mbili, zahanati yetu imefungwa. Wazee tukakaa na kulijadili na kukata shauri hadi wa Brigedia Hassan Ngwilizi. Tukiwa katika mjadala huo kwa Ngwilizi kijana wetu mmoja akatufichia aibu na kuamua kumuoa binti huyu na sasa ndiyo maana hadi leo umemkuta hapa, bado anatuhudumia, vinginevyo baba hii zahanati ingeshafungwa,haya magodoro na vitanda alitusaidia Baba Askofu Stephern Munga yule ni ndugu yetu anazaliwa kijiji hiki.”
Baada ya kukaguliwa zahanati hii ukafanyika mkutano na wananchi wa Kijiji cha Tewe kilichopo kata ya Lunguza yenye vijiji vitatu; Tewe, Lunguza na Kivingo, Wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga katika mkutano ule maswali mengi yaliulizwa dhidi ya Serikali, mojawapo lilikuwa hili;
“Wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Mwaka wa 2015 Rais John Pombe Magufuli na Mgombea wake Mwenza Samia Suluhu Hassan walitoa ahadi ya kutoa Trekta moja kila kijiji, swali je mpaka sasa lipo wapi Trekta letu.”
Swali hili lilijibiwa …lakini kumbuka ahadi inajibiwa kwa kutekelezwa kile kilichoahidiwa.
Yule jamaa aliyeookoa jahazi la ndugu zake alikuwa na uwezo kidogo hapa kijijini akiwa na maduka kadhaa duka moja likiwa jirani na Zahanati ya Kijiji cha Tewe. Kwa heshima hii Mwanakwetu alitembeleea duka la muokoa jahazi na kununua soda kisha kuondoka zake.
Katika kijiji cha Tewe Mwanakwetu alipewa zawadi mbalimbali ikiwamo mikugu miwili ya ndizi ambazo zilitumiwa na watumishi ziara kama kifungua kinywa siku iliyofuata kijijini Mnazi. Katika kijiji cha Tewe mtu maarufu sana aliyekuwa mzaliwa wake alikuwa ni Baba Askofu Stephern Munga ambaye wakati huo huo alikuwa Askofu wa Kanisa la Kiinjili na Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Mashariki DKMs.
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
“Zahanati ya Tewe baadaye iliongozewa watumishi watatu. Jambo la pili makala haya yanaandikwa kama kumuadhimisha Baba Askofu Stephern Munga ambapo amefariki dunia hivi karibuni.”
Ndugu msomaji wangu kwa heshima ya Baba Askofu Munga ambaye hatunaya tena niliamua nikupe jambo moja nzuri sana la ndugu zake Baba Askofu Munga kutoka Kijiji cha Tewe, Kata ya Lunguza Wilayani Lushoto, Mkoani Tanga ambapo ndipo anapozaliwa Baba Askofu Stephern Munga ambapo haya yote Mwanakwetu alishuhudia kwa macho yake.
Mwanakwetu upo?
“Vituko vya Ndugu wa Askofu Munga.”
Nakutakia Siku Njema.
0717649257.
Post a Comment