Adeladius Makwega-Mukendo Musoma MARA
Katibu Tawala Mkoa wa Mara, Mwalimu Gerald Musabila Kusaya, mapema ya Septemba 29, 2025, amekagua ukarabati mkubwa unaofanyika katika Jengo llinalotumiwa na Hazina Ndogo Mkoa wa Mara, baada ya Ofisi ya Mkoa wa Mara kupokewa shilingi milioni 127.4 kwa kazi hii.
Akifanya ukaguzi wa mradi huu unaojengwa kwa kutumia force account wenye namba RAS/077/2025/2026/NC/13 unaotakiwa kukamilika ndania ya siku 90 tangu Agosti 21, 2025 hadi Novemba 20, 2025 Mwalimu Kusaya alisema;
“Nalidhishwa kwa namna kazi inavyofanyika, nina hakika fundi wetu Peter Kisaka atamaliza kazi hii mapema ili aendelee na kazi zingine za kujenga taifa letu katika maeneo mengine.
Pia naipongeza kamati kwa kusimamia mradi hu vizuri kazi hii iendelee kufanyika vizuri hapa si mbali na mimi mradi huu upo pua na mdomo naufutilia kwa karibu mno.”
Ziara hii ya kuukagua mradi huu iliyotumia karibu dakika 23, huku Katibu Tawala akipita katika kona zote na kukagua maeneo yote yanayofanyiwa ukarabati mkubwa. Mwalimu Kusaya alipita katika kona moja nyembamba sana, nyumbamba mno, huku akimuuliza Mkuu wa Idara ya Miundo Mbinu Ofisi ya Mkuu Mkoa wa Mara Injnia Richard Moshi,
“Injini Hapa Unapita?”
Wakuu wa Idara na Vitengo wakiwa ziarani humo walicheka huku wakilinganisha uchochoro wenyewe unaotajwa na injinia huyu kuweza kupita katika njia hiyo nyembamba kwa Amani. Mwanakwetu aliiutazama uchochoro huu na kuona kabisa Injini Moshi hawezi kupita katika uchochoro huu.
“Tunamshukuru Katibu Tawala kwa kutupongeza kwa namna kazi hii inayofanyika, tuna hakika tutaendelea kuisimamia vizuri na mradi huu utakamilika mapema. Katibu Tawala ametutia moyo na kutupa ari zaidi ya kusimamia ujenzi huu na hata tumeongeza moyo wa kujituma kwa majukumu mengine atakayotupangia .”
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
“Mwanakwetu akiwa katika mradi huu alikutana na vitu viwili vizuri; Kwanza jengo hili linalofanyiwa ukarabati lilijengwa mwaka 1970 likiwa na miaka karibu 50 ambapo huu umri ni sawa na wa Mwanakwetu.”
Jambo la pili ;
“Jengo hili la awali lilikuwa limejengwa kwa kutumia mawe na udogo na likiwa imara sana.”
Kulingana na maelezo ya fundi anayejenga jengo hili Petro Masiga Kisaka alipoulizwa ubora wa ujenzi wa kisasa wa saruji , tofali na mchanga na ule ujenzi wa awali wa udongo na mawe. Ndugu Kisaka alisema kuwa ujenzi wa kutumia mawe na udongo ni imara lakini ni ujenzi wa gharama kubwa kwa kuwa sasa mawe kuyapata ni gharama ndiyo maana maeneo mengi ya Musoma Mjini ambayo yalikuwa na mawe sasa mawe hakuna maana yametumika sana kujengea makazi ya binadamu.
“Ili kufanya mazingira yabakia kuwa salama, kwa sasa ujenzi wa tofali , mchanga na saruji ni wa lazima.
Kwa sasa ujenzi huu una changamoto kubwa hasa kwa mchanga unaotumika kuwa na chumvi chumvi kwa hiyo inahitaji utumie saruji ya kiwango cha juu kinyume chake ni hatari.”
Mwanakwetu upo?
Je makala haya yaitwaje? Ujenzi wa kutumia Saruji Haukwepeki?Ujenzi wa Mawe na Udongo ni Imara au Injini Hapa Unapita? Mwanakwetu anachagua Injini Hapa Unapita?
Nakutakia Siku Njema.
makwadeladius @gmail.com
0717649257

Post a Comment