UJENZI MAKAZI YA VIONGOZI UFANYIKE KWA UMAKINI

 

 

Adeladius Makwega-Bweri Musoma MARA

Mapema ya Septemba 25, 2025 Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Evans Alfred Mtambi anatembelea Ujenzi wa Makazi ya Viongozi Bweri Musoma Mjini ambapo ujenzi wake unaendelea hapa Mkoani Mara, chini ya ufadhili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika ziara hii ya Kanali Mtambi anapokelewa na Dominicus Lusasi-Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mara akiwa na Wakuu wa Idara na Vitengo kadhaa.

Kwanza kabisa kiongozi huyu anakagua ujenzi wa mradi huo hatua kwa hatua, akiuliza maswali na kujibiwa. Miongoni mwa majibu ya Mkandarasi Mshauri kutoka TBA, Msanifu Majengo Selestine Kaitaba;

“Mkuu wa Mkoa, ujenzi huo unaendelea vizuri huku Mkandarasi Mjenzi Nice Construction and General Suppliers amekuwa akizingatia vigezo vyote vya ujenzi huu wa Makazi ya Viongozi.”

Nayeye Mkandarasi Mjenzi Injinia Masour Twalibu kwa niaba ya kampuni yake ya Nice Construction and General Suppliers anasema kuwa kazi inaendelea vizuri hatua kwa hatua na wanatarajia kazi hii itakamilika kwa wakati.

Akizungumza katika ukaguzi huu Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Mtambi alikitaja kisa hiki;

“Kuna wakati tulikwenda pahala katika shughuli za Kimataifa, mgeni wetu akafika pahala alipoandaliwa katika jengo hilo lilikuwa la ghorofa kadhaa lakini chumba maalumu yaani VIP kilikuwa juu(ghorafani) lakini mgeni huyu umri ulikuwa umesogea hivyo kushindwa kupanda ngazi kwenda chumba hicho, kilichoamuliwa Mgeni Maalumu alilala chumba cha mlinzi nayeye mlinzi kulala chumba maalumu.

Hiki ni kituko lakini hali ilikuwa hivyo. Sasa  hapa leo hii maagizo yangu kwenu,

‘Kila mnapojenga majengo haya ya viongozi lazima mzingatie vyumba maalumu kuwa katika mazigira yote, kukwepa kutokea tukio kama hili ninalolisimulia.’

Sawa jamani?”

Agizo hili lilipokelewa, Mwanakwetu analiweka katika makala haya ili maeneo mengine ya Tanzania na mataifa mengine wajifunze kutoka na agizo hili na Kanali Evans Mtambi Mkuu wa Mkoa wa Mara yanapojengwa majengo ya namna hii.

 

Ukaguzi wa mradi huu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaendelea kufanyika ambapo baadaye Kanali Mtambi anatoa pongezi wa kampuni inayojenga mradi huu;

“Kampuni hii inafanya kazi nzuri za ujenzi si Mkoani Mara tu, hata katika maeneno mengine, imepewa kazi ya ujenzi wa makazi ya viongozi kwa kufuata taratibu zote huku ufanyaji kazi wake nzuri, umekuwa kivutio ambapo kigezo namba moja ni umahiri wa namna wanavyofanya kazi.”

Haya ni ya ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Mara hapa Bweri Ujenzi wa Makazi ya Viongozi Septemba 25, 2025.





Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?Mwanakwetu anayo mambo makubwa matatu ambayo anamuomba msomaji wake ayazingaite;

Kwanza makazi ya viongozi ni nini?

“Katika baadhi ya mikoa ya Jamhuri ya Muungano huwa kunakuwa na Ikulu Ndogo na mikoa mingine huwa kuna makazi maalumu ya viongozi ambapo viongozi mbalimbali wa kitaifa wanafikia  nandiyo haya yanayojengwa hapa Bweri Musoma Mjini.”

Jambo la pili ni hili, katika masuala ya ujenzi huu kumetajwa misamiati mikubwa mitatu ;

“Msanifu Majengo- yeye ndiye anaandaa mpango mzima wa jengo kabla ya kazi kuanza, kisha anakuja Mkadiliaji Majenzi huyu ndiye anayepiga hesabu za vifaa na gharama zake na huwa ni msomi wa uchumi na pia yupo Mkandarasi Ujenzi huyu ndiye anajenga jengo husika na kukamilika.”

Jambo la tatu na mwisho ambalo Mwanakwetu anapenda msomaji wake alielewe leo hii ni juu ya eneo hili unapofanyika ujenzi huu hapa Bweri Musoma Mjini.

Historia inadokeza kuwa eneo hili lilikuwa ni sehemu ya Musoma Chidren’s Home ambayo lilianza kama kituo cha kulelea watoto yatima waliokotwa au wale waliofiwa na wazazi wao wote wawili.

“Mwaka 1989 Wizara ya Kazi, Utamaduni na Ustawi wa Jamii ilipokea maombi ya Bwana Daniel Granlund ya kujenga kituo cha kulelea Watoto Yatima na Wenye Uhitaji kwa kuwa kulikuwa na uhitaji huo…mapema Mei 22,1989 ombi hili likakubaliwa… wahitaji wa eneo yaani huyu ndugu Grandund na mkewe walihitaji eneo la kufanyia kazi hii ndipo ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara mwaka 1990 iliwapatia eneo hilo… na ujenzi kukamilika mapema mwaka 1994.

Ndugu hawa waliopewa eneo hili walikuwa raia wa kigeni na walifanya kazi chini ya mwavuli wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God of Tanzania lililoko Musoma na walipata leseni ya Musoma Children’s Home na huku uendeshaji wa kazi hii ilitolewa mwaka 1995 huku Serikali ya Finland na Kanisa la Sionforsamlingen I Visa la huko Finland walifadhli ujenzi huo na baadaye kuweza kuanza kutoa huduma hiyo...”

Kwa mujibu wa nyaraka hizo ndugu Granlund walikuwa wazee hivyo basi wakaona umri umekwenda, hawawezi tena kuifanya kazi hii ya malezi na kuamua kurudi kwao. Hapo hapo Kanisa la Evangelistic Assemblies of God (T) wakamtaka Granlund na mkewe wakabidhi mali na eneo hili kwao lakini Bwana Granlund na mkewe wakasema.

“…asanteni sana kwa Kanisa kuliona hili, lakini tunawajibu kuwa eneo hili ni mali zote zilizomo humu ni mali ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, sisi hatuna mamlaka hayo ya kufanya hivyo, kwa hivyo basi tutakabidhi mali hizo kwa Serikali na yenyewe ndiyo itakayoweza kuamua nini juu ya mali hizi…”

Kwlei Februari 8, 2020 kukabidhiwa kwa serikali naye ndugu Granlund, Askofu wa Kanisa husika na mashahidi wa pande zote kuwepo kukiwa na mali kadhaa, majengo na eneo lenye ukubwa wa ekali karibu sita na ushehe ambapo sasa sehemu shughuli hiyo ya malezi ya yatima inaendelea na eneo kiasi(eneo dogo) ndilo makazi haya ya viongozi yanajengwa amabpo ndugu yetu Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Mtambi anakagua ujenzi huu.

Nina hakika msomaji wangu umepata jambo juu la ziara hii ya Mkuu wa Mkoa wa Mara hapa Bweri Septemba 25, 2025.

 

Makala haya yametayarishwa na MwAnAkWeTu kwa heshima ya Serikali ya Finland hasa kutokana na heshima kubwa walionesha raia hawa wa Finland walipokuwa hapa nchini kwa kukabidhi mali hizi kwa Serikali ya Tanzania na kuheshimu viapo vyao na makubaliano yao na serikali ya awali na mali hizi bado zinatunzwa na serikali hadi kesho.

Makala haya yanamnukuu Rais wa Finland katika Bunge la Ulaya kama heshimu kwa taifa hili.

“Asante. Asante sana. Mheshimiwa Rais, ninalihutubia Baraza la Usalama kwa niaba ya nchi za Kaskazini — Sweden, Norway, Iceland, Denmark, na Finland. Huenda nimetunukiwa heshima ya kufanya hivyo kwa sababu Finland inapakana na Urusi kwa urefu wa kilomita 1,340. Sasa, Baraza la Usalama limekuwa na suala la Ukraine katika ajenda yake kwa miaka 11 iliyopita, likiwa na matokeo machache kwenye karatasi na hata machache zaidi katika utekelezaji. Wakati huohuo, iko wazi kwamba Mkutano Mkuu mara kadhaa umelaani kwa wingi kitendo cha uchokozi cha Urusi.”

Mwanakwetu upo?

Kumbuka

“Ujenzi Makazi ya Viongozi Ufanyike Kwa Umakini.”

Nakutakia siku Njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257


  


 






 

 

 

 

 


0/Post a Comment/Comments